jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 35,034
- 28,201
China yalipiza kisasi kwa kuongeza ushuru kwa bidhaa za Marekani
China imesema leo kuwa itaongeza ushuru kwa bidhaa za Marekani za thamani ya dola bilioni 60 kuanzia Juni mosi, katika hatua ya kujibu duru ya karibuni ya Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa za China na mipango ya Marekani kuzilenga bidhaa zote zinazoingizwa nchini mwake kutoka China.
Tangazo hilo limekuja baada ya mazungumzo ya karibuni kabisa ya biashara kati ya Marekani na China kumalizika Ijumaa bila makubaliano, na baada ya Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa za China za thamani ya dola bilioni 200.
Licha ya hatua hiyo ya kulipiza kisasi, China imeonekana kutoa muda zaidi wa hadi Juni mosi. Ushuru mpya utazilenga bidhaa kadhaa za Marekani kuanzia asilimia tano hadi 25. Jibu la China limetangazwa mara tu baada ya Trump kuionya kutolipiza kisasi.
Awali, msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya China Geng Shuang alisema kuwa China hitawahi kusalimu amri kwa shinikizo la kimataifa.
==================
China has decided to impose tariffs of 25 percent, 20 percent and 10 percent on certain U.S. products starting June 1, announced the Customs Tariff Commission of the State Council in a statement issued Monday.
The tariffs will be targeting U.S. goods worth 60 billion U.S. dollars, the statement said, adding that the products under five percent tariff cap would not be affected by this round of tariffs.
SOURCE: CGTN