China yasitisha usafiri wa umma katika mkoa wa Wuhan kudhibiti Virusi Corona

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,941
2,000
1579754763892.png

China imefanya maamuzi magumu ya kusitisha usafiri wa umma hasa katika mkoa wa Wuhan, unaokaliwa na watu karibu milioni tisa, wakati wa mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa Corona.

Watu wanaoishi katika jiji hilo wameambiwa wasiondoke nje ya mji huo, na uwanja wa ndege na vituo vya treni vitafungwa kwa abiria wanaotoka nje ya eneo hilo.

Basi, reli za chini ya ardhi, feri, na mitandao ya uchukuzi wa umbali mrefu itasitishwa kuanzia leo Alhamisi.

Virusi vipya vimeenea kutoka Wuhan hadi majimbo kadhaa ya China, Marekani, Thailand na Korea Kusini.

Virusi, vinavyojulikana kama 2019-nCoV, inaarifiwa kuwa ni aina mpya ambavyo havijatambuliwa awali kuwa vinaathari kwa wanaadamu.

Taarifa hii yenye kuogofya ulimwenguni kutokana na kasi ya ueneaji wa ugonjwa huo, mlipuko huo umewauwa watu 17, na kuna kesi 440 zilizothibitishwa.

Wachunguzi wa afya wanaarifu kuwa Virusi hiyo ilitoka katika soko la vyakula vya baharini ambalo "lilichanganya vyakula hivyo na shughuli haramu za wanyama wa porini".

Kama hiyo haitoshi Viongozi huko Hong Kong pia waliripoti kesi mbili za kwanza za eneo hilo.

Kama utakumbuka vizuri kulikuwa na virusi vya Sars ambavyo viliwauwa karibu watu 800 ulimwenguni mwanzoni mwa miaka ya 2000 na madaktari wanaarifu kuwa navyo ni jamii ya virusi vya Corona.

Mkutano wa kutathmini hatari za kiafya zinazokabili ulimwenguni ulisitishwa ili kuamua ikiwa inapaswa kutangazwa dharura ya afya kimataifa kama ilivyotokea wakati wa homa ya nguruwe na ugonjwa wa Ebola pia.

Jioni ya Jumatano, viongozi wa China walithibitisha idadi ya waliokufa ilikuwa karibu mara mbili kutoka tisa kwa siku moja . Wote waliofariki hadi sasa ni kutoka Hubei, mkoa unaozunguka Wuhan.

Maafisa wa China waliarifu kuwa nchi hiyo kwa sasa iko katika "hatua muhimu zaidi" ya kuzuia na kudhibiti virusi hivyo.

Maafisa wanaarifu kuwa "Kimsingi, usiende Wuhan. Na wale wa Wuhan tafadhali usiondoke mjini," alisema makamu wa Tume ya Kitaifa ya Afya Li Bin katika mojawapo ya mkutano wa kwanza wa umma tangu kuzuka vya virusi hivyo. Mapema wiki hii, China ilithibitisha kwamba maambukizi baina ya binadamu na binadamu yametokea.

Dalili za maambukizi ya virusi hivi vipya vya Corona ni pamoja na dalili ya kushindwa kupumua vyema, homa, na kikohozi.

Kesi ya kwanza nchini Marekani ilithibitishwa mwanzoni mwa wiki hii . Rais Donald Trump alisema hali hiyo imedhibitiwa na kwamba anaamini taarifa iliyotolewa na viongozi wa China.

Ni jaribio kubwa la kuzuia kuenea kwa virusi hivi vya Corona , ambavyo tunajua sasa vinaweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

Kuzuia usafiri wa aina yoyote kutoka sehemu moja kwenye ingine ulimwenguni Kunaweza kupunguza nafasi ya virusi vya Corona kufikia miji mingine nchini China na nchi zingine ulimwenguni.

Zuio hilo limetekelezwa kutokana na mamilioni ya watu wanaojiandaa kusafiri kwenda nchini China kwa likizo ya wiki nzima ambayo ni Mwaka Mpya wa Lunar.

Swali kubwa lililosalia ni ikiwa ni je wakaazi wa milioni 8.9 wa Wuhan wanaweza kutumia njia za barabara kuondoka eneo hilo.

Chanzo: BBC Swahili
 

Mwamba028

JF-Expert Member
Nov 15, 2013
4,177
2,000
Hao wachina acha wafe tuu mana wanakula kila kitu tena wanakulaga mpk viumbe wakiwa wazima kbisa, kuna mdada wa kichina youtube huko anakulaga pweza akiwa mzima kbs anachezesha mikia yake
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
17,016
2,000
Kinachoshangaza tunadhani dunia ni ile ya miaka ya 60
Siku hizi wachina wanasafiri kila nchi duniani na kwetu wanaingia kila siku
Haya ni kama mafua tu na yanauwa na yanaambukiza sasa je hao wanaoingia kwetu wako salama?
UK wamekaa wizara zote kikao cha dharura na Scotland kuna watu wamewekwa quarantines
Hili suala sio la kuchekea
China wanajenga hospital ya haraka kwa ajili ya ugonjwa huu na itachukua siku 6 tu na kuhifadhi watu 1000
Adjustments.jpgSent from my iPhone using Tapatalk
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom