Chini ya Mwamvuli wa CCM Mawaziri wataendelea kufanya Madudu,kujiuzulu kwa mashinikizo sio mwisho.

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,619
2,000
Habari ya Siku hii

Sikushangazwa na wale waliotoa pongezi kwa 'serikali ya ccm' kwa yaliyotokea hapo jana baada ya Ripoti ya Lembeli kuwaingiza mkenge mawaziri kadhaa 'WALIOFUTWA KAZI'

Niseme tu kuwa wasije kutoa pongezi nyingine ndani ya miezi sita ijayo baada ya wateule wengine watakaoapishwa kucheza rafu dhidi ya maisha ya watanzania na haki za binadamu.

Wangeshatoa pongezi hivi karibumi kwa matokeo ya mabomu ya gongo la mboto dhidi ya Hussein Mwinyi na pia waziri wa elimu na naibu wake waliogoma kujiuzulu.

Tatizo hapa ni mfumo dhaifu wa chama cha mapinduzi,uzembe wa Rais na waziri mkuu ambao wangestahili KUJIFURUSHA wenyewe toka ktk ofisi ya umma.

Sintashangaa baada ya James Lembeli kumfurusha MAIGE sasa KAGASHEKI pengine ndani ya miezi saba 'ALIYESAHAULIKA' akanaswa na LEMBELI na safari hii tuhuma zake ZIKAMBURUZA Mahakamani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom