China yazungumzia uboreshwaji wa TAZARA

mnyalilungulu

Senior Member
Sep 27, 2019
172
250
Dar es Salaam. Serikali ya China imesema haitaliacha Shirika la Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) life bali itaendelea kufanya kazi na nchi hizo mbili ili kuhakikisha usafiri huo ulioanza miaka 40 iliyopita unadumu.

Akizungumza katika ofisi za kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) Tabata Relini jijini Dar es Salaam, Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke amesema Tazara ni umoja wa nchi za Tanzania, Zambia na China na inapaswa kuendelea kuwapo.

Amesema ujenzi wa reli hiyo kati ya Dar es Salaam na Kapiri Mposhi uliofanyika kati ya mwaka 1970 hadi 1976 ilikuwa ni zawadi ya China kwa mataifa ya Zambia na Tanzania, hivyo nchi hizo zinapaswa kuendelea kushirikiana.

Akizungumzia taarifa za vyombo vya habari kuwa Tanzania ilitaka kuboresha masharti matano yaliyohusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo kwa sababu hayakuwa na faida kwa Serikali ya Tanzania, amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote. Ke amesema taarifa hizo zimeandikwa mtandaoni kutoka Kenya na si kwenye gazeti na wenyewe kama ubalozi hawafahamu zilitoka wapi.

Alisema mradi huo wa Bandari ni muhimu na unahusu Serikali na mwekezaji kutoka China ambao ndiyo wanaopaswa kuzungumzia ni namna gani wanaweza kuuendeleza. Ke amesema China inapenda kuona mwekezaji kutoka nchini humo anawekeza katika mradi huo wa bandari kwa faida ya nchi na raia.
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
6,819
2,000
Hahaha maneno ya Rais wetu Magufuli wanasema yalitoka Kenya?

Kumbe mabalozi nao wanafanya siasa nchi za watu?!
 
Da Pride

JF-Expert Member
Nov 29, 2017
482
500
Nmeliona gazeti la The East African, written by Onyango.

Katika nakala yake ameongelea mambo matano ambayo kama Tanzania imemtaka mwekezaji kuyarekebisha au kuachana kabisa na Ujenzi huo wa Bandari kubwa na ya kisasa Mashariki mwa Afrika.
 
Katavi yetu

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
827
1,000
Bora kuboresha TAZARA kuliko kujenga bandari mpya bagamoyo kwa sababu hii rail inafaida kubwa sana kiuchumi kulinganisha na bandari inayotaka kujengwa
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
6,928
2,000
Akizungumzia taarifa za vyombo vya habari kuwa Tanzania ilitaka kuboresha masharti matano yaliyohusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo kwa sababu hayakuwa na faida kwa Serikali ya Tanzania, amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote. Ke amesema taarifa hizo zimeandikwa mtandaoni kutoka Kenya na si kwenye gazeti na wenyewe kama ubalozi hawafahamu zilitoka wapi.
Eeeh, unasemaje?
"Tanzania gives Chinese firm conditions for Bagamoyo port," ilikuwa ni habari feki katika gazeti la The Citizen?

Mbona hii inaelekea kuwa 'vita baridi' na jirani!

Kama kuna ukweli wowote kuhusu 'ufeki' wa taarifa hiyo, basi tayari tuko vitani.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
6,928
2,000
Nmeliona gazeti la The East African, written by Onyango.

Katika nakala yake ameongelea mambo matano ambayo kama Tanzania imemtaka mwekezaji kuyarekebisha au kuachana kabisa na Ujenzi huo wa Bandari kubwa na ya kisasa Mashariki mwa Afrika.
Makala hiyo ilionekana kwanza kwenye 'The Citizen', ambalo linachapishwa hapo hapo Tabata; halafu Balozi anasema ni habari toka Kenya, si maajabu hayo?
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,093
2,000
Nmeliona gazeti la The East African, written by Onyango.

