ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,418
- 9,599
China yapata pigo baada ya nchi za Tanzania na Kenya kusitisha miradi ya mabilioni ya dola.
Rais Magufuli wa Tanzania alieleza sababu kuu ya kusitisha mradi wa bandari ya Bagamoyo ambayo ingefadhiliwa na Uchina ni masharti magumu na ya kinyonyaji.
Nchi nyingi zimeanza kupitia upya miradi ya China zikiwemo Malaysia,Pakistan, Ethiopia kufuatia madai ya China kuziingiza nchi kwenye madeni makubwa yasiyolipika kwa lengo la kutwaa rasilimali na maeneo muhimu ya nchi kama vile bandari nk.
Malaysia ilisitisha miradi ya mabilioni ya dola ikieleza kwamba ubora na thamani ya miradi hiyo haiendani na kiwango ambacho China ilipanga kukitumia kuijenga.
Nchi za magharibi pia imekua ikiitupia lawama China kwa kuziweka nchi masikini kwenye lindi la madeni lakini China imekua ikipuuzia tuhuma hizo.
Mwaka 2018 China ilitwaa bandari ya Srilanka ambayo itaimiliki kwa kipindi cha miaka Mia moja sababu nchi hiyo ilishindwa kulipa mkopo iliyochukua toka Uchina.
Nchi za Africa zimetajwa kupendelea mikopo ya Uchina sababu haina masharti magumu kama Ile ya nchi za magharibi