CHINA wakili kuzalisha bidhaa Feki - Mteja akili kumkichwa

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,226
[h=3]Nchi za Afrika lawamani kwa bidhaa feki[/h]

Na Mwandishi Wetu, China

NCHI za Afrika zinawajibika kuingiza na kuruhusu bidhaa feki kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo wafanyabiashara wenye tamaa kusafirisha bidhaa hizo na Serikali katika nchi husika kushindwa kuzikamata wala kuzuia uingizwaji wake.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara Mahusiano ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Bw. Lu Shaye, aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao walihudhuria mkutano wa tano wa Mawaziri katika Kongamano la Ushirikiano kati ya nchi za Afrika na China uliofunguliwa jana.

Mkutano huo ambao umefunguliwa na Rais wa China, Bw. Hu Jintao, ulihudhuriwa na Mawaziri mbalimbali kutoka barani Afrika na maraisi sita ambao ni pamoja na Bw. Jaboc Zuma (Rais mstaafu wa Afrika Kusini), ambapo Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Bernard Membe.

Waandishi walimuuliza Bw. Shaye kama mkutano huo utakuwa na ajenda ambayo itajadili suala la bidhaa feki kupelekwa nchi za Afrika na zile halizi kuuzwa Ulaya na Marekani.

Akijibu swali hilo, Bw. Shaye alisema moja ya sababu kubwa za bidhaa feki ni Serikali za Afrika kushindwa kuzuia kwenye idara zake za ushuru ambapo China inakiri kuwa zipo bidhaa feki ambazo zinazalishwa nchini humo.

“Sio sera yetu kupeleka bidhaa feki katika nchi za Afrika, ukiacha suala la China kuzalisha bidhaa feki, nchi za Afrika zimeshindwa kuzuia bidhaa hizo kuingia katika mipaka yake, mahitaji ya nchi nyingi za Afrika na uwezo wa kununua, yanachangia kuzalishwa bidhaa nyingi za bei rahisi.

“China inaamini pamoja na jitihada kubwa za kupambana na bidhaa feki, imefanikiwa kupunguza uzalishwaji wa bidhaa hizi ambapo wafanyabiashara wasio na nia njema, wamekuwa wakitumia njia mbalimbali kuendeleza uhuni huu,” alisema Bw. Shaye.

Aliongeza kuwa, ajenda ya bidhaa feki haitakuwepo katika mkutano huo bali China itawakilisha mkakati wa kuzisaidia nchi za Afrika kuendesha idara za ushuru na kuzuia uingizwaji wa bidhaa feki.

Bidhaa feki zimekuwa kitendawili kikubwa katika nchi nyingi duniani ikiwepo Tanzania ambapo China imekuwa ikilaumiwa kwa kuzalisha bidhaa zisizo na viwango hivyo kusababisha madhara makubwa kwa watumiaji.

Hata hivyo, Serikali ya China imekuwa mstari wa mbele kupiga vita uzalishwaji bidhaa feki na kasafirishwa nje ambapo mataifa mengi yameilaumu nchi hiyo kuhusiana na suala hilo.

Mkutano huo utazungumzia jinsi China na Afrika zinavyoweza kudumisha mahusiano yaliyopo.
 
Back
Top Bottom