China yakubali kujenga Reli ya Kati kwa kiwango cha 'Standard Gauge'

Mr. MTUI

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
8,130
8,351
Dar es salaam-25 Aprili, 2016

china.jpg

CHINA imekubali kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa reli ya kati yenye urefu wa kilometa 2,561 kwa kiwango cha kisasa yaani "Standard Gauge" ambao zabuni za ujenzi zinatarajiwa kutangazwa hivi karibuni.

Balozi wa China hapa nchini Mheshimiwa Dkt. Lu Youqing ametoa kauli hiyo leo tarehe 25 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambapo pia amemkabidhi barua yenye ujumbe kutoka kwa Rais wa China Mheshimiwa Xi Jinping.

Katika Mazungumzo hayo Rais Magufuli amemweleza Balozi Lu kuwa Tanzania imedhamiria kuanza ujenzi wa Reli ya kati haraka iwezekanavyo na tayari imetenga fedha kiasi cha shilingi Trilioni 1 katika bajeti yake ijayo kwa ajili ya kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi huo.

"Tuna imani kuwa mradi huu utasaidia kuleta mapinduzi makubwa ya uchumi katika nchi yetu na katika nchi nyingine za Afrika Mashariki na kati zikiwemo Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ndio maana hatutaki kupoteza muda kwa mazungumzo marefu, tunataka kazi ianze na watu waanze kunufaika"
Amesisitiza Rais Magufuli.

Kwa upande wake Balozi China hapa nchini Dkt. Lu Youqing amempongeza Rais Magufuli na serikali yake kwa kujiandaa kwa fedha, vifaa na rasilimali watu kwa ajili ya kutekeleza mradi huu mkubwa na kwamba Serikali ya China, Taasisi za fedha za China na Makampuni mbalimbali yatatoa ushirikiano wote katika utekelezaji wa mradi huu.

"Kama ambavyo Prof. Mbarawa amefanya mazungumzo na Serikali ya China, Taasisi za fedha za China na Makampuni, naahidi kuwa tutaanza kazi kama ambavyo taratibu na viwango vya ujenzi vimewekwa, tutafanya kazi kwa kujali muda, ubora na gharama nafuu"
Amesema Balozi Lu.

Mradi mzima wa ujenzi wa reli ya kati unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 6.8 na umepangwa kutekelezwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa kilometa 1,216 za kutoka Dar es salaam - Tabora - Isaka - Mwanza na itajengwa kwa ushirikiano wa Tanzania na China.

Tayari Rais Magufuli amemtuma Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa Mnyaa kwenda nchini China kukamilisha mazungumzo juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ukiwemo wa ujenzi wa reli ya kati, ambapo Prof. Mbarawa anasema hatua inayofuata sasa ni kutangaza zabuni ya ujenzi wa reli hiyo kwa uwazi, ili makampuni mbalimbali ya ujenzi yaombe na hatimaye kupata washindi watakaoanza kazi mara moja.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

==========
Tujikumbushe:

Sun May 31, 2015 | 6:48 AM EDT

Tanzania awards $9 bln rail projects to Chinese companies

DAR ES SALAAM (Reuters) - Tanzania has awarded contracts to build new railway lines worth about $9 billion to Chinese firms, its transport minister said, expanding Beijing's presence in East Africa's second-biggest economy.

Transport Minister Samuel Sitta told parliament on Saturday a Chinese consortium had been awarded a contract to build a 2,561 km (1,536 miles) standard gauge railway connecting Dar es Salaam port to land-locked neighbours at a cost of $7.6 billion.

"A consortium of Chinese railway companies led by China Railway Materials (CRM) has been picked to help us build the railway line," he said.

The consortium will provide 10 percent of the funding for the project while financial adviser Rothschild is finalising procedures for financing of the project through banks, Sitta said.

The minister said construction of the railway line was expected to start in June.

He said Tanzania had signed a framework agreement with another Chinese company, China Railway No.2 Engineering Group Co. Ltd., to build a railway line linking coal and iron ore mine projects, also under development by a Chinese group, to the southern port of Mtwara near big offshore natural gas discoveries.

The 1,000 km standard gauge railway line is expected to cost at least $1.4 billion, according to the Tanzanian government estimates.

Tanzania said in March it planned to spend $14.2 billion to construct a new rail network in the next five years financed with commercial loans, as the country aims to become a regional transport hub.

Tanzania, like its neighbour Kenya, wants to profit from its long coastline and upgrade existing railways and roads to serve growing economies in the land-locked heart of Africa.

Oil discoveries in Kenya and Uganda and gas finds in Tanzania have turned East Africa into an exploration hotspot for oil firms but transport infrastructure in those countries has suffered from decades of under-investment.

Tanzania last year signed an agreement with China Merchant Holding International (CMHI) to build a new mega port and economic zone at Bagamoyo expected to cost at least $10 billion.

China is also financing a $1.2 billion, 532 km (330 mile) natural gas pipeline in Tanzania.
(Reporting by Fumbuka Ng'wanakilala. Editing by Jane Merriman)
 
Kuna wanaJF humu wanadai "Tanzania ya Serikali ya Magufuli haina mwelekeo". Nawakumbusha yafuatayo yanayoongoza utendaji wa serikali:

1) Sera na Mikakati mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiteknolojia (km Vision 2025, MKUKUTA, Water Policy, Energy Policy, nk). Ni vizuri mkaisoma kabla ya kushutumu utendaji wa Serikali.

2) Sera na Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Isomeni na kuielewa kabla ya kukosoa.

3) Rejeeni hotuba za Rais Magufuli, wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2015, na baada ya kuteuliwa, kuapishwa na kuanza kazi kama Rais.

HAPA NI KAZITU#
 
wataisoma namba...mana hyo reli yao ya km 600 wanavyoipigia promo utafikiri nini sijui..sasa sisi tunajenga ya km 2561. Hatare
Kuna vitu 3
Hawa nakuambia Awamu hii ya Magu wata kubari
1. Uchumi
2.Reli
3.highway
Hawa hivi vitu vimekuwa ngonjera kwao
Tunafunika kila kitu
Kwanza ni 128km dar-chalinze super highways

Pili ni
Dar-kigoma
Tabora-Mwanza
Isaka - Kigali
Reli yakisasa

Mbona tutaelewana
 
Kuna wanaJF humu wanadai "Tanzania ya Serikali ya Magufuli haina mwelekeo". Nawakumbusha yafuatayo yanayoongoza utendaji wa serikali:

1) Sera na Mikakati mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiteknolojia (km Vision 2025, MKUKUTA, Water Policy, Energy Policy, nk). Ni vizuri mkaisoma kabla ya kushutumu utendaji wa Serikali.

2) Sera na Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Isomeni na kuielewa kabla ya kukosoa.

3) Rejeeni hotuba za Rais Magufuli, wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2015, na baada ya kuteuliwa, kuapishwa na kuanza kazi kama Rais.

HAPA NI KAZITU#
Hawa wana hali ngumu kwasasa
Hawana hoja
Wala usisumbue akili yako
Wenyewe wanafahamu
Serikali hii ya Magu nihabari nyingine
Tatizo nikuwa wengi wao wanaishi na kula kupitia siasa
Unadhani watafanyeje zaidi ya kutapatapa

TANZANIA KWANZA
#HAPA KAZI TU
 
Kila mara hua nasema kuhusu positive action za Tz muda huu kuliko kenya mwishoe naambiwa mm mtz,,but the tym will tell
Wanaishi kwa sifa
Kwahio ukiwa sio mpenda sifa
Utaitwa Mtanzania
Wadharau kwani hawa kuishi wala kukupa mshahara
Kama mkenya utaendelea kuwa mkenya
Wachana na VILAZA hawa wachache
 
Kuna wanaJF humu wanadai "Tanzania ya Serikali ya Magufuli haina mwelekeo". Nawakumbusha yafuatayo yanayoongoza utendaji wa serikali:

1) Sera na Mikakati mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiteknolojia (km Vision 2025, MKUKUTA, Water Policy, Energy Policy, nk). Ni vizuri mkaisoma kabla ya kushutumu utendaji wa Serikali.

2) Sera na Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Isomeni na kuielewa kabla ya kukosoa.

3) Rejeeni hotuba za Rais Magufuli, wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2015, na baada ya kuteuliwa, kuapishwa na kuanza kazi kama Rais.

HAPA NI KAZITU#
Peleka huko ccm yako, sisi tunataka maendeleo.
Hapa msituletee upuuzi wenu wa fisiem wala ukawa, tunatiana kinyaa hapa, siasa zenyewe mnafanya maigizo..
We need actions hizo vyama msilete hapa kwenye miradi ya serikali.
Huo ni upuuzi, issue ni ya nchi watu tunalipa kodi, Mi nakatwa 14% PAYE halafu mpuuzi anahusisha kodi yangu na chama chake. Upuuzi huu,
Waliopewa dhamana wafanye kazi, sifa za mavyama yenu pelekeni hukohuko.
Lol.
 
Kuna wanaJF humu wanadai "Tanzania ya Serikali ya Magufuli haina mwelekeo". Nawakumbusha yafuatayo yanayoongoza utendaji wa serikali:

1) Sera na Mikakati mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiteknolojia (km Vision 2025, MKUKUTA, Water Policy, Energy Policy, nk). Ni vizuri mkaisoma kabla ya kushutumu utendaji wa Serikali.

2) Sera na Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Isomeni na kuielewa kabla ya kukosoa.

3) Rejeeni hotuba za Rais Magufuli, wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2015, na baada ya kuteuliwa, kuapishwa na kuanza kazi kama Rais.

HAPA NI KAZITU#
Usijisumbue bro
We sema2 kuwa ni miezi miezi6 tangu aingie madarakani
Ila UCHAMA auhusiki
 
Back
Top Bottom