China - Tanzania Security wameshindwa kuilinda miundombinu ya UDART (Mwendokasi)

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
May 23, 2008
1,932
985
CT Security ndiyo waliopewa jukumu la kulinda miundombinu ya Mradi wa mabasi ya mwendokasi: Kimara hadi Kivukoni, Morocco hadi Gerezani, Depot yao pale Jangwani na feeder stops kama zile za Shekilango, Kinondoni.

Katika feeder posts sasa hivi kumeshaanza kufunguliwa bolt na nuts zake. Tunakokwenda huko...mmh!!

Kwa upande wa vituo vya Ubungo na Kimara ndiko hali ni mbaya zaidi. Pamoja na kwamba kabla ya kupanda madaraja au kutoka katika vituo hivyo kuelekea madarajani kuna alama za makatazo ya kuzuia watu kukaa/kusimama kwa muda, kutokupiga picha, kutokufanya biashara, n.k. vitu hivyo vinafanyika.

Pamekuwa utupaji wa chupa zenye mikojo na watu pia kukojoa katika baadhi ya kona.

Kituo cha Ubungo ni aibu kubwa. Nguzo karibu zote za madaraja ya waenda kwa miguu kituoni hapo ni rundo la mikojo na nyingine kinyesi pia. Njia ya wheel chairs kuingia kituo cha UBT imekuwa ina vifurushi vya kinyeshi na marundo ya mikojo. Kwenye transformer iliyochini ya daraja, mara tu unapotoka kituoni, kunarundo la mikojo.

Wachafuaji wakubwa ni wale mawakala au vibarua wa mabasi ambao wanadaka abiria na kuwapeleka maofisini au moja kwa moja kwenye mabasi. Mara kadha nimewaona, nao korokoloni wa CT wamewaona lakini hawajakamatwa.

Kuna ukweli kuwa, rushwa ndogondogo wanazopewa walinzi wa CT na hao mawakala na mikwala midogo vinawafanya, kujifanyia watakavyo.

Jambo la ajabu hata wale walinzi wanaotembea na ile Land Cruiser ya patrol wanayaona mengine na kunyamaza kimya.

Sana sana wanaishia kuwa kamata vijana wanaotoka mikoani na kupiga picha na camera za simu, ili wawatishetishe na kuwakamua hela. Wakati huo huo pale juu darajani kuna vijana wawili ni wafanyabiashara za kupiga picha na kila siku wapo hapo.

Nimeambia, sijaona, kuwa vituo vya Posta Mpya na Mwembechai ni malazi ya mateja.

Makubwa yanatakiwa yafanywe dhidi ya kampuni hili la ulinzi ili kunusuru uharibifu wa miundombinu ambayo kila Mtanzania anadaiwa hela ya ujenzi wake. Kwani hata Polisi wanaokwenda kuongeza nguvu, pale Kimara na Ubungo, huishia kukaa vituoni na kuwa wasomaji wa simu na kuchati tu.
 
[SUB]Lile daraja la pale ubungo limejaa mikojo na vinyesi, yaani unashindwa kuelewa kuwa inakuaje mtu mzima na akili zake anavua nguo na kujisaidia pale![/SUB]
 
[SUB]Lile daraja la pale ubungo limejaa mikojo na vinyesi, yaani unashindwa kuelewa kuwa inakuaje mtu mzima na akili zake anavua nguo na kujisaidia pale![/SUB]
Ustaarab kweli kwetu ni mgumu yani sometimes mimi jitu zima kabisa uwa narusha kopo la maji barabarani sijui akili nakuwaga nimeiweka wapi.
 
Waacha wahangaike na CDM huku mambo mengine yaende combo kisa woga unaoongozwa na hofu
 
Hili suala wakabiziwe Vijana wa Jkt ....Sumajkt......Mtaona mabadiliko soon tuuuuu....
 
Mkuu nimetuma post yako kwenye email ya TAMISEMI ambaye ndiye mkono wa serikali huko kwenye mradi.
Lkn pia pale kituo cha Ubungo mabati yameanza kung'oka na wala hakuna anayechukua hatua za kukarabati kuyarudishia. Ni aibu, ni fedhea, Inatia hasira na wakati mwingine unajiuliza hivi kwa akili zetu MRADI WA SGR tutauweza Kuuhudumia kweli??? Vip ile Terminal Uwanja wa Ndege wa Kisasa?? Kwanini akili zetu hazifikirii kuhusu MATENGENEZO??
 
Wanaoharibu miundombinu, ni wapiga kura wangu, MSIWABUGHUZE alisikika mtu mmoja akiongea.
 
Wameshindwa kabisa bida boda kariakoo na postal wanapanga njiani, hatabstand machinga wanauza vitu
 
Inasikitisha sana...
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...

Tunaishia kusifia vya wenzetu, tukiletewa tunaharibu...



Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom