China yafanikiwa kuviunganisha vyombo vyake angani!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
China imefanikiwa kuviunganisha, vyombo viwili vya kwanza angani visivyokuwa na watu, hatua ambayo ni muhimu, kuelekea kutuma chombo chenye watu kwenye kituo cha anga, ifikapo mwaka 2020. Hadi siku za hivi karibuni, ni Urusi na Marekani pekee, zilizokuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

Msemaji wa kituo cha uendeshaji wa vyombo vya anga cha China, amesema kuwa, chombo kilichorushwa Jumanne iliyopita, kwa jina Shenzhou 8, kimeungana na chombo chengine, kilichorushwa mwezi Septemba, kwa jina Tiangong 1. Hatua inayofuatia sasa, ni majaribio ya kurusha tena vyombo viwili hapo mwakani, huku kimojawapo kikiwa na wanaanga wa Kichina. Shirika la Habari China, Shin-waa, limesema kuwa, kituo cha anga kinachopangwa kujengwa na nchi hiyo, kitawapokea "wanasayansi kutoka ulimweguni kote".
 
Up china,soon and very soon they are going to run the world na sio mataifa ya kishoga kama uingereza!
 
Back
Top Bottom