#COVID19 China yaendelea kutimiza ahadi yake ya kusaidia nchi za Afrika kupata chanjo ya Covid-19 na kuhamisha teknolojia

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,033
12342412.jpg
Hadi mwishoni mwa mwezi Mei China ilikuwa imetoa msaada wa zaidi ya dozi milioni 20 za chanjo ya Covid-19 kwa karibu nchi 40 za Afrika ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kuhakikisha dunia inasonga pamoja kwenye utoaji wa chanjo.

Kama sehemu ya Ushirikiano wa Kusini na Kusini, China iliahidi mwishoni mwa Februari 2021 kutoa chanjo za COVID-19 kwa nchi 19 za Afrika.

Afisa wa Wizara ya Mambo ya nje anayesimamia idara ya Afrika Wu Peng anasema pia China inauza chanjo kwa nchi za Afrika kwa bei nafuu.

"Tunaamini kwamba ni muhimu kuhakikisha kwamba watu wa China wanapata chanjo haraka iwezekanavyo, lakini kwa nchi zingine zinazohitaji, sisi pia tunajaribu kadri tuwezavyo kutoa msaada wa chanjo," anasema Wu.

Taakwimu zinaonesha kuwa kampuni kubwa 4 za kuzalisha chanjo zina uwezo wa kutoa angalau dozi bilioni 2.6 mwaka huu, na hivyo kusaidia nchi nyingi zaidi.

Lakini pia bwana Wu anasema sera ya China siku zote ni kuwezesha nchi za Afrika kujitegemea na kujitosheleza yenyewe kwa mahitaji yake.

Hivyo China inasaidia nchi hizo kuanza kuzalisha chanjo yao wenyewe ili kupunguza gharama na kufanikisha lengo la kuchanja watu wengi.

Misri itaanza uzalishaji wa ndani wa chanjo ya China Sinovac mwezi Juni ambao utawezeshwa na kupata msaada wa utaalam na kiufundi.

Sinovac pia, itatoa leseni ya kutengeneza na kupakia chanjo hiyo huko Misri.

"Msaada pekee hauwezi kutatua masuala ya chanjo ya Afrika. Lazima tuunge mkono utengenezaji wa chanjo za ndani barani Afrika, ingawa hii ni ngumu kutokana na viwango vya chini vya ukuaji wa viwanda, "Wu anasema.

Tarehe 21 mwezi Mei, Misri ilipokea shehena yake ya kwanza ya vifaa vya kutengeneza chanjo ya Sinovac.

Lita 1,400 za chanjo zitatengenezwa kuwa dozi milioni 2 ndogo ambazo zitatumika kwa chanjo huko Misri katika miezi miwili ijayo.

makubaliano kati ya China na Misri pia ni pamoja na kuhamisha teknolojia ya uzalishaji na utengenezaji ili kuwezesha uzalishaji wa ndani wa viungo vya chanjo ya Sinovac katika siku zijazo.

Misri imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kushirikiana na China kwenye uzalishaji wa chanjo hiyo.

Msimamo wa China kwenye suala la kukabili janga la corona umekuwa ni kupitia ushirikiano wa kimataifa.

Mwezi Mei Rais Xi Jinping wa China alitangaza hatua mpya za China kuunga mkono juhudi za kimataifa za kukabiliana na janga la COVID-19.

Hatua hizo ni pamoja na China kutoa msaada wa dola bilioni 3 za kimarekani zaidi kwa nchi zinazoendelea katika miaka mitatu ijayo, ili kuzisaidia kukabiliana na janga hilo na kufufua uchumi.

Alisema pia China itaunga mkono kampuni zake kutoa teknolojia na kufanya ushirikiano na nchi za nje katika kutengeneza chanjo.

China aidha imetangaza kuacha hakimiliki za chanjo yake ya COVID-19, na China inapendekeza kuanzisha kongamano la kimataifa la ushirikiano kuhusu chanjo, ili kuhimiza ugawanyaji wa haki wa chanjo hiyo.

Hatua mpya za China zinajibu wito wa Shirika la Afya duniani wa kuwa na usawa wa utoaji wa chanjo duniani.

Mwishoni mwa mwezi Mei Mshauri mwandamizi wa mtendaji mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Bruce Aylward, alisema hali ya ukosefu wa usawa katika ugawaji wa chanjo ya COVID-19 duniani inaongezeka.

Bw. Aylward amesema kati ya dozi bilioni 1.6 ya chanjo hiyo zilizotolewa, asilimia 83 zimetumiwa na nchi zenye mapato ya juu na ya kati. Licha ya hayo idadi ya upimaji wa virusi vya Corona unaofanywa kila siku katika nchi zilizoendelea, ni mara 125 kuliko ile ya nchi zinazoendelea.

Amesisitiza kuwa kama virusi haviwezi kugunduliwa, maambukizi yake hayatazuilika, na hali hii italeta maafa makubwa.
 
Nafikiri kwenye global rumbling, marafiki wa kweli baina ni 🇬🇧 na 🇺🇸/ 🇺🇸 na 🇮🇱
tuliobaki sidhani kama kuna deep friendship bila unyonyaji ndani yake
China 🇨🇳 wamemaliza kujenga jengo la bunge la zimbabwe 🇿🇼 na jengo la AU 🇪🇹 Lakini deep down pesa kutoka central govt sehemu kubwa imerudi kwenye circulation ndani ya china 🇨🇳

Nafikiri Afrika kuamua tu,CDC-Africa (SA) ingekua kipaumbele kwenye mambo ya chanjo etc, si mbaya kuiga EU 🇪🇺 Integration model
Tungepeana hubs
EA labda flight hub
Southern Afrika wapewe hub
West Afrika
Horn of Afrika
Central etc etc
 
Back
Top Bottom