China ndiyo nchi pekee duniani iliyofanikiwa kudhibiti gonjwa hili la COVID-19 kwa kiwango kikubwa, timu yetu ya Corona ifanye ziara China

Tupende tusipende ukweli unabaki pale pale kwamba China ndiyo nchi pekee duniani iliyofanikiwa kuudhibiti ugonjwa huu wa covid-19 kwa kiwango kikubwa. Nchi hii yenye population ya watu 1.4 billion ndiyo ambayo mlipuko wa gonjwa hili la COVID19 ulikoanzia. Kwa zaidi ya miezi 4 sasa mlipuko huo hauko tena China bali kuna sporadic cases za hapa na pale zisizozidi 10 kwa siku na hakuna vifo.

Tangia mlipuko wa gonjwa hili uanze hadi sasa waliougua ugonjwa huu huko China ni watu 90,483 tu ukilinganisha na nchi kama India yenye population inayolingana na China ambayo watu 14.8 million wameugua ugonjwa huu. Kwa sasa huko India licha ya chanjo za AstraZeneca kutengenezwa kwa wingi nchini India kasi ya maambukizi ya gonjwa hili yamepanda kwa kasi kubwa hadi kufikia watu 260,000 kwa siku.

Kenya yenye population ya watu million 54 ndiyo inayoongoza kwa idadi ya maambukizi kwenye nchi za Afrika zilizo kusini ya jangwa la sahara ukitoa Afrika kusini.Maambukizi yamefikia watu 151,287 na kasi ya maambukizi baada ya kuanza chanjo yamepanda hadi kufikia takribani elfu moja kwa siku. NB: Nigeria ambayo jumla ya maambukizi ni 164,207 kwa kuwa population yake ni watu 210 million inapitwa na Kenya.

Nchi za ulaya na amerika hawapendi kukubali mafanikio hayo makubwa ya China kudhibiti gonjwa hili. Watasema takwimu za China ni fake nk. Ukweli ni kwamba China wamefanikiwa na maisha yao yanaendelea kiuchumi kama kawaida. Timu yetu ya corona iliyoundwa na rais wetu kwa madhumuni ya kuishauri serikali, ingalifaa baadhi ya wajumbe wake wakafanya ziara nchini China kujifunza mbinu ambazo nchi hiyo imetumia kudhibiti gonjwa hili.
Wahuni hao, nilikuwepo Beijing mwaka Jana kabla ya rokudauni wanaficha ukweli sana
 
Wakajifunze kitu gani mbali na kufuata maelekezo ya WHO ya kudhibiti magonjwa ya milipuko ambayo wachina waliyafuata "to the letter" toka mwanzo!

Hapa Tanzania kuna mtaalam wa eneo hilo la magonjwa ya ilipuko asiyejua ni mambo gani yanayahitaji kufanyika?
Naona kama mtoa mada anajitekenya na kucheka. Kama anataka kucheka si acheke tu bila kujitekenya?
 
Amini. Wachina wako mbali. Hata hizo genetic codes za cov-2 wanazotumia wazungu kutengenezea chanjo za mRNA, hiyo decoding yake ilifanywa na Mchina. Angeweza kukaa nazo na kuwa siri yake, hivyo hawangaliweza kutengeneza hizo za teknolojia ya vinasaba. Lakini kwa ukarimu wake alizitoa aliitoa hiyo entire genetic code ya kirusi hicho kwenye maabara za biogenetics zote duniani na hivyo kuwezesha tafiti zaidi za kupambana na virusi hivi.

Bila shaka kuna makubwa zaidi anayoyajua (China) kuhusu virusi hivi ambavyo hakuzi share na wengine. Ndiyo maana chanjo zake wala hazitumii mRNA wala DNA adenovirus vectors.

Kama huamini kwamba China hakuna mlipuko wa covid 19 bali kuna endemic sporadic cases za hapo na pale, funga safari ukatalii China utajionea ninachokisema.
Eti China wakarimu! Unapenda sana kuwapigia promo hivi vijamaa..
Unethical masters of fake products..
 
Tupende tusipende ukweli unabaki pale pale kwamba China ndiyo nchi pekee duniani iliyofanikiwa kuudhibiti ugonjwa huu wa covid-19 kwa kiwango kikubwa. Nchi hii yenye population ya watu 1.4 billion ndiyo ambayo mlipuko wa gonjwa hili la COVID19 ulikoanzia. Kwa zaidi ya miezi 4 sasa mlipuko huo hauko tena China bali kuna sporadic cases za hapa na pale zisizozidi 10 kwa siku na hakuna vifo.

