China yanyonga waliohusika na kashfa ya maziwa – wahusika Richmond na EPA vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

China yanyonga waliohusika na kashfa ya maziwa – wahusika Richmond na EPA vipi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magezi, Nov 24, 2009.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  China imewanyonga watu wawili waliotiwa hatiani katika kashfa ya maziwa ya unga yaliyosababisha vifo vya watoto sita.

  Zaidi ya watoto wengine 300,000 waliugua baada ya kutumia maziwa hayo ya unga yaliyokuwa yamechanganywa na kemikali inayotumiwa kutengeneza mbolea na bidhaa za plastiki.

  Zhang Yujun na Geng Jinping ndio watu pekee walionyongwa kuhusiana na kashfa hiyo.
  Washtakiwa wengine kumi na tisa walihukumiwa vifungo vya jela.

  Zhang Yujun alishtakiwa kuhatarisha afya ya umma kwa kutumia njia hatari baada ya kuuza zaidi ya tani 770 za maziwa hayo ya unga kuanzia mwezi Julai mwaka 2007 hadi mwezi Agosti mwaka 2008.

  Geng Jinping, aliyekuwa akisimamia uzalishaji wa maziwa hayo, alitiwa hatiani kwa kusambaza maziwa hayo kwa kampuni ya Sanlu Group ambayo sasa imefilisika, pamoja na kampuni nyingine za maziwa.

  Watu hao walihukumiwa mwezi Januari huko Shijiazhuang, mji mkuu wa Hebei, ilipokuwa makao makuu ya Sanlu. Rufaa yao ilitupwa na mahakama kuu ya Hebei mwezi wa Machi.


  Source: BBC
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Tafadhali kikwete tunataka wahusika wa Richmond, EPA, Kagoda, Kiwira, Radar, Meremeta, Deep Green, Buzwagi n.k. wahukumiwe kwa sheria za china haraka na kama na wewe unahusika sheria hizo hizo zitumike.
   
 3. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  china haina mchezo kwenye mambo yao ndio maana nchi yao inaendelea kwa kasi sana, kwetu tz ni kupiga midomo tu na ahadi za uongo ili kuridhisha watu kwamba kuna uwajibikaji. fikiria jitu limeiba pesa za serikali eti linaona haya linaamua kujiuzulu wakati huohuo bado ni mbunge, sasa mtu kama huyo kweli kuna kilichoharibika kwake zaidi ya kujipanga tena ili atoke vipi next time. Hawa mafisadi ndio haohao viongozi wetu, so hawawezi kuunga mkono sheria kali kama hizo kozi wanajua either watajinyonga wao wenyewe au watawanyonga marafiki na ndugu zao waliowakingia vifua vya kutafuna pesa.... hili suala linakera.. yaani ukitaka ukose raha duniani we anza kuizungumzia tz kwenye kipengele hiki..... inaleta hasira na uchungu mkubwa sana..........mafisadi wote wanastahili adhabu kali kama hiyo ya kifo ndio itakuwa fundisho.
   
 4. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2009
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  yani kama tungetimia sheria za china ungekuta tumesha wasahau wakina EL,RA siku nyingi
   
 5. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  We are in Tanzania. Sheria zitakazotumika ni za kitanzania na si za china. Labda bunge libadili seria za TZ zifanane na za China,lakini pamoja na hayo,
  Kwa Tanzania hilo halitawezekana.
   
 6. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,407
  Likes Received: 3,738
  Trophy Points: 280
  Watakonusurika ni wachache saaanaaa kama sheria hiyo itatumika TZ
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  na kweli hapa tungekuwa tiumeshawasahau muda mrefu lakini kwa nchi yetu kula kiulaiiiiiiini
   
Loading...