Chochote anachosaini Kiongozi nje ya nchi kiwe 'ceremonial' tu hadi kipitishwe na Bunge

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,873
Niseme sijafuatilia in details mikataba aliyosaini Rais Samia huko Kenya.

Inawezekana kuna hitilafu na inawezekana ni majungu yetu ya kila siku.

Lakini kitu kimoja nilichowahi kukiona Kwa utaratibu wa serikali ya Marekani..huwa nakitamani Sana tukiweke kwenye sheria na katiba yetu.

Ni mikataba yote inayosainiwa na Rais, Makamu, Waziri Mkuu, mawaziri na yeyote Yule Kwa niaba ya Taifa hasa nje ya nje ni kuwa mikataba yeyote ambayo haijapita kwenye Bunge huwa 'sio halali'

Rais anaruhusiwa kusaini mkataba wowote ule popote pale lakini uhalali wake ni mpaka upitishwe na Bunge.

Hili kama Wamarekani wameliona umuhimu wake. Je, sisi Taifa changa?

Hivi Mnakumbuka Mustapha Karamagi alivyowahi kwenda kusaini mikataba ya madini Kwa siri na hotelin nchi ya nje usiku wa manane?

Kama tungekuwa na sheria hizi wala tusingeumiza kichwa.

Viongozi hufanya errors nyingi kwenye ziara nje ya nchi na wasingependa onekana 'vizingiti' vya mahusiano bora Kati ya nchi na nchi lakini zikiwepo sheria wala hakuna shida.

Kama hatuna hii sheria basi wabunge huu ndo wakati.

Chochote watakachaosaini viongozi wetu.

Huko nje kinakuwa 'sio halali'hadi kipitiwe na wabunge na kipitishwe Kwa kura.

Wakati wa kudai sheria hizi ndo sasa
 
Hao wanasheria nguli wanatakiwa wawe wanatoa ushauri wa kitaalam kwa rais before signing contracts.

Sielewi kama baada ya Rais kusaini ije irudi kwa ngazi ya bunge tena. Sijui kuhusu organization structure ya huko juu.

Alisaini huko kwa m7 leo anasaini kwa uhuru na hawa wote ni manguli wa siasa na uchumi pia.

Naamini pia wanachukua chance chap kwa kitu walichokitamani before na wakashindwa kupata.
 
Siku zote bunge letu ni rubber stamp tu serikali.

Kinachoamriwa na serikali ndicho hicho hicho kitapita.

Itakuwa ni kupoteza muda na gharama tu za mlipa kodi.

Hata kama lakini majadiliano yataweza kuifanya serikali ione makosa ..
 
Hoja Imeungwa Mkono Changamoto Kubwa Naiona Kwenye Maslahi Ya Taifa Wenye Dhamana Wamelala
AG Apeleke Bill Bungeni.


Ukweli Wanatuingiza Chako Wasomi Wetu
Darasa La Saba Hoyee
 
Kwanini Samia anaonekana dhaifu sana? sasa kwanini wale waliokuwa hawataki awe Rais huko chamani kwao mliwapiga vita wakati walikuwa sahihi?

Kumbe tatizo la nchi yetu sio nani yupo ikulu, tatizo letu ni uwepo wa CCM iliyochoka na kuishiwa mbinu za kutuongoza, hata hilo bunge kibogoyo unalotaka liidhinishe hiyo mikataba nalo lingeipitisha ili kumlinda mwenyekiti wa chama chao, hivyo hii solution yako nayo haisaidii, kama tuliumbwa ili tuchezewe na CCM then I see no way out.
 
Siku zote bunge letu ni rubber stamp tu serikali.

Kinachoamriwa na serikali ndicho hicho hicho kitapita.

Itakuwa ni kupoteza muda na gharama tu za mlipa kodi.



Civics Lesson

Serikali = Bunge + Mahakama/Judicial Body + Executive
 
Kwanini Samia anaonekana dhaifu sana?


Kwa sababu hana malengo ya kizalendo ya kulikomboa taifa, mbali na vihotuba vyake seemingly vitamuuuuuuuuuuuuuu na vyenye harufu nzuri mithili ya karafu za Pemba.

^Magufuli was arguably the best president because he had a clarity of vision which was underpinned by unassuming, undaunted and undoubtful sense of unmistakable patriotism^ ~ Prof. Lumumba
 
Hata kama lakini majadiliano yataweza kuifanya serikali ione makosa ..
Majadiliano hayajawahi kuwa na mwisho kwasababu kila mtu ana mtazamo wake.

Vile vile kwa siasa zetu zilivyo, hayo majadiliano ndani ya bunge yataishia tu kuathiriwa na itikadi za vyama.

Muhimu mimi naona ni kuwa na team huru ya wataalamu.

Nikisema namaanisha isiwe kama ile ya Makinikia, ya kumfurahisha Magu.
 
Back
Top Bottom