Chini ya Mwenyekiti Magufuli akaunti ya CCM yanona, kutoka million 5 kwa mwaka hadi bilioni 20!

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Katibu mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally amesema kulikuwa na mchwa ndani ya ccm waliochota hela za chama mpaka kukifanya kubakiwa na million 5 tu kwa mwaka mzima! Lakini upepo umebadilika baada ya kuingia rais Magufuli sasa chama kinafunga mwaka na hadi billion 20 kwenye akaunti!.

Moja ya watu waliobanwa na kuzitema hizo mali ndio hao wanaoandika waraka uchwara kulenga kumchafua mwenyekiti wa ccm ,rais Magufuli.

Ni bora wanachama na wafusi wa chadema wakaiga mfano wa rais Magufuli na kuanza kuhoji na kujua mali na ruzuku ya chama zinaenda wapi.

Nina uhakika wakifanya hizi watagundua mengi sana kwa sababu kila unapofika uchaguzi Mbowe amekuwa analalamika chama hakina hela na kuamua kukikopesha kwa pesa zake binafsi! Upuuzi huu haukubaliki na lazima uhojiwe.
 
Mali za ccm ziliporwa toka kwa wananchi. Ccm haina mali zozote zaidi ya kurasimisha uporaji mkubwa wa mali za umma uliopata kutokea katika nchi yetu. Nitajie mali moja tu inayomilikiwa na ccm ambayo waliipata kihalali
Hiki ndicho wafuasi wengi wa ccm hawakijui. Kwamba kilipora mali za umma eg viwanja, majengo ya umma mali zingine zinazohamishika bila ridhaa ya wananchi. Na hata leo ukiangalia bila dola ccm haipo.
 
Hii ndiyo sababu inayozuia chadema kuwa na mali zao?
 
Hiki ndicho wafuasi wengi wa ccm hawakijui. Kwamba kilipora mali za umma eg viwanja, majengo ya umma mali zingine zinazohamishika bila ridhaa ya wananchi. Na hata leo ukiangalia bila dola ccm haipo.
Huu ndiyo uchochoro wa vibaraka wa Mbowe kuhalalisha wizi wa ruzuku ya chama.
 
Hili jengo hapa Dodoma ulitupa babako
Mali za ccm ziliporwa toka kwa wananchi. Ccm haina mali zozote zaidi ya kurasimisha uporaji mkubwa wa mali za umma uliopata kutokea katika nchi yetu. Nitajie mali moja tu inayomilikiwa na ccm ambayo waliipata kihalali
 
Mbowe anatetemeka sasa ,alisikika kijana wa bavicha
Siasa bwana...kwasasa mali ya Chama zinaliwa na Mkumbo..mama Anna...Patrobas Katambi ; Mbowe nae akiamia huko anazila tu. Yaani wanachama wa CCM hawajui kua pesa za Chama ndo Mkuu wa mkoa anachota kuwafanyia watu tafrija na kutoa zawadi kwa jinsi apendavyo.
 
Baada ya uchaguzi Account itakuwa zero

Sasa hivi Account lazima itune kwa kuwa tunaenda kwny Uchaguzi

Hata wenzie walitunisha Accounts za Chama walipokaribia uchaguzi

Ubora wa Comrade ni kuvusha Chama kwny kipindi kigumu mno kwny Historia ya Chama enzi hizo yeye Bashiru akiwa kwny Midahalo akitabiri ambayo hayakutokea

Hata Accounts za vilabu vyetu vya Simba na Yanga huwa zinanenepa nyakati za usajili

Ushamba mzigo kweli
 
Back
Top Bottom