China yafuta uzazi wa mpango, ruksa kuzaa watoto zaidi ya mmoja sasa

Tanzania hatupangii watu kuwa na watoto wangapi wala Tanzania hatuna Hospital special za kutoa mimba kama China! Sasa sijui mnaongea nini inawezekana hamjui. Uzazi wa mpango wa Tanzania ni ushauri ambao hata US upo hii inasaidia kuondokana na watu kutokupata watoto wakati hawako tayari na kuhakikisha watoto wanapishana miaka. Sababu kubwa ni kutokana na ukweli kwamba Africa bado tuna vifo vya uzazi. Vilevile uzazi wa utotoni. China wameruhusu kutoka mmoja mpaka wawili wa tatu serikali inatoa mimba! Mnajua hilo au mnaongelea China bila kujua.
BAVICHA
 
Mtaji wa ccm ni wajinga na umasikini wa Watanzania.Kisha unatumia utegemezi wao mfano nitawapa elimu bure, madawa,maji,umeme nk...
Tusijilinganishe na China.
Kama tunahitaji mifumo na taasisi imara.
 
Tanzania hatupangii watu kuwa na watoto wangapi wala Tanzania hatuna Hospital special za kutoa mimba kama China! Sasa sijui mnaongea nini inawezekana hamjui. Uzazi wa mpango wa Tanzania ni ushauri ambao hata US upo hii inasaidia kuondokana na watu kutokupata watoto wakati hawako tayari na kuhakikisha watoto wanapishana miaka. Sababu kubwa ni kutokana na ukweli kwamba Africa bado tuna vifo vya uzazi. Vilevile uzazi wa utotoni. China wameruhusu kutoka mmoja mpaka wawili wa tatu serikali inatoa mimba! Mnajua hilo au mnaongelea China bila kujua.
Wewe unaejua uko China, mnavyofanya na wachina wenzenu mtujulishe
 
Kujifananisha na taifa ambalo halipokei misaada ya mpango wa uzazi,ARV, tb, utapiamlo, mabusha na matende, be serious
Tukijifanya wabishi tukafyatua watoto, izo dawa za uzazi wa mpango,ARV, TB, Surua, na chanjo za watoto watatuuzia sasa apo tutajifia na kurudi ktk idadi ile ile. Mzungu mtu wa maesabu sana
 
Mwaka 1980 China mwanamke mmoja alikuwa anaweza kuzaa watoto 4.7 wakati huo Tanzania ilikuwa watoto 6. Wachina waliamua kuanza kuzaa mtoto mmoja tu kwa couple ili kupunguza wimbi l ukuaji kwa kasi wa watu. Hadi mwaka jana (2017). China ilishusha idadi ya watoto kwa mwanamke mmoja kutoka 4.7 (1980) hadi 1.7 (2017). Wakati Tanznania idadi hiyo imeshuka kutoka 6 (1980) hadi 4.7 (2017). Idadi hii kwa Tanzania inaifanya kuwa ya 17 duniani kwa mwanamke mmoja kuzaa watoto wengi!!! Tafakari

Mwaka 1960, watanznia walikuwa takribani milioni 12, na sasa tuko takribani milioni 56 (2018) yaani ongezeko la watu wastani wa watu 771,929 (wastani wa 3% kwa mwaka)!! Tafakari

Taarifa
Idadi ya watoto kwa nchi ambazo miaka ya 80 tulikuwa tunaelekeana kiuchumi
Malaysia 2.5
Singapore 0.83
Mauritius 1.75 estm
China 1.7
Tanzania 4.7!
Dunia 2.5 est.

TAFAKARI!!!
 
Hao Wachina wala hawatazaa sana kihivyo hasa ktk zama hizi ambapo uchumi wao sasa utaanza kuporomoka kufuatia zile Trade Tariffs za Marekani.

Gharama ya maisha nchini China inapanda kwa kasi na maisha ni magumu ndio maana Wachina wengi wanaenda nje kwenda kutafuta maisha hadi wengine wanaishia kufanya tu umachinga ugenini.

Na kwa kuwa kwa sasa Wachina wana idadi kubwa ya wasomi spidi yao ya kuzaa kiuzoefu haiwezi kuwa kubwa kwani penye idadi ndogo ya wasomi birth rate huwa juu. Huku tuendako uchumi wa China unatarajia kuanza kushuka.
 
tattizo wengi hamjui uzazi wa mpango ninini kama boss wenu mzee wa fyatueni. tanzania hatuna sheria ya limiti ya watoto. idadi ya kuzaa ni nguvu zako tangu zaman. kinacho zuiwa ni kuzaa kwa mpangilio. hata sijui JPM alikua anapinga nn. kwamba nyie huyu boss wenu alitaka kila mwaka watu wazae yaan huyu yuko miez sita huku mama mimba nyingine??
una muhoji" mtu anayejiita" Kichaa" !?
 
Hao Wachina wala hawatazaa sana kihivyo hasa ktk zama hizi ambapo uchumi wao sasa utaanza kuporomoka kufuatia zile Trade Tariffs za Marekani.

Gharama ya maisha nchini China inapanda kwa kasi na maisha ni magumu ndio maana Wachina wengi wanaenda nje kwenda kutafuta maisha hadi wengine wanaishia kufanya tu umachinga ugenini.

Na kwa kuwa kwa sasa Wachina wana idadi kubwa ya wasomi spidi yao ya kuzaa kiuzoefu haiwezi kuwa kubwa kwani penye idadi ndogo ya wasomi birth rate huwa juu. Huku tuendako uchumi wa China unatarajia kuanza kushuka.
Sababau nyingine ni kuwa idadi yao kwa sasa haiongezeki na hao wazee wakishaondoka hapo baadae idadi yao itapungua mpaka kufikia kweye milioni 700 hivi, kwa hiyo ilibdid wabadilishe sheria.
 
Kwa muda mrefu wachina wamesha kuwa na uelewa wa kutosha. kuhusu uzazi wa mpango kwahiyo mtu ambaye atakuja leo hii kichwa kichwa na kusema wachina wazaane kama kuku. huyo lazima wachina watamuona ni mwizi tu anataka kuwaibia aikili.
 
Back
Top Bottom