Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,378
- 39,315
Chiriku wako ni wako, popote pale alipo,
Popote huko aliko, mawazoni kwake upo,
Ndege huyo ni wa kwako, Chiriku wa kwako yupo,
Chiriku yuko tunduni, mbona wewe humuoni?
Ni wewe ulimpata, Chiriku akawa wako,
Kama kalishwa limbwata, uliko wewe yeye yuko,
Wendako anakufuata, kama mwana na mbeleko,
Chiriku yuko Tunduni, mbona unamtafuta?
Ulimuahidi nini, Chiriku asubiria,
Ulisema siku gani, punje utamwagia,
Sasa kagoma tunduni, tenzi unamtungia,
Chiriku yuko tunduni, mbona unamlilia?
Chiriku kaimba nyimbo, na miluzi akapiga,
Muziki kama ulimbo, na wengine wakaiga,
Amekuwa ni makombo, kumbe wewe ulizuga,
Chiriku yuko tunduni, mbona wimbo hujajibu?
Chiriku ana huzuni, tunduni amejilaza,
Amefanya kosa gani, Chiriku ajiuliza,
Alalamika tunduni, nani atamtuliza,
Chiriku yuko tunduni, mbona kasahauliwa?
Beti zangu zinakoma, mapenzi ninakuasa,
Na ufanye wewe hima, Chiriku utamkosa,
Wengine waje jinoma, kwa yako wewe makosa,
Chiriku yuko tunduni, mbona akusubiria?!