Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,011
- 144,371
Hasara na upotevu huu unaotokana na taarifa za CAG ambapo wanasiasa waliochambua report ya CAG aliepita,Prof. Assad, waliibua utata wa matumizi ya shilling ya shilling trilioni 1.5 na hii ya hivi karibuni inatueleza hasara ya billion 150 katika uendeshaji wa ATCL.
Hasara na upotevu huu uliotokea chini ya utawala wa Magufuli, ni mbali na mamilion na mabilioni mengine yaliyopotea katika sekta za utalii, n.k kama inyoonyeshwa katika report ya CAG ya mwaka huu.
Bado hasara zinazotokana na serikali kufunguliwa makesi katika mahakama za usuluhishi za kimataifa bila kusahau hasara zilizotokana na siasa za hovyo za watu kujiuzulu kwa hoja ya kuunga mkono juhudi na kuliingiza Taifa gharama kubwa za mamilion kugharamia chaguzi ndogo.
Kwa kifupi, katika awamu ya Magufuli, Taifa limepata hasara kubwa Katika baadhi ya maeneo na pia kuna fedha nyingi zimetumika na kuacha utata mtupu kama hayo matumizi ya shilingi trilioni moja yaliyohojiwa na wabunge wa upinzani baada ya kuichambu report ya CAG aliepita(Prof.Assad).
Itakuwa ni jambo jema Bunge kuunda kamati teule kuchunguza utata wa matumizi haya ya shilingi trilioni 1.5 ili umma ujue ukweli ni upi na si hizi kelele za MATAGA kutaka kutuaminisha kuwa ufisadi ulidhibitiwa enzi za Hayati Magufuli tofauti na awamu zilizopita.
Kama hamtaki kuchunguza tuhuma hizi, acheni kumlinganisha Magufuli na watangulizi wake, hasa Kikwete, ambae wakati wake Bunge liliweze kuunda kamati teule na kuchunguza tuhuma zinazoihusu serikali, na pia vyombo vya habari viliweza kuanika kashifa mbalimbali za serikali bila kusahau Whistleblowers (kina Tumbili) waliweza kuanika madudu yaliyokuwa yanaendelea serikalini tofauti kabisa na ilivyokuwa wakati wa Magufuli .