Chochote anachosaini Kiongozi nje ya nchi kiwe 'ceremonial' tu hadi kipitishwe na Bunge

Bora afanye mwenyewe tu na wachache anaowaamini wamsaidie mawazo Tanzania hii hatuna bunge lenye uhalali wa kupitisha chochote kwa Haki.
 
Unamaanisha Nazir Karamagi? Halafu Marekani sio kipimo cha kila kitu kwamba kikiwa chafanyika huko na huku iwe hivyo. Mikataba hadi usainiwe kuna majadiliano marefu yanakuwa yameshafanyika nyuma ya pazia. Hakuna haja ya kuwa na mashaka
 
Niseme sijafuatilia in details mikataba aliyosaini Rais Samia huko Kenya.

Inawezekana kuna hitilafu na inawezekana ni majungu yetu ya kila siku.

Lakini kitu kimoja nilichowahi kukiona Kwa utaratibu wa serikali ya Marekani..huwa nakitamani Sana tukiweke kwenye sheria na katiba yetu.

Ni mikataba yote inayosainiwa na Rais,Makamu,Waziri Mkuu, mawaziri na yeyote Yule Kwa niaba ya Taifa hasa nje ya nje ni kuwa mikataba yeyote ambayo haijapita kwenye Bunge huwa 'sio halali'

Rais anaruhusiwa kusaini mkataba wowote ule popote pale lakini uhalali wake ni mpaka upitishwe na Bunge.

Hili kama Wamarekani wameliona umuhimu wake. Je, sisi Taifa changa?

Hivi Mnakumbuka Mustapha Karamagi alivyowahi kwenda kusaini mikataba ya madini Kwa siri na hotelin nchi ya nje ..usiku wa manane?

Kama tungekuwa na sheria hizi wala tusingeumiza kichwa.

Viongozi hufanya errors nyingi kwenye ziara nje ya nchi..na wasingependa onekana 'vizingiti' vya mahusiano bora Kati ya nchi na nchi lakini zikiwepo sheria
Wala hakuna shida...

Kama hatuna hii sheria basi wabunge huu ndo wakati.

Chochote watakachaosaini Viongozi wetu
Huko nje kinakuwa 'sio halali'hadi kipitiwe na wabunge.
...na kipitishwe Kwa kura..


Wakati wa kudai sheria hizi ndo sasa
Good idea mkuu, but one thing to note wabunge wa chama chake wanaweza kumpinga ??
 
Good idea mkuu, but one thing to note wabunge wa chama chake wanaweza kumpinga ??

Swala si kupinga
Wanaweza kuboresha pia..
Sio kupinga ndo kila kitu ..
Unaweza ukafanyiwa marekebisho kabla ya kupitishwa...
 
Tatizo ni kuwa hatuna bunge kabisa na spika ndiyo hatuna kabisa kama yupo basi ni zumbukuku mzungu wa reli ulimwengu uko huku
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom