Chinga wampasua Meya

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,201
233
Inasemekana Meya Wa Jiji La Dar Es Salaam Mh Jumaaa Amepasuliwa Na Jiwe Kichwani Baada Ya Kuingilia Ugomvi Kati Ya Mgambo Wa Manispaa Na Wamachinga

Kasheshe Hiyo Ilianza Pale Askari Hao Walivyoanza Kumtwanga Kijana Mmoja Kwa Jina La Hassani Eneo La Kitumbini

Habari Zaidi Soma Magazeti Ya Kesho
 
ohoooo
jambo limezua jambo
nampa pole meya (kama ni kweli kapasuliwa)
 
chinga boyzz, ni dalili mbaya maana hata Bukombe, Kagera, Singida, matukio ya kutumia nguvu yanajitokeza.

Tume itaundwa kubaini tatizo
 
Inasemekana Meya Wa Jiji La Dar Es Salaam Mh Jumaaa Amepasuliwa Na Jiwe Kichwani Baada Ya Kuingilia Ugomvi Kati Ya Mgambo Wa Manispaa Na Wamachinga

Ni Abuu Jumaa ni Meya wa Manispaa ya Ilala, na Kama ni Meya wa Jiji ni Adam Kimbisa, sasa sijui ni yupi... lakini naamin atakua ni Abuu Jumaa, maana Kitumbini iko aneo lake, lakini pia Kimbisa ni msomi na hawezi kwenda kichwa kichwa. Huyu mzee Abuu Jumaa, ana kashfa nyingi za chinichini lakini katika suala la elimu, hana tofauti na mimi na babu yangu Hassan Dalali wa Simba, saa nafasi aliyopewa kwa dunia ya sasa ya Utandawazi ni kubwa mno kwa upeo wake. Zama za kupeana nafasi kwa fedha ama umaarufu zimekwisha na huu uwe msimu wake wa mwisho kuongoza. Familia yake inahusishwa na mambo mengi na sasa kuna kesi mahakamani inayohusu wizi wa magogo, ambayo polisi wameipiga chenga na sasa iko Mahakama ya Temeke kama kesi ya madai badala ya wizi.
 
Ahsanteni sana wachangiaji, pamoja na kuwa hili tukio si la kuchekesha lakini mmenivunja mbavu sana...LOL!
 
Lakini mi nasema wagambo wamezidi kuwanyanyapaa wamachinga! lazima wawe wagumu sasa! Nakumbuka wakati wa bomoabomoa waliwaahidi eti watawajengea 'mall' ya ghorofa 10 ya wamachinga! Mmh! Sasa miaka 2 imepita hizo soko walzipangiwa ni duni na wamejazana! Na sasa wanabughudhiwa huko Mchikichini walipopangiwa kuuza! Tatizo serikai yetu haina mipango (no plans) ni kichwa cha mwendawazimu. Akiamka meya au waziri mkuu anasema "Safisha jiji" kwani hao wamachinga ni uchafu? Si ni wanadamu?! Ah!:mad:
 
Itabdi, maana wakimpeleka Muhimbili unaweza ukakuta anapasuliwa uti wa mgongo badala ya kichwa!


By the way tunapokuwa na wagonjwa tuwe nao karibu at least ukijua mgonjwa wako anaenda thieatre saa ngapi na anafanyiwa operation na doctor gani itasaidia kuhakiki yanatokea hayo vizuri, maana waweza mgonjwa aweza kuumwa kidole cha mguu akapaduliwa jicho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom