Chinese Vs. Tanzanians. Kuna Tatizo Serikali Inalifumbia Macho

Nairobian

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
873
2,277
Ndugu zangu, kuna tatizo kubwa humu nchini ya ki usalama linaloendelea dhidi ya watanzania linalosababishwa na Wachina.

Katika Miradi mikubwa inayotekelezwa na Wachina kuna sehemu ndogo za Mradi ambazo zingetekelezwa na Watanzania, lakini tatizo ni kwamba, hakuna kampuni ya Kichina inayoweza kuipa kampuni ya Kitanzania kazi. Unless ni kazi ndogo sana. Kazi nyingi wanapewa Wachina hata kama hawana vigezo lazima watapeana wenyewe kwa wenyewe.

Na hata kwenye ajira, ni wachina kwa wachina. Watanzania wanapewa kazi za kitumwa. Na wananyanyaswa hasa. Sehemu yoyote ya Kichina. Kwa wanaokuwa na wasiwasi kuhusu hili, jaribuni kuangazs macho kwenye Miradi mikubwa ya ujenzi Nk. Mtakuta kubwa sub -contractor's ni wachina. Watanzania watakaopewa kutokana na serikali kutaka kampuni fulani yenye uwezo kupewa,hiyo kazi, Wachina watagoma kulipa.

Mvutano utakuwepo hata miezi 8 hadi 9 wasilipe. Haya ni mambo ya ki usalama ya nchi. Serikali angalienj hili. Nina mifano mingi lakini sitaki kutaja makampuni ambayo yamefanyiwa huu unyama na wachina.

Je ni mikataba na Serikali inaruhusu kazi zote kwenda kwa Wachina, au Wachina wenyewe wanatufanyia uhuni?
 
ELIMU ELIMU ELIMU, Ili kuondoa hili na hayo matatizo ni lazima tujitegemee na kukubali kutumia wataalam wetu, je huo uwezo tunao????????
 
ELIMU ELIMU ELIMU, Ili kuondoa hili na hayo matatizo ni lazima tujitegemee na kukubali kutumia wataalam wetu, je huo uwezo tunao????????
Hakika... Kabla ya kuwalaumu wa china lazima tujiulize hilo swali.. je TUNAJIWEZA? TUNA UWEZO EA KUJITEGEMEA KWA KILA KITU?

MÊmENtO HoMO
 
Kuna mradi wa maj huku arusha naona wengine wamekuwa mpaka madereva wabongo wamebaki kuwa wapambe na wachimba mitaro ya bomba Kubwa
 
Bila kupepesa macho watanzania wengi wezi na wavivu hayo wachina wanayajua ndo maana hawataki masihara
 
Back
Top Bottom