Tangia mlipuko wa gonjwa hili uanze hadi sasa waliougua ugonjwa huu huko China ni watu 90,483 tu ukilinganisha na nchi kama India yenye population inayolingana na China ambayo watu 14.8 million wameugua ugonjwa huu. Kwa sasa huko India licha ya chanjo za AstraZeneca kutengenezwa kwa wingi nchini India kasi ya maambukizi ya gonjwa hili yamepanda kwa kasi kubwa hadi kufikia watu 260,000 kwa siku.

Kenya yenye population ya watu million 54 ndiyo inayoongoza kwa idadi ya maambukizi kwenye nchi za Afrika zilizo kusini ya jangwa la sahara ukitoa Afrika kusini.Maambukizi yamefikia watu 151,287 na kasi ya maambukizi baada ya kuanza chanjo yamepanda hadi kufikia takribani elfu moja kwa siku. NB: Nigeria ambayo jumla ya maambukizi ni 164,207 kwa kuwa population yake ni watu 210 million inapitwa na Kenya.

Nchi za ulaya na amerika hawapendi kukubali mafanikio hayo makubwa ya China kudhibiti gonjwa hili. Watasema takwimu za China ni fake nk. Ukweli ni kwamba China wamefanikiwa na maisha yao yanaendelea kiuchumi kama kawaida. Timu yetu ya corona iliyoundwa na rais wetu kwa madhumuni ya kuishauri serikali, ingalifaa baadhi ya wajumbe wake wakafanya ziara nchini China kujifunza mbinu ambazo nchi hiyo imetumia kudhibiti gonjwa hili.
Ugojwa umetokea kwao na hakuna habari za wazi China. Mpaka leo chanjo yao haijulikani imetengenezwa vipi kwasababu hawajatoa ripoti ya majaribio. Msikimbilie kuamini nchi ambayo sio huru
 
Tupende tusipende ukweli unabaki pale pale kwamba China ndiyo nchi pekee duniani iliyofanikiwa kuudhibiti ugonjwa huu wa covid-19 kwa kiwango kikubwa. Nchi hii yenye population ya watu 1.4 billion ndiyo ambayo mlipuko wa gonjwa hili la COVID19 ulikoanzia. Kwa zaidi ya miezi 4 sasa mlipuko huo hauko tena China bali kuna sporadic cases za hapa na pale zisizozidi 10 kwa siku na hakuna vifo.

Tangia mlipuko wa gonjwa hili uanze hadi sasa waliougua ugonjwa huu huko China ni watu 90,483 tu ukilinganisha na nchi kama India yenye population inayolingana na China ambayo watu 14.8 million wameugua ugonjwa huu. Kwa sasa huko India licha ya chanjo za AstraZeneca kutengenezwa kwa wingi nchini India kasi ya maambukizi ya gonjwa hili yamepanda kwa kasi kubwa hadi kufikia watu 260,000 kwa siku.

Kenya yenye population ya watu million 54 ndiyo inayoongoza kwa idadi ya maambukizi kwenye nchi za Afrika zilizo kusini ya jangwa la sahara ukitoa Afrika kusini.Maambukizi yamefikia watu 151,287 na kasi ya maambukizi baada ya kuanza chanjo yamepanda hadi kufikia takribani elfu moja kwa siku. NB: Nigeria ambayo jumla ya maambukizi ni 164,207 kwa kuwa population yake ni watu 210 million inapitwa na Kenya.

Nchi za ulaya na amerika hawapendi kukubali mafanikio hayo makubwa ya China kudhibiti gonjwa hili. Watasema takwimu za China ni fake nk. Ukweli ni kwamba China wamefanikiwa na maisha yao yanaendelea kiuchumi kama kawaida. Timu yetu ya corona iliyoundwa na rais wetu kwa madhumuni ya kuishauri serikali, ingalifaa baadhi ya wajumbe wake wakafanya ziara nchini China kujifunza mbinu ambazo nchi hiyo imetumia kudhibiti gonjwa hili.
Ni wazi kwamba ugonjwa wa Covid-19 ulipolipuka, kila nchi imeupata si kutokana na idadi ya watu wake, bali kwa jinsi ugonjwa huu ulivyoweza kuenea kwa nchi husika hata katika nchi ambazo zilizingatia ushauri wa wataalamu wa afya. Kuna nchi hadi leo hii hazina takwimu za idadi ya watu walioupata, waliokufa, waliopona na kama bado ugonjwa katika nchi husika. North Korea: total population: 25.67 million (2019) World Bank, total cases (-), total recovered (-), active cases (-) ni nchi mojawapo katika nchi hizo. Kuna nchi pia ambazo zilipata wagonjwa na walipona wote na hakuna aliyepoteza maisha na pia hakuna maambukizi tena katika nchi hizo [kwa mujibu wa worldmoter.info April 20,2021 (18:15)]. Mfano: Micronesia (population 115,985): total cases (1), total recovered (1), active cases (0); Marshall Islands: total population (59,509), total cases 4, total recovered (4), active cases (0); Greenland: population (56,849); total cases 31, total recovered 31, active cases (0). Sasa je, hoja yako umeijenga katika nini ili useme China ndiyo nchi pekee iliyofanikiwa kupambana na Covid-19 na wataalamu wetu waende huko?
 
Wahuni hao, nilikuwepo Beijing mwaka Jana kabla ya rokudauni wanaficha ukweli sana
Mimi nilikuwako mwaka huu mwezi jana, hali ni shwari sana na shughuli za kiuchumi zinaendelea kwa kasi kubwa. China sasa hivi ni an economic super power duniani. Imeipita kwa mbali USA. Believe me my friend.
 
Wachina wako serious sana na mambo serious. Hata hivyo mbinu zilizotumia kupambana na korona china haziwezi kufanya kazi kabisa afrika kulingana na utofauti wa mazingira, uchumi, teknolojia na sana ya watu
 
Kuna nchi hadi leo hii hazina takwimu za idadi ya watu walioupata, waliokufa, waliopona na kama bado ugonjwa katika nchi husika.
Hakuna nchi ambayo hospitali na vituo tiba vyake huwa hazikusanyi takwimu za magonjwa yake mbali mbali. Iwe ni malaria, ukimwi, ebola, kipindupindu, zika, uti nk. Takwimu hizi hupelekwa kwenye mamlaka ya nchi husika kila siku au kila mwezi kutegemea na matakwa ya mamlaka ya nchi (wizara ya afya). Si lazima mamlaka ya nchi kupeleke takwimu hizo WHO kwenye worldometer.

Takwimu wanazozihitaji WHO wala siyo hizo za hospitali ulizozitaja. Wao wanataka kila mtu apimwe virusi vya corona. Wanaposema New cases hawamaanishi ni wagonjwa wa corona. Wengi wa hao new cases ni si wagonjwa bali ni wale waliopatikana kuwa na virusi hivyo kwenye mkakati wao wa testing, testing, testing ambao sisi tumeuona hauna faida yo yote ikizingatiwa kuwa kila kipimo cha PCR ni Sh 120,000/. Hivyo biashara hiyo hatuitaki na wala haisaidii cho chote kudhibiti gonjwa hili. Hata Trump aliwatupilia mbali hao WHO. Na nchi zote zinazotoa takwimu huko ni under reporting kutegemea na wanasiasa wanachokitaka. Sasa hivi UK kupalilia chanjo yao ya AstraZeneca takwimu zao zinaonesha kumaliza mlipuko huo wa covid-19. Ni ulaghai mtupu.
 
Nchi pekee duniani iliyofanikiwa kutegua kitendawili cha corona ni Tanzania. Mataifa mengine yanapaswa kuja kujifunza kwetu!! Leo hii hakuna mtanzania mwenye hofu na corona. Tumamshukuru sana Mungu kwa kuiponya nchi yetu na corona. Tuendelee kukiri hivyo na kuamini hivyo na ndivyo ilivyo. Tulimwomba Mungu na Mungu alituponya. Kama kuna mtu anadhani Mungu hakutuponya
namshauri aende mexico, India, marekani aone nchi zenye corona zinavyofanana!
Tumshukuru sana Mungu na tumshukuru pia Raid Magufuli (marehemu) kwa kutuongoza vizuri na kutuongoza kumtànguliza Mungu mbele ya mambo yote katika vita vya corona na ushindi tumeuona site.
Rais Magufuli alimwamini Mungu kuhusu kutuponya watanzania na corona hadi pumzi yake ya mwisho!
Hakuna atakayekuelewa humu. Kuanzia mitaani mpaka kwenye vyombo vya habari, hakuna tena habari za korona wala vitisho. Vile vifo vya viongozi vimeshakidhi lengo lake, nadhani wameridhika sasa.

Mama ametoa uhuru, nilitegemea kwa kipindi cha wiki moja tuijue hali halisi ya ugonjwa huo unaosemekana taarifa zake zimefichwa, lakini mwezi umeisha sasa, hakuna hizo takwimu.

Hatukuwa na dawa, tahadhari wala lockdown, waweke taarifa zilizo zilizofichwa ili tuone ukweli ulikuaje basi!

Wenzetu walisumbuliwa sana na wanaendelea kusumbuliwa na mafua ya msimu, wanajipiga FLU JAB kila msimu ila hawana chanjo bado ya kukomesha mafua hayo.

Naona maisha yanaenda kama kawaida mtaani, kazi inaendelea, kama kuna wa kumshukuru au kukishukuru, tufanye hivyo kwa moyo mkunjufu tu.
 
Hakika hapa China imeuonyesha ulimwengu ni jinsi gani walivyotofauti sana na mataifa mengine; hadi wakubwa kuanza kujihisi kwamba kwa 'discipline' hii, hata kama ni ya kikandamizaji, hata vita ikija Mchina atawatoa kamasi (Ukiondoa ma-nuclear).

Mchina anajua kila alipo raia wake; mithili ya nyumba kumi kumi zetu, ila wao hawacheki na mtu.

Kukitokea sehemu COVID-19 inaibuka, sehemu hiyo inadhibitiwa hapo hapo, hakuna wa kuingia wala kutoka, na wote waliokwishafika hapo mahala wiki kadhaa za nyuma watatafutwa popote walipo na kupigwa karantini.

Sasa nikuulize wewe, muundo huo na 'discipline hiyo tunavyo hapa kwetu? Labda Magufuli pekee ndiye angeweza kama angeamini uwepo wa corona, maanake yeye alikuwa hasiti kuyatumia mapolisi na mabunduki yao.

Hata hivyo mazingira yetu yangefanya kazi kuwa ngumu sana. Watu wangekula nini?

Hata hivyo, mkazo wa kufanya baadhi ya mambo kwa ufanisi ingesaidia; kama kuwafanya watu wawe na ufahamu na kuchukua tahadhari kwa kufanya yanayowezekana kama kutumia barakoa, n.k.

Kumbuka Trump alivyochezacheza na corona, na mijamaa yake mingine ikitoa mabunduki mitaani kutishia watawala wa majimboni kwao kama watathubutu kuweka 'lockdown'. Katika hali hiyo utaidhibiti vipi corona!
Mchina mwepesi sana bado ndio maana hata yeye hajiamini kwenye vita na Taiwan tu
 
Hakuna nchi ambayo hospitali na vituo tiba vyake huwa hazikusanyi takwimu za magonjwa yake mbali mbali. Iwe ni malaria, ukimwi, ebola, kipindupindu, zika, uti nk. Takwimu hizi hupelekwa kwenye mamlaka ya nchi husika kila siku au kila mwezi kutegemea na matakwa ya mamlaka ya nchi (wizara ya afya). Si lazima mamlaka ya nchi kupeleke takwimu hizo WHO kwenye worldometer.

Takwimu wanazozihitaji WHO wala siyo hizo za hospitali ulizozitaja. Wao wanataka kila mtu apimwe virusi vya corona. Wanaposema New cases hawamaanishi ni wagonjwa wa corona. Wengi wa hao new cases ni si wagonjwa bali ni wale waliopatikana kuwa na virusi hivyo kwenye mkakati wao wa testing, testing, testing ambao sisi tumeuona hauna faida yo yote ikizingatiwa kuwa kila kipimo cha PCR ni Sh 120,000/. Hivyo biashara hiyo hatuitaki na wala haisaidii cho chote kudhibiti gonjwa hili. Hata Trump aliwatupilia mbali hao WHO. Na nchi zote zinazotoa takwimu huko ni under reporting kutegemea na wanasiasa wanachokitaka. Sasa hivi UK kupalilia chanjo yao ya AstraZeneca takwimu zao zinaonesha kumaliza mlipuko huo wa covid-19. Ni ulaghai mtupu.
Ukiwa mwanachama wa WHO na hakuna taarifa zako na hakuna kupima mtu wala maiti. Takwimu zako hizo za vipimo unazipataje na unapeleka wapi?
 
