China umenikuna kwa kupiga marifuku biashara ya meno ya tembo

CORAL

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
2,673
2,000
Habari ya China kuamua kupiga marufuku biashara ya meno ya tembo imenikuna hasa. China itatekeleza marufuku hiyo hatua kwa hatua kufikia mwishoni mwa 2017. China na Marekani zilikubaliana kupiga marufuku biashara ya meno ya tembo ili kulinda wanyama hao wasitoweke duniani. Soko la meno ya tembo la China limekuwa kikwazo kikubwa cha mapambano dhidi ya ujangili. Habari kamili hapa New york times
China Bans Its Ivory Trade, Moving Against Elephant Poaching
 

Pakawa

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
6,343
2,000
Wameshatoweka ndio wanatoa matamko! Waache kutufanya zumbukuku! Wameshafaidika ndio wanakuja na statement mbovu kama Hii. Wawakamate basi wote waliojisghughulisha na biashara Hii haramu.
 

CORAL

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
2,673
2,000
Wameshatoweka ndio wanatoa matamko! Waache kutufanya zumbukuku! Wameshafaidika ndio wanakuja na statement mbovu kama Hii. Wawakamate basi wote waliojisghughulisha na biashara Hii haramu.
Halafu kumbe ilikuwa biashara kubwa sana inatambulika kisheria na watu wanalipa kodi. Yaani unaposema wawakamate wote waliojihusisha na biashara hiyo pamoja na processing za meno ya tembo wao wanahangaika kuwatafutia shughuli mbadala ya kufanya. Kwa maneno mengine sweikali ya China ina waonea huruma na hivyo kuwahangaikia wapate kazi nyingine. Ndio maana hawawazuii kufanya biashara hiyo ghafla ila mchakato utachukua karibu mwaka wote wa 2017.
 

Mwanzi1

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
5,724
2,000
Ni mapema sana kujua kama uamuzi wao utazaa matunda, walio onja asali watafanya kila njia kuchonga mzinga.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom