China na Russia kamwe hawawezi kutumia hiyo chanjo ya mRNA ya kampuni ya Pfizer (Billgate) na BioNTech (Mjerumani): Kwa nini Afrika tulazimishwe?

Oxlade-Chamberlain

JF-Expert Member
May 26, 2009
8,578
2,000
Hivi sisi wa Africa hatuna wana sayansi wa kufanya research na kututengenezea chanjo bora? Au wanafundishana wenyewe tu wazungu na kutengeza chanjo na madawa uku wanatuachia sayansi ya kulalamika tu.

Kila siku tunalilia hatukaki vipimo, hatutaki chanjo wanataka kutuua, wana sayansi wetu wako wapi watutengengezee dawa na chanjo bora.

Vyuo vyetu vinafundisha nini? Tofauti nini na wanacho fundishwa hawa wenzetu ambao kutwa wanatungenezea sisi dawa.

Umuhimu wa Afrika kwenye sayansi nini zaidi ya kuwa kifaa cha majaribio?
 

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,473
2,000
kuna tofauti kubwa kati ya kuwa ground zero na kuwa na dawa.
mfano. ground zero ya ebola virus ni congo river. congo ni magwiji wa kutengeneza chanjo ya ebola nope?
sars outbreak ilitokea Nov 2002 to may 19 2004.
location: foshan,china.

sars cov-1 simply ilitoweka na waliweza kwa kuwela karantini na isolation mapema. so ugonjwa haukuvuka pande zingine za dunia.

kwanza sars cov-2 ilianza 2019 wuhan china.

unasema china ndio walikuwa wakwanza kutengeneza chanjooo ? nope

30 dec 2020 china ilitangaza jaribia la tatu limeonyesha 79% ya mafanikio.

in 13 jan 2021 brazil ilisitisha matumizi ya chanjo ya china baada ya kugundua kuwa ina 50% capability na si 79% kama china ilivyotangaza before.


so hao magwiji wa corona virus wanashindwaje kuwa na chanjo isiyo aminika?
why hawakutengeneza chanjo effective 100%?

kisa ugonjwa umeanzia kwako.. haimaanishi ww ndio gwiji la madawa.
 

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,473
2,000
Hakuna ugonjwa mbaya kama hofu watu hivi sasa tumejazwa hofu kubwa, tena tunaambiwa hii covid ya sasa ni hatari kuliko ile ya kwanza, cha ajabu wao bado ligi na michezo inaendelea kule kwao. Hapa ndio utagundua kwa nini walitaka idadi ya wagonjwa iwe inatangazwa kila siku tena iwe inatajwa kila siku badala ya kurecord kimya kimya kama inavyofanyika kwa magonjwa mengine, tena idadi ya wagonjwa iwe inaongezeka badala ya kushuka, na pia utashanga kwa nini mke wa Bilgate alitabiri Africa tutakufa kama kuku na pia utajiuliza ni kwa nini Biligate amekuwa akizungumzia utishio wa covid utadhani yeye ni waziri wa afya.

Mimi napongeza msimamo wa Mh. Rais asikubali kufuata mkumbo, wananchi tunapaswa kuchukua tahadhari na kuendelea na shughuli zetu kama kawaida. Ni ajabu kuona nchi za Africa zimeshindwa kuthibiti vifo vinavyotokana na malaria, njaa, mafuriko, na ajali za barabarani ambavyo ndio vinagharimu maisha ya raia kwa wingi eti leo wanatumia njia za matajiri wa magharibi kudhibiti na kujikinga na covid.

Corona itakuja na mengi, binafsi naiona kama hii issue imekaa kibiashara zaidi, sikatai kwamba hakuna coron, corona ila kwa jinsi inavyopaishwa wengi warakufa na kwa hofu. Embu tujiulize, mbona mafua yamekuwa tishio kwa wazungu miaka nenda rudi mbona hakuna chanjo yake? Sisi wa Afrika tukiugua mafua ndani ya siku saba yanaisha yenyewe. Kumbe kuna uwezekano wazungu wangeamua kututia hofu kwenye mafua basi na sisi tungeanza kufa kwa hofu ya mafua then tungeambiwa tumekufa kwa mafua.

Ifike mahala viongozi wetu wajitambue, kwa mujibu wa maandiko mamlaka yeyote yametoka kwa Mungu, tuliona awamu ya kwanza Mh. Rais alikataa lockdown dunia ikamshanga lakini baadae karibu dunia nzima ilifuata njia zake lakini sijaona hao WHO wakimpa tuzo. Naamini na kwenye hii awamu ya pili ataibuka kidedea tena.
 

Shift

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
1,074
2,000
Hata mimi niko Rwanda acha ujinga. Chanjo za covid zinazoletwa Africa kwa mpango wa WHO unaoitwa COVAX ni za kampuni ya AstraZeneca zilizotengenezwa kutokana na attenuated live chimpanzee adenovirus kwa utalaam wa Oxford University ya UK. Hizi zinatumia jokofu la kawaida kama chanjo zingine na zinaweza kutunzwa kwa miezi 6 kwenye hizo cold chain zetu za chanjo. Hizi ndizo wanatumia South Africa, India, Ulaya na kwingineko duniani ukiacha USA, China na Russia. Rwanda hamuna uwezo wa kuzitunza chanjo hizo za USA kwenye hizo -94 degrees F hadi kwa mchanjwaji huko vijijini. Achilia mbali hiyo cost ya USD 33 per dose ikilinganishwa na USD 4 per dose ya AstraZeneca. Achilia mbali uwezo wa wanasayansi wenu kutokuwa nayo ku verify hizo genetical instructions zilizobebwa na hao messenger RNA!

Mimi ni scientist mbobezi, ninajaribu kuwaelimisha kuhusu ugonjwa huu, wewe unaleta ujinga wako wakati hujui cho chote kuhusu sayansi hii. Jukwaa la Jf pia ni la kuelimisha jamii ya watanzania. Wewe wa Rwanda usitake kutuvuruga. Au kuna waliokutuma? Nyie huko endeleeni kuwekwa lockdown na kuchanjwa madawa msiyoyajua na kuvalishwa barakoa zilizobebeshwa corona na hao mabepari ili muweze kukopeshwa tu USD. Umeniudhi sana, ninamwomba rafiki wa taifa letu Mh. Paul Kagame anisamehe kwa kusema haya niliyoyasema. Na uwezekano ni mkubwa kuwa hili linalojiita Shift ni jitu la hapa hapa ufipa linalotafuta kick ya kisiasa kwenye kila jambo.
Hakuna scientists kilaza ksma wewe, gundua sasa ya kwako
 

reg edit

JF-Expert Member
Oct 4, 2012
378
500
Ni wakati sahihi kwa serikali yetu kuanzisha kitengo kikubwa cha biological warfare ndani ya JWTZ military intelligence unit.

Ni wakati sahihi wa kusomesha wataalamu wa hali ya juu wa microbiology, biotechnology, synthetic biology na vitu kama hivyo.
Huko tuendako sio kuzuri.

Tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye sayansi kwa ajili ya usalama wetu siku za usoni.

La mgambo hili!
HII NDIO POINT YA MSINGI KABISA, MNAOMSHAURI MH. RAISI MFIKISHIENI HUU UJUMBE. TUMECHELEWA LAKINI SIO MBAYA. HUKO TUENDAPO INAONEKANA KUTAKUA KUBAYA ZAIDI.

ZIJENGWE MAABARA ZA KISASA KWA AJILI YA HAYA MAMBO.
 

Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
2,547
2,000
Soma vizuri nilichoandika kuhusu masharti ya uvaaji barakoa na PPEs iliziweze kukukinga angalao kwa hiyo asilimia niliyoitaja. Usipotimiza hayo masharti hizo barakoa na PPEs zinageuka kuwa ni chanzo (reserveur) ya maambukizi na usambaaji wa hivi virusi. Unapaswa kuzibadili (dispose) kila baada ya saa moja. Maana yake ni shillingi zisizopungua elfu tatu kila saa. Nani mwenye uwezo wa kufanya hivyo hapa Tanzania? Halafu barakoa ukishaivaa haitakiwi kuwa unaikamata kamata na ndiyo maana watoto wadogo hawapaswi kuvyalishwa barakoa kwani zitawaambukiza corona badala ya kuwakinga. Halafu mijitu kama nyie utakuta limevaa barakoa lakini pua yake iko nje. Hii ni sawa na kuvaa chupi lakini nyeti zako ziko nje ya chupi! Unategemea hiyo chupi imesitiri kitu gani hapo kama nyeti zimeachwa nje?
Du eti gharama ni kubwa. Kwa hiyo gharama ya maisha na gharama ya 3000 kwa siku ipi kubwa?

Kukazwa hospitali siku moja sio Chini ya 30,000 hapo ni kitanda tu ukiweka gharama matibabu ventilator au oxygen etc. Maana yake kuvaa barakoa ni rahisi kuliko gharama ya matibabu plus mateso ya siku za kuugua na hatimae hata kufa.

Mtu anaweza kushona hata barakoa tano zikamsaidia kwa asilimia Fulani kuliko Hali ilivyo.

Kuhusu wahudumu wa afya eti ni gharama kubwa laki tano. Si serikali ilipewa msaada zaidi ya 200m USD na wanasema wanazielekeza kuwakinga first line soldiers. Sasa eti zimekuwa ghali, sitabishana Tena wajinga kilichobakia ni kukaa kimya ili umuona baba na mamako wakifa, wanao na mkeo na wewe uwe wa mwisho ili upate uchungu kabla na wewe kupata Hilo pigo
 

Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
13,989
2,000
Hivi sisi wa Africa hatuna wana sayansi wa kufanya research na kututengenezea chanjo bora? Au wanafundishana wenyewe tu wazungu na kutengeza chanjo na madawa uku wanatuachia sayansi ya kulalamika tu.

Kila siku tunalilia hatukaki vipimo, hatutaki chanjo wanataka kutuua, wana sayansi wetu wako wapi watutengengezee dawa na chanjo bora.

Vyuo vyetu vinafundisha nini? Tofauti nini na wanacho fundishwa hawa wenzetu ambao kutwa wanatungenezea sisi dawa.

Umuhimu wa Afrika kwenye sayansi nini zaidi ya kuwa kifaa cha majaribio?
siasa nyingi sana afrika. walichotuzid wenzetu wao wamewekeza kwenye science. kuna funds za kutosha ndio maana chanjo zinapatikana.

afrika ni reverse.. sisi tunawekeza kwenye siasa. ndio maana hata wasomi wetu wanakimbilia siasa.
 

The 13

JF-Expert Member
Oct 14, 2018
2,000
2,000
Ni wakati sahihi kwa serikali yetu kuanzisha kitengo kikubwa cha biological warfare ndani ya JWTZ military intelligence unit.

Ni wakati sahihi wa kusomesha wataalamu wa hali ya juu wa microbiology, biotechnology, synthetic biology na vitu kama hivyo.
Huko tuendako sio kuzuri.

Tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye sayansi kwa ajili ya usalama wetu siku za usoni.

La mgambo hili!
Wanajeshi wetu wanonekana kama wavietinam sembuse hayo madubwasha mkuu.
 

Young fadson

Senior Member
Nov 6, 2017
123
225
Umeongea point hakuna watu wajinga Kama waafrika walio wengi akiwemo mtoa mada, anadhani hao warusi na wachina ni watu wazuri sana kumbe ni walele kwanza ni wabaguzi wa wazi wazi ukienda nchi zao

Ukiangalia USAID hela anayochangia kwenye sekta ya afya ni kubwa lakin leo tunawaona ni wabaya
Issue sio kuchangia, hapa issue ni kwa sababu gani amechangia
 

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,159
2,000
Hivi sisi wa Africa hatuna wana sayansi wa kufanya research na kututengenezea chanjo bora? Au wanafundishana wenyewe tu wazungu na kutengeza chanjo na madawa uku wanatuachia sayansi ya kulalamika tu.

Kila siku tunalilia hatukaki vipimo, hatutaki chanjo wanataka kutuua, wana sayansi wetu wako wapi watutengengezee dawa na chanjo bora.

Vyuo vyetu vinafundisha nini? Tofauti nini na wanacho fundishwa hawa wenzetu ambao kutwa wanatungenezea sisi dawa.

Umuhimu wa Afrika kwenye sayansi nini zaidi ya kuwa kifaa cha majaribio?
Hawa wazungu wamehakikisha wameua elimu yetu kwa kuifanya digital only. Yaani hatufundishi tena ile original. Utakuta medical students wetu wanafanya human anatomy dissection kwenye computer yenye digital cadaver. Laboratory technician anafundishwa kutumia tu kutumia computerized machines zinazopima vipimo vyote. Kazi yake ni ku press tu a button kwenye hiyo mashine na kupata results ya hiko kipimo. Hafundishwi kufanya Gimsa stain manually kwani inafanywa na digital machine iliyokuwa fed na gimsa application na mzungu. Utakuta daktari hawezi kufanya diagnosis bila CT scan au MRI machine. Hafundishwi tena manual science ya kuweza kufanya diagnosis bila hiyo mashine ya CT scan. Yaani yeye anaiamini hiyo CT scan kuliko brain yake kwani brain yake haikufundishwa hivyo. Kwa hiyo yeye hawezi kutengeneza digita applications za hiyo CT scan kuiboresha na hivyo anavyotaka CT scan hiyo imfanyie.

Wenzetu wazungu wanakazana na hiyo original education ya manual na kui advance. Digital applications wanazitengeneza tu kurahisisha kazi za manual walizozigundua. Sasa sisi tunaona utumiaji wa hizo automated applications kuwa ndiyo elimu. Kwa hiyo mtu hata wa darasa la saba tu unaweza kumfundisha kufanya vipimo vyote anavyofanya laboratory technician wetu ndani ya mwezi mmoja tu na hawatakuwa na tofauti ye yote ya maana.
 

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,469
2,000
Wewe ndio umeleta hii hoja mfu ambayo haipo. Bill Gates anamiliki makampuni gani ya pharmaceuticals na ana hisa asilimia ngapi?

Ujuaji wa kipuuzi utakuja kuwafanya mfe kwa stress. Pfizer, Moderna, AstraZeneca, Johnson & Johnson na BionTech wapi ambako Gates kahusika. Watu kama nyinyi huwa mnaishi kwa shemeji hamna hata kazi mnajikuta genius kumbe vilaza tu.
Mtu ni philanthropist kwenye sekta ya afya, tiyari mnamuita mtengeneza madawa. Mtu akigawa magodoro shuleni mtasema ana kiwanda cha magodoro?
Pole! Unavyolalama ni kama huyu jamaa ni nabii wa magonjwa. Is he one of your brothers? Kama hujui kinachoendelea duniani, stop that unnecessary agape!
 

Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
1,426
2,000
Hiyo tunayoiita chanjo inayotengenezwa na kampuni ya Pfizer ikishirikiana na kampuni ya BioNTech ya ujerumani si sawa na chanjo zinazojulikana ambazo hutumia virusi vya ugonjwa huo huo vilivyopunguzwa makali (attenuated live viruses). Hawa wanatumia genetically engineered manufactured synthetics za genetitically coded mRNA to instruct our DNA in the genes of our cells (nucleas chromosomes) to produce certain proteins which are thought to be protective or curative of certain diseases including cancer diseases.

Utafiti wa kutumia synthetic mRNA kutibu au kukinga magonjwa ya cancer, rabies, zika etc ni wa siku nyingi. Hata hivyo dawa au chanjo za magonjwa hayo zinazotumia genetic mRNA hazikuweza kupata approval ya kutumika kwa binadamu kutoka FDA. Kwa sababu ya taharuki, hofu na wasiwasi wa janga hili la covid - 19 FDA imezipa emergency approval dawa/ chanjo hizo za mRNA. Hazijapitia hatua zote za kimchakato za usalama kama inavyotakiwa kisayansi. Inaelekea waafrika baada ya kujazwa hofu na pesa kupenyezwa walitumika kama guine pigs katika utafiti wa usalama na uwezo wa dawa hizi. Utafiti huo haukuoneshwa kwani ulikuwa unethical.

Chanjo za covid 19 zinazotengenezwa China na Urusi ndizo chanjo halisi zinazotumia live attenuated sars- cov-2, kirusi kinachosababisha covid-19. Urusi na Uchina kamwe haziwezi kutumia hizo chanjo za mRNA kutoka Pfizer/ BioNTech. Ni kipi cha ajabu Tanzania chini ya rais mwanasayansi wa level ya PhD kuzikataa au kuzitilia mashaka hizo chanjo zao za mRNA. Kama tutaamua kuchanja tutatumia chanjo toka China au Russia kwani hizo hazichezi na DNA zetu. Chanjo zinazotumia live attenuated viruses ni rahisi kuzi verify. Hizo za mRNA huwezi ukatambua code (ujumbe) zilizobebeshwa hizo RNA.

Halafu ukweli ni kuwa Afrika ugonjwa huu si tishio hata kidogo. Takwimu ambazo tumelazimishwa na WHO kwamba hata wale ambao hawana ugonjwa lakini wame test positive kwa baadhi ya antigens za cov-2 tuwahesabu kama ni wagonjwa (covid-19), ni kitu ambacho si sahihi na hakikubaliki kisayansi. Unachokonolewa pua kutafuta kama una hizo antigen wakati antigen hizi ungaliweza kuzipata kwenye kinyesi au kwa kuchokonolewa kwenye mkundu. China sasa hivi wanatumia kipimo cha kinyesi au rectal swab which is easier and more convinient. Halafu WHO inatulazimisha tupimane sana na vipimo hatupewi bure, ni za ghari takribani Tsh laki moja kila kipimo - wanatukopesha.

Takwimu wanazozitaka siyo za prevalence wala incidence ya ugonjwa au wa virusi hao wa cov-2 kiepidemolojia nakisayansi. Ndiyo maana Trump aliiondoa USA kwenye shirika hili la WHO kwa kuvurunda kwake kuhusu suala hili. Kama ni kutaka kujua prevalence ya virusi hivi ni vyema a scientific prevalance survey of an unbiased sample population ikafanyika. Si hizi takwimu za kujumlisha contact tracing, patients and carriers.Virusi hivi vimekuwapo duniani tangia zaidi ya miaka million 50 iliyopita. Binadamu amekuwapo hapa duniani kwa miaka million tano tu. Dunia imekuwapo kwa miaka billion tano (after the Big - Bang)!

Hata kwa hizo takwimu tulizolazimishwa kukusanya bado Afrika corona si tatizo la kutufanya tutaharuki. Kwa mfano Kenya ambayo population yake ni 55 million kwa kipindi cha mwaka mmoja ni watu elfu 90 tu ndiyo wame test kuwa na antigen za corona kwenye pua zao, yaani elfu nane tu kwa mwezi! Na wanaofikiriwa kufa kwa corona (kama primary cause of death) hawazidi elfu moja kwa mwaka. Na wengi wa hawa waliokufa walikuwa na magonjwa yao mengine kama kisukari, pressure, congestive cardiac failure, renal failure, cor pulmonary, bronchoathma (pumu) etc. Wala corona haikuwa the primary cause of death. Kwa sababu ya woga na taharuki iliyojengwa kuhusu corona wagonjwa wote hawa wenye changamoto la upumuaji (dypsnoea and tachpnoea) wamekuwa wakikimbiwa au kuogopwa na wauguzi/ madaktari na kupelekea wasipate huduma sahihi ya magonjwa yao na kusababisha vifo vyao. Tumeshuhudia hadi migomo ya wauuguzi, madaktari na watoa huduma za afya wengine.

