China yazisaidia nchi za Afrika kupata maendeleo katika matumizi ya teknolojia ya mawasiliano

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
Na Caroline Nassoro

VCG11422519097.jpg

Karne hii ya 21 inajulikana kama karne ya Sayansi na Teknolojia. Sekta hii imepewa umuhimu wa kipekee katika zama hizi, na ni ajabu kama utakuta mtu hana japo simu ya mkononi, kwani siku hiz, hususan simu janja (smart phones) ni sawasawa na benki, shajara, na kila kitu.

Baada ya mlipuko wa janga la virusi vya Corona kutokea duniani, sekta ya sayansi na teknolojia imepewa kipaumbele cha kipekee. Mataifa mengi yalifunga shughuli zote za kibiashara na kijamii, wafanyakazi walitakiwa kufanya kazi wakiwa majumbani, wanafunzi kusoma kupitia masomo yaliyokuwa yakitolewa kwa njia ya mtandao. Kwa ufupi, teknolojia imekuwa kitu cha muhimu na cha lazima katika kipindi hiki.

Kwa kuzingatia hilo, China, ambayo ni nchi mwenzi wa kutegemewa wa Afrika, inaongeza uwepo wake wa kidijitali katika bara hilo, kama mkakati wake muhimu kwa bara la Afrika baada ya janga la COVID-19. Kampuni za China katika bara hilo zimewekeza karibu dola za kimarekani bilioni 8.43 barani Afrika kama sehemu ya mkakati huo mkubwa.

Kama sehemu ya mkakati huu, serikali ya Cina imependekeza kampuni kubwa za teknolojia ya mawasiliano HUAWEI, ZTE na Cloudwalk kujihusisha na utengenezaji wa simu za mkononi, matumizi ya mitandao ya kijamii na biashara kupitia mtandao barani Afrika.

Tukitolea mfano kampuni kubwa ya mawasiliano ya China HUAWEI, ambayo imekuwa ikichochea maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano barani Afrika kupitia njia mbalimbali, ikiwemo mashindano ya Teknolojia, Habari, na Mawasiliano (TEHAMA) kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, na pia kutoa mafunzo kwa wanafunzi hao.

Lengo kuu la mashindano ya TEHAMA yamayoandaliwa na kampuni hiyo ni kutoa jukwaa kwa vijana wenye vipaji katika sekta hiyo kuonyesha uwezo wao, kushindana na kuwasiliana, na pia kuhimiza utafiti wa TEHAMA na kusaidia ukuaji wa mfumo thabiti wa teknolojia hiyo.

Licha ya mashindano kama hayo, kampuni ya HUAWEI pia hutoa mafunzo ya kuendeleza vipaji vya TEHAMA kwa wanafunzi katika nchi husika, kuongeza ufahamu wa kubadilishana ujuzi, na kuchochea ushirikishi katika jamii ya kidijitali.

Mafunzo hayo yanaendana na mikakati ya kidijitali ya nchi nyingi za Afrika inayolenga kuwa na wataalamu wa TEHAMA ambao ni muhimu sana katika maendeleo ya viwanda na kutoa mchango katika kupunguza tatizo la upatikanaji wa ajira.

Kwa msaada wa kampuni za China, nchi za Afrika kwa sasa zinajivunia maendeleo makubwa katika sekta ya teknolojia ya mawasiliano. Simu janja zinazotengenezwa na kampuni za China barani Afrika zinaendana na mahitaji halisi ya watu katika maeneo husika, na pia zinasaidia katika kurahisisha mawasiliano.

Kupitia simu hizo, wajasiriamali wengi wameweza kutangaza na kuuza bidhaa zao bila ya kutumia muda mwingi katika shughuli hiyo. Majukwaa ama maduka mengi katika mtandao yanayohusiana na Kundi la Alibaba pia yanazisaidia nchi za Afrika kutangaza na kuuza bidhaa zao za kilimo.

Kutokana na hayo machache, ni wazi kuwa, tofauti na madai yanayotolewa na baadhi ya nchi za Magharibi, China ni mwenzi muhimu wa maendeleo kwa bara la Afrika, na ushirikiano kati ya pande hizo ni wa kunufaishana, kusaidiana, na kuendelea kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom