China, Qatar, Turkey, Iran na Urusi zatajwa kuwa washirika wakuu wa Taliban

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
6,661
2,000
China, Qatar na Uturuki , Iran na Urusi zatajwa kuwa washirika wakuu wa Taliban katika kuijenga Afghanistan
Msemaji wa kundi la Taliban amesema, China, Uturuki na Qatar ni washirika wakuu wa kundi hilo kwa ajili ya kuijenga upya Afghanistan.

Zabihullah Mujahid ameliambia gazeti la Italia la Repubblica kuwa "washirika wetu wakuu kwa ajili ya ukarabati na kuijenga upya Afghanistan ni China, Qatar na Uturuki na tunafanya jitihada kupitia China ili tuweze kuingia kwenye masoko ya dunia."

Mujahid ameongeza kuwa, China ndiye mshirika muhimu zaidi wa kibiashara na kiuchumi wa Taliban na kwamba iko tayari kuwekeza nchini Afghanistan.

Msemaji wa Taliban amebainisha kuwa, kwa mtazamo wa kundi hilo, mpango wa kuanzisha ukanda na barabara kuu ya China una umuhimu mkubwa. Ameongeza kuwa, Afghanistan ina utajiri mkubwa wa madini ya shaba na China inaweza kuyafufua machimbo ya madini hayo kwa kuipatia nchi hiyo teknolojia ya kisasa ya uchimbaji madini.

Viongozi wa kundi la Taliban
Alipoulizwa kuhusu Russia, Zabihullah Mujahid amesema, Russia ni nchi muhimu na kwamba Taliban ina uhusiano mzuri na nchi hiyo kama mshirika muhimu. Ameongeza kuwa uhusiano wa Taliban na Russia ni wa kisiasa na kiuchumi na kwamba Moscow inafanya juhudi za upatanishi wa kuleta suluhu kimataifa kwa manufaa ya kundi hilo.

Kuhusu uundaji wa serikali, Mujahid amesema, kwa kipindi kifupi, serikali itaundwa ikiwa na nusu ya mawaziri na akaongeza kuwa, kwa mujibu wa hukumu za Qur'ani na sharia za dini wanawake hawawezi kuwa mawaziri, lakini hakuna kizuizi chochote kwa wao kufanya kazi katika sekta za tiba na elimu
 

thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,525
2,000
Kwa China haishangazi, wanaplan kuendelea kutawala katika ya uuzaji WA material ya utengenezaji wa betri za lithium(betri za simu na magari ya umeme).

Afghanistan ina wingi WA hayo madini ya cobalt.

Taliban wasipokuwa makini na China, itakuwa kama Congo ambaye ameuza cobalt Kwa China.
70% ya lithium duniani ni kutoka Congo lakini China ndiye anayedhibiti uzalishaji WA lithium duniani kote.
 

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
6,661
2,000
Kwa China haishangazi, wanaplan kuendelea kutawala katika ya uuzaji WA material ya utengenezaji wa betri za lithium(betri za simu na magari ya umeme).

Afghanistan ina wingi WA hayo madini ya cobalt.

Taliban wasipokuwa makini na China, itakuwa kama Congo ambaye ameuza cobalt Kwa China.
70% ya lithium duniani ni kutoka Congo lakini China ndiye anayedhibiti uzalishaji WA lithium duniani kote.
Tunataka tuijenge nchi hile kwa rasilimali zilizopo, marekani amekaa karibu miaka 20 na bado kazidi kuichafua na kuu watu wengi, sasa ni muda wa kutengeneza fursa za maendeleo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom