China na Tanzania zasaini mpango mpya wa utekelezaji wa makubaliano ya kiutamaduni

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,008
1,032
Serikali za China na Tanzania jana Alhamis zilisaini mpango mpya wa 2022-2025 wa utekelezaji wa makubaliano ya kiutamaduni unaolenga kuimarisha ushirikiano wa pande mbili kwenye nyanja mbalimbali.

Kwa mujibu wa ubalozi wa China nchini Tanzania, mpango huo uliosainiwa jijini Dar es Salaam na balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjiang na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa ambao unaangazia maeneo ya utamaduni, Sanaa, utalii, uandishi wa habari, michezo na elimu, unadhamiria kuimarisha kwa kina urafiki wa jadi kati ya nchi mbili. Mpango huo pia unahamasisha ushiriki mpana katika kukuza utalii na kutumia bidhaa za utamaduni na utalii kwa pamoja kati ya pande mbili.

Akiongea baada ya kusainiwa, Mchengerwa amesema ushirikiano wa kiutamaduni kati ya China na Tanzania unailetea tija nyingi Tanzania. Naye balozi Chen amesema nchi hizi mbili zinafurahia urafiki mkubwa wa jadi na zimekuwa zikishirikiana kwa karibu kwenye maeneo ya utamaduni, Sanaa, redio, filamu, televisheni, elimu na sayansi na teknolojia.

1655973184654.png

Semina ya makada vijana ya Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere yafunguliwa

Semina ya mwaka 2022 ya makada vijana wa Vyama 6 vya Ukombozi wa Kusini mwa Afrika imefunguliwa katika Chuo cha Mwalimu Julius Nyerere.
Wanafunzi 120 kutoka vyama hivyo wamekusanyika katika chuo hicho ili kujadili mada ya maendeleo katika zama mpya. Semina hiyo ina maana muhimu kwa kuimarisha mawasiliano kuhusu utawala wa nchi kati ya CPC na vyama hivyo sita, na kuvisaidia vyama hivyo kufundisha makada vijana.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Kamati Kuu ya CPC Song Tao amesema Hii ni semina ya kwanza iliyoandaliwa na CPC kwa vyama hivyo sita kwenye Chuo hicho, na pia ni hatua halisi ya kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi hao. Kutokana na mkakati wa kurithisha majukumu ya kuendeleza nchi zetu, makada vijana hodari wamechaguliwa kuwa kikundi cha kwanza cha wanafunzi wa semina hiyo, kwa kulenga kuwafundisha makada watakaobeba majukumu makubwa.
Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi cha Tanzania CCM Daniel Chongolo amesema, semina hiyo unayowahusisha makada vijana, yatajikita katika kufundisha masuala ya uongozi yanayolenga kusaidia vyama hivyo tawala katika nchi yao, kuendana na mazingira ya wakati hasa katika kubaini na kutambua mwelekeo mzuri wa kufanikisha na kusimamia upatikanaji wa maendeleo hasa katika kukabiliana na changamoto kinzani za ndani na nje, kwa maslahi ya wananchi katika nchi hizo.
Bw. Chongolo ameishukuru China kwa kuunga mkono ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Julius Nyerere na maandalizi ya semina hiyo.
 
Back
Top Bottom