Katika nakala yake ameongelea mambo matano ambayo kama Tanzania imemtaka mwekezaji kuyarekebisha au kuachana kabisa na Ujenzi huo wa Bandari kubwa na ya kisasa Mashariki mwa Afrika.
Onyango Ni mkenya balozi was China Yuko sahihi kuwa hayo maneno yametokea kenya
 
Da Pride

JF-Expert Member
Nov 29, 2017
482
500
Bora kuboresha TAZARA kuliko kujenga bandari mpya bagamoyo kwa sababu hii rail inafaida kubwa sana kiuchumi kulinganisha na bandari inayotaka kujengwa
Upo sahihi kwa mtazamo wako mkuu....

Ila kama Nchi tunahitaji sana kua na Bandari mfano wa hiyo ya Bagamoyo kwani itakua kubwa ukanda huu wa EA pia yenye teknolojia kubwa zaid na ufanisi wa kiwango chake.

Kwanini tuwe na Bandari ya Bagamoyo?
i/. Kwanza haipo mbali na bandar kubwa ya Mombasa hivyo ujenzi wake utachochea ushindani na huduma bora kwa Mteja.

ii/. Kwa ukubwa na ubora wake tunataraji kuongeza mapato kwa kiwango kikubwa zaidi.

iii/. Itaongeza ajira nyingi zaidi kwa Wazawa.

iv/. Ni kichocheo kikubwa sana kwa Biashara kwenye shoroba zetu zote kuanzia kusini mashariki, magharibi hadi kaskazini Mwa nchi yetu hasa ukizingatia uboreshwaji wa miundombinu uliofanywa na Serikali kuanzia ujenzi wa Barabara na religious zote SGR, CGR na MGR.

v/. The concept of Multiplier effect, uwepo wa bandari ya Bagamoyo ni catalyst kwa uchumi wa nchi kwani uwepo wake tu itachochea shughuli mbali mbali za kiuchumi kuanzia kilimo, machimbo, mifugo na sekta ya Viwanda.

Hivo basi,
Natambua nia thabiti ya serikali yetu kua installation of Bagamoyo port ni lazima iwe inatosha win - win situation btn mwekezaji na Serikali tofauti na awali ambapo faida kwa nchi ilijikita kwenye indirect profit as only Multiplier effect not directly kama ukusanyaji wa kodi.

Serikali haina budi kukaa na Mwekezaji ili kutatua changamoto zilizojitokeza awali, kwa kuangalia umuhim wa Bandar hiyo kwa kizazi cha lao nambie kijacho.

Da Pride.
 
carter

JF-Expert Member
Jan 23, 2009
3,088
2,000
Eeeh, unasemaje?
"Tanzania gives Chinese firm conditions for Bagamoyo port," ilikuwa ni habari feki katika gazeti la The Citizen?

Mbona hii inaelekea kuwa 'vita baridi' na jirani!

Kama kuna ukweli wowote kuhusu 'ufeki' wa taarifa hiyo, basi tayari tuko vitani.
Vita ipo toka kitambo mkuu, sema Sasa ndio inajionesha dhahiri..refer vyombo vingi vya habari na matisho ya Ebola. Habari zilitoka zaidi nje kuliko ndani.
 
Da Pride

JF-Expert Member
Nov 29, 2017
482
500
But the article narrates about our Tanzanian government.
Onyango Ni mkenya balozi was China Yuko sahihi kuwa hayo maneno yametokea kenya
How come the author speaks on our behalf? What are the motives behind that?
No, We should stop them immediately course they might have their own Agendas regarding our economic race.
 
marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
13,356
2,000
Akizungumzia taarifa za vyombo vya habari kuwa Tanzania ilitaka kuboresha masharti matano yaliyohusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo kwa sababu hayakuwa na faida kwa Serikali ya Tanzania, amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote. Ke amesema taarifa hizo zimeandikwa mtandaoni kutoka Kenya na si kwenye gazeti na wenyewe kama ubalozi hawafahamu zilitoka wapi.
Mbona hata kiongozi wetu alisema hadharani kuwa mradi ule hauna tija kwa taifa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom