China yakomesha sera ya watu kuwa na watoto wawili pekee

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,862
Mimba

China sasa imewaruhusu watu kuwa na hadi watoto watatu baada ya kupungua kwa kiwango cha watoto wanaozaliwa nchini humo.Hatua hiyo ni mabadiliko makubwa ya kisera kwa serikali ya nchi hiyo.

Shirika la habari linalomilikiwa na serikali Xinhua, limesema uamuzi huo ulitangazwa siku ya Jumatatu katika mkutano wa viongozi wakuu wa chama cha kikomunisti .

Tangazo hilo linajiri baada ya matokeo ya hesabu ya watu inayofanyika kila baada ya miaka kumi kuonesha kwamba idadi ya Wachina ilisajili ukuaji mdogo sana katika miongo iliyopita.
Hatua hiyo imeishinikiza Beijing kubadilisha sera ili kuwauhusu watu kuwa na watoto watatu.

China ilifutilia mbali sera yake ya mtoto mmoja mnamo 2016, na kuibadilisha na kikomo cha watoto wawili ambacho kimeshindwa kusababisha kuongezeka kwa idadi ya watu .

Gharama ya kulea watoto katika miji imezuia wanandoa wengi wa China kuza watoto zaidi.Hatua hiyo ya hivi karibuni iliidhinishwa na Rais Xi Jinping katika mkutano wa viongoziwakuu wa kisiasa shirika la habari la serikali limesema Kutakuwa na "hatua za kuunga mkono, ambazo zitasaidia kuboresha muundo wa idadi ya watu wa nchi yetu, kutimiza mkakati wa nchi kukabiliana kikamilifu na idadi ya watu waliozeeka na kudumisha faida na utoaji wa nguvu azi ", Xinhua ilisema.

Lakini wataalam wengine walikuwa na wasiwasi juu ya athari ya sera hiyo"Ikiwa kulegeza sera ya idadi ya watoto kungekuwa na ufanisi, sera ya sasa ya watoto wawili inapaswa kudhibitishwa kuwa na ufanisi pia," Hao Zhou, mchumi mwandamizi huko Commerzbank, aliambia Reuters."Lakini ni nani anataka kuwa na watoto watatu? Vijana wanaweza kuwa na watoto wawiliiwapo ni wengi. Suala la msingi ni gharama ya maisha ni kubwa sana na shinikizo za maisha ni kubwa sana."

BBC Swahili
 
Ili. ku maintain population ya nchi yoyote inabidi kila mwanamke azae watoto 2.2 .lakini sasa maishani hakuna fraction ya mtu, hivyo inabidi kila anayeweza awe na watoto 3 kamili Chini ya hapo nchi yoyote idadi ya watu wanapungua mifano ni Russia na Japan. Kupungua kwa watu kunashusha maendeleo na wakizidi umaskini hukithiri. Ndio maana Japan anawekeza sana kwenye technologia ya Robots zone zifanye Kazi za binadamu
 
Gharama za malezi ya watoto kwa ujumla ni kubwa sana kwa China ya sasa. Ni changamoto kubwa sana kwa familia nyingi. Hali hii ndiyo iliyopelekea sera ya watoto wawili (2) kutoleta matokeo ya kuridhisha.

Suala la muhimu au la msingi zaidi ni kutengeneza mazingira yatakayo rahisisha gharama za malezi (childcare). Haya maamuzi ya kuwaambia watu wazaliane tu si suluhisho la kudumu la tatizo.
 
View attachment 1803515
China sasa imewaruhusu watu kuwa na hadi watoto watatu baada ya kupungua kwa kiwango cha watoto wanaozaliwa nchini humo.Hatua hiyo ni mabadiliko makubwa ya kisera kwa serikali ya nchi hiyo.

Shirika la habari linalomilikiwa na serikali Xinhua, limesema uamuzi huo ulitangazwa siku ya Jumatatu katika mkutano wa viongozi wakuu wa chama cha kikomunisti .

Tangazo hilo linajiri baada ya matokeo ya hesabu ya watu inayofanyika kila baada ya miaka kumi kuonesha kwamba idadi ya Wachina ilisajili ukuaji mdogo sana katika miongo iliyopita.
Hatua hiyo imeishinikiza Beijing kubadilisha sera ili kuwauhusu watu kuwa na watoto watatu.

China ilifutilia mbali sera yake ya mtoto mmoja mnamo 2016, na kuibadilisha na kikomo cha watoto wawili ambacho kimeshindwa kusababisha kuongezeka kwa idadi ya watu .

Gharama ya kulea watoto katika miji imezuia wanandoa wengi wa China kuza watoto zaidi.Hatua hiyo ya hivi karibuni iliidhinishwa na Rais Xi Jinping katika mkutano wa viongoziwakuu wa kisiasa shirika la habari la serikali limesema Kutakuwa na "hatua za kuunga mkono, ambazo zitasaidia kuboresha muundo wa idadi ya watu wa nchi yetu, kutimiza mkakati wa nchi kukabiliana kikamilifu na idadi ya watu waliozeeka na kudumisha faida na utoaji wa nguvu azi ", Xinhua ilisema.

Lakini wataalam wengine walikuwa na wasiwasi juu ya athari ya sera hiyo"Ikiwa kulegeza sera ya idadi ya watoto kungekuwa na ufanisi, sera ya sasa ya watoto wawili inapaswa kudhibitishwa kuwa na ufanisi pia," Hao Zhou, mchumi mwandamizi huko Commerzbank, aliambia Reuters."Lakini ni nani anataka kuwa na watoto watatu? Vijana wanaweza kuwa na watoto wawiliiwapo ni wengi. Suala la msingi ni gharama ya maisha ni kubwa sana na shinikizo za maisha ni kubwa sana."

BBC Swahili
They have no option as the your population is soo needed and has importance in economic growth through engagement in various sectors.
China is facing aging problem, with life expectancy currently standing at 75 yrs from previously 67 yrs and with decreased fertility to 1.7 from 2.8 this is likely to create a setback to economic growth if appropriate measures are aimed at stimlating population growth are not going to be implemented.
 
Athari ya kutokuzaliana ndio wanaiona sasa,
Huwezi kwenda kinyume na nature ukafaidika,
Ni bora kuwa wengi mule kidogo, kuliko kuwa wachache mumwage chakula
 
Back
Top Bottom