lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,147
- 33,299
Dunia imejaa fitina, wakati Marekani kafungasha virago vyake huko Afghanistan na kuwaachia Wataliban wakijitwalia ushindi mnono na kujiandaa kuunda serikali, China yasema iko tayari kushirikiana na Serikali ya Wataleban.
Wakati nchi kadhaa zikiwa kwenye hatihati za kufunga balozi zao, Urusi yasema Ubalozi wake utaendelea kuwepo Kabul. Wakati hayo yakitokea Ujerumani yajuta na kusema yanayotokea Afghanistan kwa sasa Ni aibu kubwa Sana kwa NATO.
Wanazuoni tunajiuliza Marekani alifuata Nini Huko? Je malengo yake yametimia?
Watalibani wanarudi Tena madarakani baada ya kufurushwa miaka takriban 20 iliyopota. Marekani aliondoka Vietnam kiajabu, aliondoka Korea kiajabu, aliondoka Cuba kiajabu, aliondoka Somalia kiajabu, aliondoka Iraq kiajabu, aliondoka Syria kiajabu.
Kwa hiyo Marekani karidhia aliowaita magaidi kurudi Tena Ikulu? Kwangu Mimi Wataleban hawakuwa magaidi Ila walimkaribisha gaidi Osama bin Laden na kundi lake la Al Qaida.
Wakati huo Wataliban wakiongozwa na Mullah Omar Mohamed na Osama bin Laden Raia wa Saud Arabia/yemen akiongoza kundi la Al Qaida.
Bin laden ndio aliyesimamia shoo ya kulipua balozi za Marekani zilizopo Dar es salaam na Nairobi, kulipua meli ya Marekani Yemen na kuteketeza majengo marefu zaidi mawili duniani WTC wakati ule, kulipua makao makuu ya Jeshi yanayolindwa zaidi duniani pentagon na kusudio lililoshindwa la kulipua majengo muhimu ya Marekani.
Osama bin laden alipewa hifadhi na Watalaban huko Afghanistan na ndio ikapelekea Marekani kwenda huko kumsaka na hatimae kumuua.
Marekani ilikusudia kuwafuta kabisa wafadhili wa maficho ya Osama Wataliban ili asije akatokea Osama mwingine akapewa hifadhi huko.
Marekani ilimuandama rafiki kipenzi wa Osama Mkuu wa Watalaban ndugu Mullar Omar Mohamed kiongozi wa Kiroho wa Talaban hatimae inasemekana alifia mafichoni.
Lakini watalibani bado wapo,na Leo hii wamerudi madarakani. Malengo ya Marekani yametimia au ilikua Ni kuchoma noti tu, na kupoteza vijana wa kimarekani?
"Lone survivor"