Taharuki hii kwa nchi za Afrika ndiyo wazungu wanataka ili wapate watu wa kujaribia dawa au chanjo za ugonjwa huu na pia kupiga pesa. JPM kawagusa penyewe. Ndiyo maana hawakuchelewa kuwawaya - mara oh jiandae kupokea chanjo za msaada (lakini mkopo) za mRNA etc.

Inasikitisha sana Kanisa katoliki kupitia Padre wake machachari wa Baraza la Maaskofu Tanzania, anayeitwa Kitima, bila ushahidi wa kisayansi wala ridhaa ya malaka husika, ghafla kwa taharuki limeamua kuvunja utulivu wa nchi yetu uliokuwapo dhidi ya virusi hivi. Nchi ilikuwa imetulia chini ya ulinzi wa Mungu kwa kutambua kuwa ugonjwa huu hauna tiba wala kinga na kwamba kinachoua kwenye ugonjwa huu hasa ni ile hofu na taharuki na si ukali wa virusi hivi. Hizo barakola, social distancing na lockdown hazisaidii cho chote (useless) na hapa kwetu zina madhara zadi (dangerous) au haviwezekani. Wazungu wamefanya hivyo hazikusaidia chochote. Sweden hawakufanya hivyo kama sisi and are much better! Waafrika waliouawa kwa risasi kwa sababu ya kukiuka masharti ya lockdown ni wengi kuliko waliouawa na corona.

Hata hizo barakola za grade ya juu zinazouzwa Sh elfu kumi kwa moja ambazo zinapaswa kubadilishwa kila baada ya nusu sasa, bado uwezo wake wa kuzuia virusi hivi ni 60% tu. Hivi vya nguo vikibadilishwa kila nusu saa uwezo wake ni 20%. Ukikaa nayo muda murefu (zaidi ya saa)yenyewe ndiyo inakuwa source ya kukuambukiza. Hizo PPEs wanazotakiwa kuvaa watoa huduma wa afya bei yake ni sh laki tano, na zinatakiwa kubadilishwa kila saa moja (disposable).

Na bado udhibiti wake wa virusi hivi ni kama 80% tu! Haya mambo si rahisi scientifically. Isitoshe barakola nyingi zinazoingizwa nchini zinaelekea zilishapandikizwa virusi vya corona. Barakola hizi zinasaidia tu kupunguza hofu kwa wasiojua lakini ni more risk na hatari sana hasa zinapotumika visivyo. Kumuamini Mungu kunatoa hofu hii bila risk yo yote. Na hichi ndicho rais wetu alichokuwa amekifanya kuanzia mwezi April 2020. Vifo vya corona vilitoweka baada ya wananchi kuondokewa na hofu. Walimuamini Mungu, waliamini nyungu na dawa zingine za asili. Sasa kanisa katoliki limeturudisha tulikotoka - kwenye hofu na taharuki. Vyama vya upinzani na mabeberu wame take advantage. Tusikubali.

Social distancing kwa mazingira yetu ni next to impossible na lockdown ndiyo balaa zaidi.

Vita vya dunia ya sasa zinatumia silaha za kibiolojia za mRNA.

Napenda sana watu wanaoanalyse mambo namna hii badala ya kukimbilia ku conclude.
umesema kweli sana.
 

GREAT VISIONAIRE

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
359
500
Fuatilia katika google shirika taasisi inaitwa GAVI, na mwaka jana waliingia december, Tanzania kupitia wizara ya afya kuandaa mazingira ya chanjo kabla mh. Hajapiga ban.
Kama ilivyokuwa mkutano wa berlin, mabeberu waligawana makoloni basi sasa hv wanagawana masoko. Ndio maana gates na gavi yake na wenzake wamelenga africa, urusi ana yake, china ana yake, marekani na Europe wana zao pia tofauti.

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom