China, Tanzania zatofautiana ujenzi Bandari ya Bagamoyo

spika

JF-Expert Member
Dec 7, 2014
458
426
Pengine ni kwa dhamira nzuri ya serikali kuweka mbele maslahi ya Taifa, au ni muendelezo wa diplomasia hafifu tulioanza kuionyesha awamu hii...

Kimsingi hatuna uzoefu na miradi complex kama hii ambayo ndani ya nchi inahusisha wizara na idara kadhaa za serikali, ukiacha serikali mbili na makampuni kadhaa makubwa ya kigeni..

Tunapaswa kujifunza zaidi katika hili..



Chanzo: China, Tanzania zatofautiana ujenzi Bandari ya Bagamoyo

Balozi wa China nchini, Dk Lu Youqing amesema tofauti kati ya Serikali ya Tanzania na ubalozi wa China umesababisha kukwama kwa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Mchakato wa ujenzi wa bandari hiyo ulianza kipindi cha Awamu ya Nne ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete na ulitarajiwa kuhusisha Serikali za Tanzania, China na Oman.

Akizungumza katika mahojiano na baadhi ya waandishi wa habari juzi jijini Dar es Salaam, Balozi wa China nchini, Dk Lu Youqing alisema, “Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na ukanda wa viwanda wilayani humo ni uwekezaji mkubwa kati ya China na Tanzania katika miaka ya karibuni na umeorodheshwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21).
“Kutokana na umuhimu wake unaohusisha Serikali za Tanzania, China na Oman, ushirikiano kati ya maofisa kutoka idara za Serikali ya Tanzania na ubalozi wa China wanazishauri pande zinazohusika kukunjua moyo na kumaliza tofauti ili uweze kuendelea kukiwa na makubaliano kwenye mambo ya msingi,” alisema Lu.

Hata hivyo, kwa sasa jitihada zinafanywa ili ikiwezekana makubaliano hayo katika nusu ya mwaka huu na ujenzi uanze ndani ya mwaka huu. Akizungumzia hilo kwa njia ya simu jana, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani alikiri kutofatiana na Wachina katika ujenzi huo.“Unajua vitu vingine mnapenda kuvikuza bila sababu. Sisi tuliiruhusu Serikali ya China kujenga Bandari ya Bagamoyo kwa kitu kinachoitwa PPP na ule ujenzi ulikuwa na mambo mengi kama maeneo ya viwanda ili kupata uhakika wa mizigo. Wachina wakatuletea kampuni kwamba sasa ongeeni na kampuni hii, tukawa tunaongea tunaangalia terms au unataka tuwape hivi hivi? Alihoji.

Waziri Ngonyani alisema baadaye Wachina walileta Serikali ya Oman kwenye mradi huo.
“Hivyo vingine vyote wanatafuta tu sababu ya kutuchelewesha. Mara ya mwisho tumewaambia lazima yale maeneo tuliyobishania tukubaliane ifikapo Februari 28. Kwa hiyo tunatarajia kupata taarifa ya mwisho ya ujenzi wa bandari hiyo kutoka kwa contractors wa China na Oman,” alisema.
 
Ajabu!! Wadau wengi humu walilalamikia mchakato mzima wa ujenzi huo. Leo umesimama tumeanza malalamiko tena!! Hivi tunataka nini sisi!?
 
Ajabu!! Wadau wengi humu walilalamikia mchakato mzima wa ujenzi huo. Leo umesimama tumeanza malalamiko tena!! Hivi tunataka nini sisi!?
Mchakato uendelee, faida ni nyingi kuliko hasara
 
Mm Kwa elimu yangu ndogo ya darasa la saba lakini nimekaa Mjini miaka zaidi ya 20 na Mjini kuna magazeti ya aina nyingi hivyo elimu yangu imepanuka na kufikia kidoto cha sita, tanzania tunaachwa mbali kiuchumi na nchi Jirani na hasa kenya ambaye tunajinasibu kuwa tunamkaribia hadi mnashinsanisha jiji letu la daresalaam na jiji la nairobi, mhuu imbi langu kwa watanzania jaribuni kujiongeza angalau kutembelea majiji ya wenzetu uone wenzetu wako vipi hata ukitaka kulinganisha uwe na picha halisi ya majirani zetu na ustarabu wao na ubaya vilevile! Kuna ushindani vilevile wa kiuchumi kati ya nchi zetu! Mhemko mwingine ni ule wa bomba la mafuta la uganda ambalo awali lilikuwa lipitie kenya lakini kwa sababu za kijiografia waganda wakabadili msimamo wao na wakakubali na bomba hilo kwa sasa litapia tanzania kutoka hoima uganda lakini wezetu wa kenya walikubali yaishe na Kwa haraka wakaelekeza nguvu zao za ujenzi wa reli kutoka mombasa kupitia uganda hadi rwanda na DRC wakati sisi tukiwa na mpango huu wa ujezi wa reli ambayo itaenda hadi Uganda, Rwanda, burundi na congo lakini kwa sisi tanzania bado tunasuasua kisa mradi wa ujezi wa reli ya Kenya ilikuwa na ufisadi mkubwa kutoka kwa wachina lakini wezetu kenya reli yao inaenda mbio na mwezi ujao rain ya kwanza ya mizigo itafika nairobi kutoka mombasa, wakati huo sisi hatutaki kuibiwa na kuhesabia hela zetu mfukoni lakini wenzetu wanasonga mbele, ninaimani hiyo reli ya kenya ikikamilika hakuna nchi rafiki atakayekubali kupitisha mizigo bandari ya daresalaam kwani kupitisha kwetu ni gharama Sana, mfanyabiashara gani atapenda hasara badala ya faida?watanzania tufanye kongamano la kitaifa tutafute nani mchawi aliyetuloga! tunakuja ku deal na vitu ambavyo havija faida kubwa kwa watanzania! Mungu ipendelee nchi yetu!
 
Mkuu wacha sisi tuendelee kupambana na majizi..na wakati huo huo tukiendelea kujihakikishia kwamba hatuna cha kuibiwa.
 
Back
Top Bottom