China yafuata ahadi ya kuongeza uagizaji wa bidhaa kutoka Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,006
1,026
VCG111258465501.jpg


VCG111258465518.jpg


VCG111356412694.jpg


China na nchi za Afrika zimekubaliana kuitisha mkutano wa ngazi ya mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC tarehe 29 hadi 30 mwezi huu mjini Dakar, Senegal. Pande hizo zinafikiria kufikia makubaliano ya kuhimiza zaidi maendeleo ya biashara yaliyo na uwiano na uendelevu kati yao.

Mwaka 2018, wakati viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika walipokusanyika Beijing kuhudhuria mkutano wa kilele wa FOCAC, rais Xi Jinping wa China aliahidi kuongeza uagizaji wa bidhaa zisizo za maliasili kutoka Afrika. Katika miaka hii mitatu, China imeandaa shughuli kama Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji wa Bidhaa kutoka nje ya China CIIE, Maonyesho ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika CAETE, sikukuu ya kutangaza bidhaa za Afrika kupitia mtandao wa internet n.k, shughuli ambazo ni hatua halisi za kusaidia bidhaa za Afrika kuingia kwenye soko la China.

Kwa mujibu wa Wizara ya Biashara ya China, katika miezi saba ya mwanzo ya mwaka huu, thamani ya biashara kati ya China na Afika iliongezeka kwa asilimia 40.5 na kufikia dola za kimarekani bilioni 139.1. haswa kadri bidhaa za Afrika zinavyopendwa zaidi katika soko la China, uagizaji bidhaa kutoka Afrika uliongezeka kwa asilimia 46.3 na kufikia dola za kimarekani 59.3. Wachambuzi wamekadiria kuwa kama mwelekeo wa sasa unaendelea, mwaka huu biashara ya China na Afrika inatarajiwa kuweza kuondokana na athari mbaya za janga la COVID-19 na kurudi kwenye kiwango cha kabla ya kutokea kwa janga hilo mwaka 2019.

Ili kupanua vyanzo vya uagizaji soya kutoka nje, kuanzia mwaka jana China imenunua soya kutoka Tanzania. Pararachi, chai, kahawa na maua ya waridi ya Kenya, kahawa ya Rwanda na bidhaa za nyama ya ng’ombe za Namibia na Botswana pia zimeingia kwenye soko la China kwenye mtandao wa internet au kwa njia ya ana kwa ana.

Katika kipindi hicho, mvinyo wa Afrika Kusini ulioingia kwenye soko la China uliongezeka kwa asilimia 192.8, kiasi ambacho kinaongoza miongoni mwa nchi zote. Waswahili husema, ahadi ni deni. Kitendo cha China kuongeza kwa wingi uagizaji wa bidhaa haswa mazao ya kilimo kutoka Afrika kimewawezesha raia wa Afrika kunufaika kihalisia na ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Afrika.

Mkurugenzi wa idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wu Peng mwezi uliopita alisema, ili kusaidia bidhaa za Afrika kuingia kwenye soko la China, nchi hiyo itatangaza hatua kabambe zinazolenga mkutano wa Dakar.

Kwa upande mwingine, kadri pato la watu wa China linavyoongezeka, ndivyo mahitaji yao kwa ladha na ubora wa bidhaa yanavyokuwa ya aina mbalimbali. Aidha, China inaweka mkazo kwenye usalama wa chakula. Mambo hayo mawili pia yanaathiri mazao ya kilimo ya Afrika haswa yale mabichi kuingia kwenye soko la China. Nchi za Afrika zinahitaji kuzalisha bidhaa bora, na katika jambo hilo, China imejitahidi kutoa msaada wake kwa kupitia kusafirisha teknolojia.

Mkutano wa FOCAC utakaofanyika mjini Dakar ni mkutano wa ngazi ya juu unaofanyika kati ya China na nchi za Afrika kila baada ya miaka mitatu. Wakati dunia bado haijaondokana na janga la COVID-19, China na Afrika zimeamua kufanya mkutano huo kwa mpango, hii imeonesha jinsi pande mbili ambazo ni nchi kubwa inayoendelea duniani na bara lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea zinavyoaminiana na kuungana mikono. Inaaminika kuwa nchi za Afrika zitakuwa na matarajio makubwa na mkutano huo, kwani sio tu zitaweza kuuza bidhaa zao kwa wingi kwa China, bali pia kutafuta uwekezaji mwingi zaidi kwa ujenzi wa miundombinu barani Afrika.

Profesa wa Chuo Kikuu cha Uchumi na Sayansi ya Siasa cha London Chris Alden hivi karibuni alisema baada ya kutokea kwa janga la COVID-19, ufuatiliaji na msaada uliotolewa na China kwa nchi za Afrika vimeboresha sura ya China barani humo, lakini inaonakena kuwa Afrika imesahauliwa na nchi za magharibi.
 
Hivi hakuna mwekezaji wa kurahisisha uagizaji bidhaa kutoka China?
 
Back
Top Bottom