China yakamata watu 99,000 wanaojihusisha na utapeli kwa njia ya simu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
Wizara ya Usalama wa Umma ya China imesema, Polisi nchini humo imefungua kesi 118,000 za uhalifu wa utapeli kwa kutumia simu za mkononi na kuwakamata watu elfu 99 wakati wa operesheni ya "Cloud Sword" iliyoanza mwezi Juni mwaka huu.

Mkurugenzi wa Idara ya Uchunguzi wa Uhalifu iliyo chini ya Wizara hiyo Liu Zhongyi amesema, katika operesheni hiyo, wizara ilipeleka askari kutoka mikoa 13 nchini Cambodia, Philippines na Laos.

Pande hizo nne zimeshirikiana kuharibu idadi kubwa ya magenge ya uhalifu na kuwarejesha nchini China watu 2,553 wanaoshukiwa kujihusisha na utapeli kwa kutumia simu za mkononi.

Amesema operesheni hiyo imechangia kuendelea kwa utulivu wa hali ya usalama wa jamii, na kwamba kuanzia Januari hadi Novemba mwaka huu, idadi ya kesi za uhalifu zilizofunguliwa nchini China zimeshuka kwa asilimia 3.9.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom