China yalipiza kisasi dhidi ya Marekani kuhusu Hong Kong

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,189
4,103

China imesitisha ziara ya manowari ya Marekani na kuiwekea vikwazo asasi moja ya Kimarekani, ikiwa ni hatua ya kulipa kisasi kutokana na kusainiwa kwa muswada unaowaunga mkono waandamanaji wanaodai demokrasia mjini Hong Kong.

Mji huo wa Hong Kong ulio kitovu cha biashara, umekumbwa na machafuko yanayozidi kugeuka ghasia kwa karibu miezi sita ya kudai uhuru zaidi, ambapo Beijing inasema yanachochewa na ushawishi wa mataifa ya kigeni.

Wiki iliyopita rais Donald Trump alitia saini muswada wa haki za binadamu na demokrasia wa Hong Kong, ambao unamtaka rais kupitia hali ya biashara ya mji huo kila mwaka na kutishia kuuondoa ikiwa uhuru wake nusu utayumbishwa.

Hatua hiyo ilikuja wakati mataifa hayo mawili yaliyo na nguvu duniani kiuchumi yakijaribu kukamilisha mpango wa awamu ya kwanza katika vita vya muda mrefu vya kibiashara.
 
Back
Top Bottom