China na Afrika zaimarisha ushirikiano katika sekta ya anga ya juu

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
43a0-iittafs1749817.jpg


Juu ya Mlima Entoto, ulioko takriban kilomita 20 kaskazini mwa mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, Kituo cha Utafiti wa Anga ya Juu cha Entoto kinavutia macho sana. Mafundi wa China na Ethiopia wanaovalia sare wanarekodi data iliyorejeshwa na satilaiti ya kwanza ya Ethiopia ETRSS. Satelaiti hiyo iliyotolewa na China, inatumiwa zaidi katika shughuli za kilimo, misitu, rasilimali za maji na ufuatiliaji wa majanga nchini Ethiopia.

Katika miaka ya hivi karibuni, sekta ya anga ya juu imezidi kuwa sehemu muhimu katika ushirikiano kati ya China na Afrika. Pande hizo mbili zimepata mafanikio mazuri katika nyanja mbalimbali ikiwemo kujenga kwa pamoja miundombinu, matumizi ya pamoja ya data zilizotolewa na satelaiti, utafiti wa satelaiti mpya, na mafunzo maalum.

Mwaka 2017, Umoja wa Afrika ulitoa “Sera na Mkakati wa Anga ya Juu za Afrika”, na kuamua kuanzisha Shirika la Anga ya Juu la Afrika ili kuratibu ushirikiano wa kimataifa. Kutokana na umuhimu wa sekta ya anga ya juu katika kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na kuboresha uzalishaji na maisha ya watu, teknolojia ya kisasa ya anga ya juu inathaminiwa sana na nchi za Afrika. Ripoti iliyotolewa na Shirika la Anga ya Juu Barani Afrika inaonyesha kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, bajeti za nchi za Afrika kwa ajili ya shughuli za anga ya juu zimeongezeka kwa kasi kikubwa. Kutokana na msingi dhaifu, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ni njia rahisi kwa nchi za Afrika kutimiza lengo lao la kuendeleza teknolojia ya anga ya juu. Maafisa wa Shirika la Anga ya Juu la Afrika wanasema, China ni mshirika na muungaji mkono wa lazima kwa Afrika ili kutimiza ndoto ya anga ya juu.

Misri ni nchi ya kwanza kufanya ushirikiano wa satelaiti na China chini ya mfumo wa ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Mwaka 2016, China na Misri zilisaini makubaliano kuhusu mradi wa kusaidia kujenga kituo cha kuunganisha na kupima satelaiti nchini Misri. Katika siku zijazo, Misri itakuwa nchi ya kwanza ya Afrika yenye uwezo wa kuunganisha na kupima satelaiti. Hivi sasa, Idara ya Kitaifa ya Anga ya Juu ya China na Mamlaka ya Sayansi na Teknolojia ya Anga ya Juu ya Misri zimezindua miradi mipya ya ushirikiano, ikiwemo ujenzi wa jengo jipya la ofisi za Shirika la Anga ya Juu la Afrika, kituo cha satelaiti cha AIT cha urambazaji na mawasiliano, kituo cha utafiti na maendeleo na jumba na maonesho.

Mbali na kutoa msaada wa vifaa na miundombinu, China pia inatoa mafunzo ya hali ya juu kwa watafiti wa Afrika katika kubuni, kutengeneza, kurusha na kudhibiti satelaiti. Kituo cha Elimu ya Sayansi na Teknolojia ya Anga ya Juu, kilichoko katika Chuo Kikuu cha Beihang, China, kinatoa elimu na mafunzo ya anga ya juu kwa watu wanaotoka barani Afrika. Tangu mwaka 2014, wanafunzi 32 kutoka nchi 8 za Afrika ambazo ni Algeria, Misri, Ethiopia, Togo, Cameroon, Msumbiji, Nigeria na Sudan wamehitimu kutoka kituo hicho baada ya kumaliza masomo ya shahada ya pili.

Waraka wa “Ushirikiano kati ya China na Afrika katika Enzi Mpya” uliotolewa hivi karibuni na Baraza la Serikali la China unasema China imeimarisha kikamilifu mawasiliano ya kimkakati na Afrika katika uvumbuzi wa sayansi na teknolojia ya juu, na mafanikio mapya yamepatikana katika ushirikiano wa anga ya juu. Katika zama mpya ya maendeleo, ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta ya anga ya juu utaendelea kupata maendeleo makubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom