China yasema iko tayari kushirikiana na Serikali ya Wataliban

Wanao-Support Ugaidi waende huko wakakae , watu wanabakwa , watu wanauliwa , watuwanafanyiwa matendo ya aibu . Alafu Kuna puuzi moja badala ya kulaani lina piga makofi. Cha Ajabu wanauwa watu huku wakisema الله أكبر (MUNGU ni mkubwa). Ni Mungu yupi huyo? Mungu wa mbinguni, ndiye anafurahi kuona uasi , watoto wakifanywa yatima , wanawake wakibakwa mbele ya familia zao, damu zikiminika kisa madaraka?
Kwan LIBYA na IRAQ zilizovamiwa na US+NATO watoto walikua yatima sababu ya dini au nini
Muache ujuaji tunachokijua nikwamba US paper tiger wamesanda umbwa wale hayo yataleban watajijua wenyewe huko

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Halaf watu weng hawajui...marekan huko afghan..iraq..na kwengneko ambajo wanaonekana wanajeshi wao...zile ni private companies yaan watu binafsi wanakua na makampuni ya ulinz.

Yaan jeshi kamili kabisa na silaha zotee. Ni makampun ya ma bilionea wa kimarekan..wanafanyaga michezo michafu tu huko...yaan marekan akishaingilia nchi flan..baada ya vita...bas hzo private companies huomba hzo tenda za ulinzi huko ndio maana wale askar wa jesh wanaokwenda huko huwa hawaish sabab ni donge nono

Askar analipwa mara 10 zaid anavyolipwa na serikal..ndomana unaona hawaish kwenda huko unajiuliza wamarekan hawachoki? Yaan sawasawa serikal ya Tz iseme tunaruhusu makampuni binafsi yawe na walinz level ya jeshi halaf muende mkasaidie vita congo na sehem zingne zenye migogoro. .mshahara ni donge nono...uone jins watu watakavyo changamkia fursa...mshahara unalipwa 15m. Hata ni ntaenda

Unafahamu askari wa akiba !

Kuna sehemu unakosea kidogo,usa katika upande wa jeshi lina vitengo ambavyo vengine vinafungamana na idara kama CIA,NSA na n.k

Ni asilimia ndogo inayotegemea askari binafsi
 
Hujui chochte ..naona haya uviv kukuelezea maana huto elewa

Sent from my TECNO CC6 using JamiiForums mobile app
Ebu tuelezee wewe unayejua kuhusu Nukes.unaposikia nchi inamiliki silaha za Nuclear basi ipe eshima iyo nchi maana sio silaha ya kawaida kabisa na sio silaha ambayo inakaa tu ovyo ovyo.

Mwaka gani ulishawai kusikia silaha za nuclear zinauzwa.hata muwe marafiki vipi mtu awezi kukuzia silaha za nuclear

Shida movie uwa zinawadanganya.
 
Dunia imejaa fitina, wakati Marekani kafungasha virago vyake huko Afghanistan na kuwaachia Wataliban wakijitwalia ushindi mnono na kujiandaa kuunda serikali, China yasema iko tayari kushirikiana na Serikali ya Wataleban.

Wakati nchi kadhaa zikiwa kwenye hatihati za kufunga balozi zao, Urusi yasema Ubalozi wake utaendelea kuwepo Kabul. Wakati hayo yakitokea Ujerumani yajuta na kusema yanayotokea Afghanistan kwa sasa Ni aibu kubwa Sana kwa NATO.

Wanazuoni tunajiuliza Marekani alifuata Nini Huko? Je malengo yake yametimia?

Watalibani wanarudi Tena madarakani baada ya kufurushwa miaka takriban 20 iliyopota. Marekani aliondoka Vietnam kiajabu, aliondoka Korea kiajabu, aliondoka Cuba kiajabu, aliondoka Somalia kiajabu, aliondoka Iraq kiajabu, aliondoka Syria kiajabu.

Kwa hiyo Marekani karidhia aliowaita magaidi kurudi Tena Ikulu? Kwangu Mimi Wataleban hawakuwa magaidi Ila walimkaribisha gaidi Osama bin Laden na kundi lake la Al Qaida.

Wakati huo Wataliban wakiongozwa na Mullah Omar Mohamed na Osama bin Laden Raia wa Saud Arabia/yemen akiongoza kundi la Al Qaida.

Bin laden ndio aliyesimamia shoo ya kulipua balozi za Marekani zilizopo Dar es salaam na Nairobi, kulipua meli ya Marekani Yemen na kuteketeza majengo marefu zaidi mawili duniani WTC wakati ule, kulipua makao makuu ya Jeshi yanayolindwa zaidi duniani pentagon na kusudio lililoshindwa la kulipua majengo muhimu ya Marekani.

Osama bin laden alipewa hifadhi na Watalaban huko Afghanistan na ndio ikapelekea Marekani kwenda huko kumsaka na hatimae kumuua.

Marekani ilikusudia kuwafuta kabisa wafadhili wa maficho ya Osama Wataliban ili asije akatokea Osama mwingine akapewa hifadhi huko.

Marekani ilimuandama rafiki kipenzi wa Osama Mkuu wa Watalaban ndugu Mullar Omar Mohamed kiongozi wa Kiroho wa Talaban hatimae inasemekana alifia mafichoni.

Lakini watalibani bado wapo,na Leo hii wamerudi madarakani. Malengo ya Marekani yametimia au ilikua Ni kuchoma noti tu, na kupoteza vijana wa kimarekani?

"Lone survivor"
Marekani akishavuma chake hajali yy huondoka mapema mpambane na hali yenu naiwazia CONGO/Kinshasa mpaka leo bado anapang'ang'ania Siku mali zikiisha najua atqwaacha Yatima tuu time will tell !
 
Halaf watu weng hawajui...marekan huko afghan..iraq..na kwengneko ambajo wanaonekana wanajeshi wao...zile ni private companies yaan watu binafsi wanakua na makampuni ya ulinz.

Yaan jeshi kamili kabisa na silaha zotee. Ni makampun ya ma bilionea wa kimarekan..wanafanyaga michezo michafu tu huko...yaan marekan akishaingilia nchi flan..baada ya vita...bas hzo private companies huomba hzo tenda za ulinzi huko ndio maana wale askar wa jesh wanaokwenda huko huwa hawaish sabab ni donge nono

Askar analipwa mara 10 zaid anavyolipwa na serikal..ndomana unaona hawaish kwenda huko unajiuliza wamarekan hawachoki? Yaan sawasawa serikal ya Tz iseme tunaruhusu makampuni binafsi yawe na walinz level ya jeshi halaf muende mkasaidie vita congo na sehem zingne zenye migogoro. .mshahara ni donge nono...uone jins watu watakavyo changamkia fursa...mshahara unalipwa 15m. Hata ni ntaenda
Acha uongo wewe wakati wazazi wa hao watoto/wanajeshi wanalia sababu watoto wao wanaingizwa kwenye vita zisizokuwa na kichwa wala miguu,, kwa taarifa yako tu hakuna raia wa marekani anaependa vita
 
Ahmad Shah Massoud aliyekuwa assassinated na Taliban mwaka ambao ndiyo USA ilishambuliwa na Osama, alikuwa anafavour mfumo wa maisha ya kidemokrasia ikiwemo kuwapa wanawake haki sawa na wanaume.

USA ilienda kuwatwanga Taliban kwasababu ya kumhifadhi Osama lakini pia siasa za Masoud ziliivutia USA ndiyo maana wakausaidia upande wa Masoud kuunda serikali ya Afghanistan.

Lakini waafghanistan wanaume waliowengi hawakupenda huo mfumo wa maisha ,ulionekana unakinzana na dini. Walikuwa ni masnitch wakikamua mkwanja wa USA kwa kuimarishiwa jeshi lao hata kulipwa mishahara kutoka USA.

Biden ana haki ya kuwaacha wataliban wachukue nchi kwani inaonyesha serikali ya Afghanistan ilikuwa inawaunga mkono Taliban. Haiingii akilini ,,serikali yenye jeshi(trained soldiers) na vifaa vya kisasa zikiwemo ndege kushindwa kurusha hata risasi moja dhidi ya wanamgambo wenye siraha duni hadi ikulu inatekwa.

Naona Biden kaonya Taliban wasijaribu kumgusa mmarekani yeyote. Kawambia atawajibu kwa haraka na kwa kishindo.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Biden kaongea vyema tu
 
Kitu nimegundua Taliban hawana shida na mtu na hata mimi mwenyewe niko tayari kufanya kazi na Taliban kwenye ushirikiano wa nyanja zote.
Kabisa mkuu, natamani tuwe na ubalozi huko nami niwe mmoja wa watumoshi ws ubalozini
20210817_163251.jpg
 
Back
Top Bottom