Choki amalizana na TOT, kuitumikia mwaka na nusu (MAJIRA

Nakandamiza Kibara

Senior Member
Jul 17, 2007
143
10
Na Hastin Liumba, Tabora

MWIMBAJI mahiri wa bendi ya The African Stars 'Tanga Pepeta International'
Ally Choki amejunga rasmi na bendi ya TOT Plus baada ya kusaini mkataba wa
mwaka mmoja na nusu na anatarajiwa kuambatana nayo mkoani Tabora katika
maadhimisho ya uamuzi wa busara wa kura tatu.

Akithibisha hatua hiyo mbele ya waandishi wa habari mjini hapa Mkurugenzi
Mtendaji wa TOT Plus, Jonh Komba alisema hatua hiyo ni katika kujiimarisha
kwa bendi hiyo na kurejesha matumaini ya wapenzi wake.

Alisema Choki alijiunga na kundi hilo Januari 17 mwaka huu na atakuwa
kiongozi wa bendi hiyo na ataanza kuonekana katika maonesho ya maadhimisho
ya uamuzi wa busara wa kura tatu, yanayotarajiwa kufanyika mkoani Tabora.

Alisema hatua hiyo ni katika kujiimarisha kwa kundi hilo ili kurejesha
imani na mashabiki wake na kwamba muziki wa sasa nchini na duniani kwa
ujumla ni huria na kujenga mazingira ya soko.

Ijumaa uongozi wa African Stars Entertainment (ASET) unaomiliki bendi hiyo
ulimuandikia barua Choki ukieleza kuwa mkataba wake na bendi hiyo bado
haujamalizika na pia ana deni linalokadiriwa kufikia sh. milioni 13. Juzi
mwimbaji huyo alikuwepo viwanja vya Leaders Klabu na alipanda jukwaani
wakati bendi hiyo ilipotumbuiza.

Choki alianza kujijengea jina Twanga Pepeta mwaka 2000, baada ya aliyekuwa
kiongozi wa kundi hilo Ramadhan Masanja 'Banzastone' kujiengua na kwenda
TOT, hata hivyo Choki aliachana na Twanga mwaka 2003 alipoanzisha bendi
yake iliyokuwa ikijulikana kama Extra Bongo ambayo ilikufa mwaka 2005.

Choki aliungana na Muumin na kuanzisha Double Extra iliyodumu miezi miwili
tu, baada ya kuzinduliwa, ambapo Choki alikimbilia Mchinga Generation
ambapo pia alikaa muda mfupi na kurudi Twanga mwanzoni mwa mwaka 2006.
 
CCM wanaanza ku divert issue sasa wanazindua upigaji ama wanapongeza uamuzi wa kuwa nakura 3 Chimwaga hebu soma tena hapo juu .

anatarajiwa kuambatana nayo mkoani Tabora katika
maadhimisho ya uamuzi wa busara wa kura tatu.
 
CCM wanaanza ku divert issue sasa wanazindua upigaji ama wanapongeza uamuzi wa kuwa nakura 3 Chimwaga hebu soma tena hapo juu .

anatarajiwa kuambatana nayo mkoani Tabora katika
maadhimisho ya uamuzi wa busara wa kura tatu.

Naomba mwenye uelewa wa maneno hayo anifafanulie "Uamuzi wa busara wa kura tatu" yaani tutapiga kura tatu ni zipi na zipi. Mwisho tutaziita "karata tatu" haya weeeee!!!!!!!
 
Najiuliza hii hama hama ya hawa vijana tatizo ni nini? au ndio hulka yetu wa tanzania?
Mchezo huu naona umeshaota mizizi maofisisni hadi kwenye siasa.

Leo CHADEMA kesho NCCR, ukitoka huko unaingia CCM. Hakuna uzalendo wa kweli!
 
Na mimi naomba msaada kwenye kura 3 hapo .CCM ina mambo sasa wanamwagia zege ?
 
choki hana lake kwa sasa kila mahali kazi kutanga tanga tuu...

abt kura tatu wajimini mbona mie nadhani wana mean kura ya raisi,mbunge na diwani??
lakini 2010 si bado au ndio wanaanza kampeni sasa?
 
choki hana lake kwa sasa kila mahali kazi kutanga tanga tuu...

abt kura tatu wajimini mbona mie nadhani wana mean kura ya raisi,mbunge na diwani??
lakini 2010 si bado au ndio wanaanza kampeni sasa?

HEBU RUDINI KWENYE HISTORIA NYEPESI MLIYOJIFUNZA DARASA LA NNE. HAPA WANAONGELEA MKUTANO WA KIHISTORIA WA TANU ULIOFANYIKA MJINI TABORA MWAKA 1958.
 
Back
Top Bottom