Mimi nilikuwako mwaka huu mwezi jana, hali ni shwari sana na shughuli za kiuchumi zinaendelea kwa kasi kubwa. China sasa hivi ni an economic super power duniani. Imeipita kwa mbali USA. Believe me my friend.
Mbona na Tanzania shughuli zinaendelea kama kawaida hakuna kilichobadilika sasa tukajifunze nini huko China?
 
Israel nayo ni Kati ya nchi zilizodhibiti COVID kwa kiasi kikubwa. More than 70% ya population yao iko vaccinated enough to induce herd immunity. Maisha yamerudi kama kawaida, ruksa kutovaa mask sehemu za wazi.
 
Kwa hiyo wewe unadhani "timu yetu ya mapambano dhidi ya corona kutembelea China kujifunza mbinu ambazo China imetumia kudhibiti ugonjwa huo." ndiyo suluhisho la sisi kudhibiti corona?

WHO walikuwa huko China kwa muda gani hivi karibuni, wakitafuta chanzo cha corona? Wao hawana uwezo wa kujifunza na kuelimisha dunia wafuate wanayofanya wachina?

Au unadhani sisi ndio taifa pekee tunaoaminiwa na wachina dunia hii ya kwamba wakiwa na siri, basi nasi tutafaidika na siri hiyo?

Sikiliza, wewe umejitambulisha hapa, na unajiita Dr; na bado huwezi kujua kwa nini nchi za Magharibi wameshindwa kudhibiti gonjwa hili, na wala huoni tofauti waliyofanya wachina na hao wa Magharibi katika njia zao za kuzuia na kujikinga?

Tumia upeo wako, wa elimu yako hata kama wewe sio mtaalam katika haya magonjwa ya milipuko kutofautisha wanachofanya China na wanachofanya nchi za Magharibi na wengine.
Inasikitisha sana kwamba haujui hata hiyo WHO ni kitu / chombo gani? Haujui hata kazi na ya WHO. Haujui hata aina ya watalaamu wa afya walioko WHO. Kwa akili yako finyu unafikiri WHO ndiko walioko madaktari mabingwa wa kila fani ya medicine, pharmacy, medical laboratory technology, virology, surgery, immunology, bacteriology, pathology and so forth.

Kwa taarifa yako hao mabingwa wazamifu wako kwenye mahospitali, specialised research institutes na vyuo vikuu. Huko ndiko kwenye utalaamu wa afya. WHO is just a public health global co-cordinating agency of the United Nations. Watalamu walioko huko ni wa public health (MpH) kama akina Kingwala. Wewe kama ni mtalaamu ya afya utaelewa kazi na aina ya utalaamu wa MPH (Master of Public Health). Wana office yao hapo Dar es Salaam ikiongozwa na country representative. Unaweza kuwatembelea kujifunza majukumu yao na utalaamu walio nao kuhusu magonjwa.

WHO hawana power ya kulazimisha nchi yo yote duniani kufanya wanachotaka kuhusiana na masuala ya afya. Hata maazimio ya UN lazima yakunalike (rectified) na nchi wanachama ili yatekelezwe. Hayalazimishwi. Nchi ziko huru. WHO ya sasa hasa kwenye kushughulika na suala hili la covid -19 imekuwa ikikeuka mipaka yake. Ndiyo maana aliyekuwa rais wa USA, Mh. Trump aliwatimua na kuwanyima hela ya uendeshaji (Over 70% ya gharama za uendeshaji wa WHO unatolewa na USA government). Hata rais wa Rwanda Mh. Kagame aliwatimua WHO nchini kwake wakafungasha vilago. Wakaenda China kufanya kazi ya u spy, eti kutafuta chanzo cha covid-19. Oh my God, hii si kazi yao na hawana utalaamu huo. Walichokipata huko hawatakisahau. Kwanza China ina veto power kwenye muajiri wao the United Nations.

Na sisi ni nchi huru. Hatuwezi kufanya copy & paste ya miongozo ya WHO. Sweden na wengine hawakufanya hivyo kuhusu miongozo hiyo ya WHO ambayo hadi sasa haijafanikiwa kwenye nyingi za nchi zilizotekeleza miongozo hiyo by 100%.
 
Israel nayo ni Kati ya nchi zilizodhibiti COVID kwa kiasi kikubwa. More than 70% ya population yao iko vaccinated enough to induce herd immunity. Maisha yamerudi kama kawaida, ruksa kutovaa mask sehemu za wazi.
Herd immunity unaweza kuipata passively kwa chanjo au actively kwa live viruses kama tulivyoipata sisi free of charge with no side effects huku kazi ikiendelea.
 
Back
Top Bottom