China yaendelea kuchochea kuimarika kwa biashara ndani ya kundi la nchi za Kusini

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,116
1,121
1735864882611.png


Wakati changamoto za uchumi duniani zikiendelea kuonekana, na wanasiasa wa mrengo wa kulia katika nchi za magharibi wakiendelea na hata kutamka maneno mbalimbali yenye viashiria vya kutatiza biashara huria duniani, takwimu zilizotolewa na Jarida la Guancha la China, zinaonesha kuwa biashara ndani ya kundi la BRICS, na kati ya nchi za kusini kwa jumla inaendelea kushamiri.



Jarida hilo limetoa mfano wa nchi wanachama wa jumuiya ya nchi za kusini mwa Asia (ASEAN), ambazo licha ya biashara miongoni mwao kuendelea katika hali ya kuridhisha, katika kipindi cha hivi karibuni mauzo ya nje ya nchi za eneo hilo yameongezeka kwa 12.7% na uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya eneo hilo umeongezeka kwa 3%. China imekuwa na mchango mkubwa katika maongezeko hayo mawili.



Kinachotokea miongoni kwa nchi za ASEAN, na kati ya nchi za ASEAN na China, kinafanana na kinachotokea kwenye maeneo mengine duniani. Mwishoni mwa mwaka 2023 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Bw. Peter Mathuki, alisema mwaka 2022 thamani ya biashara kati ya nchi wanachama wa jumuiya ilifikia dola za kimarekani bilioni 10.9, ikiwa imeongezeka kwa 12.1% ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Bw. Mathuki pia alisema biashara miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inaweza kuchangia hadi 40% ya jumla ya biashara ya kanda, ikilinganishwa na 15% tu mwaka 2022.

Maeneo haya mawili yanaonesha kuwa ushirikiano miongoni mwa nchi za Kusini na kati ya nchi za Kusini, ni sehemu muhimu ya kujiepusha na hatari ya vitendo vya kujilinda kibiashara vinavyoonekana kujitokeza katika baadhi ya nchi za magharibi, na hata nchi za kaskazini.

Pamoja na ukweli kuwa kwa upande mmoja China imechangia sana ongezeko la biashara kati yake na nchi za Kusini, ni wazi pia kuwa China imefanya juhudi kubwa katika kuchochea biashara miongoni mwa nchi za makundi mengine duniani. Tukiangalia tena mfano wa ongezeko la biashara kati ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, tunaweza kuona kuwa uwekezaji wa moja kwa moja wa China katika uzalishaji wa bidhaa katika nchi wanachama, na hasa bidhaa zinazoweza kuuzwa miongoni mwa nchi wanachama, na ujenzi wa miundombinu inayorahisisha biashara kati ya nchi wanachama, vimekuwa na mchango mkubwa katika kuhimiza ongezeko la biashara.

Iwe ni bandari, barabara, reli au viwanja vya ndege vilivyojengwa kupitia utaratibu wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” (BRI), au kupitia majukwaa mengine ya ushirikiano wa moja kwa moja kati ya China na nchi nyingine, ni wazi kuwa mkono wa China umekuwa na mchango katika kuchochea biashara.

Hivi karibuni Rais Mteule wa Marekani Donald Trump, amesikika akisema nchi za kundi la BRICS, au nchi nyingine yoyote ikijaribu kuondoka kwenye matumizi ya sarafu ya Dola ya Marekani kwenye biashara ya kimataifa, basi zitaadhibiwa kwa kutozwa ushuru wa 100%. Kauli ya Bw. Trump inatokana na hofu kwamba licha ya vitendo vya kujilinda kibiashara, uwezekano wa kudhoofishwa biashara kati ya nchi nyingine unazidi kupungua. Na kwamba njia ya kunufaika na jasho la nchi nyingine zinazotumia dola ya Marekani kufanya miamala kwenye biashara miongoni mwao, iko hatarini

Mwaka 2023 Rais Luiz Inácio Lula da Silva wa Brazil, alipendekeza kuunda sarafu ya pamoja nchini Amerika Kusini ili kupunguza utegemezi wa dola ya Marekani, na kuhimiza biashara miongoni mwa nchi za eneo hilo. Kundi la BRICS pia lina wazo kama hilo, la kuwa sarafu na mbadala kwenye kufanya miamala kati yao kwa lengo la kurahisisha biashara kati yao. Wakati China na nchi nyingine duniani zinatafuta njia ya kuimarisha biashara kati yao, Marekani kwa upande mwingine haifurahi kuona hilo, kama dola ya Marekani haitaendelea kuwa nyenzo ya kuzinyonya nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom