Ukifuatilia sana unaweza kubaliana na huyu jamaa. Maana wachezaji wengi ambao huonekana ni wazuri wakiwa Yanga hubadilika na kuwa wa hovyo wakienda Simba na ama Azam kwa sasa. Hali hii ni tofauti na kinyume chake. Ni wachache sana waliofanya vyema (kuanzia miaka ya tisini). Kidogo Aswile, Kipese, Kizota, Mwanamtwa, Nemes. Ila kwa wanaotoka Yanga na kwenda timu zingine kisha Simba/Azam hao sawa mf. China, Muso. Ila kwa wanaotoka Simba/Azam kwenda yanga karibu wote mambo huwanyookea. Mogella, Gaga, Method, Yondan, SMG, Makunda, Ajib, Gadiel, nk. Nadhani yanga ni makini zaidi wanapochukua mchezaji toka timu pinzani na wanaangalia kiwango kwa makini tofauti na Simba/Azamu, wao huchukua tu mradi katoka Yanga.Ukitoka Yanga Kwa mbwembwe utaacha mpira Yanga