China na Afrika zaendelea kuimarisha uhusiano wa kibiashara

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,006
1,026
TZ.jpg

Na Fadhili Mpunji

Maonyesho ya pili ya biashara na uchumi kati ya China na Afrika yanaendelea kufanyika mjini Changsha, Hunan kusini mwa China. Maonyesho haya ni moja ya majukwaa muhimu ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na nchi za Afrika, na ni fursa adimu inayotolewa na China kwa nchi za Afrika kuonyesha bidhaa zake moja kwa moja kwenye soko la China.

Maonyesho haya yaliyofunguliwa Septemba 26 yanafanyika wakati dunia bado haijaondokana na janga la COVID-19, na katika kipindi ambacho changamoto za uchumi zinaendelea kuzitatiza nchi duniani. China imeweza kuandaa maonyesho haya katika mazingira kama haya, na kuwaalika wafanyabiashara karibu 900 kutoka katika nchi 40 za Afrika.

Maonyesho haya ni moja ya juhudi za serikali ya China kufungua moja kwa moja soko lake kwa wafanyabiashara na wakulima wa Afrika, ambao kutokana na changamoto za gharama, taratibu za karantini na forodha, inaweza kuwa vigumu kwao kulifikia soko la China. Lakini kupitia maonyesho haya taratibu zimepunguzwa na wafanyabiashara hao wanaweza kuja kwenye soko la China kuuza na kutangaza bidhaa zao.

Tukumbuke kuwa taratibu za karantini na hatua mbalimbali za kupambana na janga la COVID-19 bado zinaendelea, na kufanya baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchi za Afrika waliokuwa na nia ya kushiriki washindwe kufika China. Uzuri ni kwamba mbali na ushiriki wa moja kwa moja wa wafanyabiashara kutoka nchi za Afrika, kulikuwa na maonyesho mengine kwa njia ya mtandao wa internet. Kupitia maonyesho hayo, bidhaa kutoka nchi mbalimbali za Afrika kama vile kahawa kutoka Ethiopia, ufuta kutoka Tanzania na pilipili nyeupe kutoka Cameroon zimeweza kuuzwa kwa wachina.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita makampuni mengi madogo yanayofanya biashara kati ya China na nchi za Afrika, yalikumbwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na ugumu wa kuagiza bidhaa kutoka nje ya Afrika. Janga la COVID-19 lilitokea katika wakati mbaya, ambapo ushirikiano wa kiuchumi hasa ule wa kunufaisha (win-win) kati ya China na Afrika ulikuwa ukishika kasi. Kulikuwa na mfululizo ya maonyesho ya biashara yaliyokuwa fursa nzuri kwa wakulima na wafanyabiashara wa Afrika.

Mbali na biashara ya mazao ya kilimo, maonesho haya pia ni fursa nzuri kwa nchi za Afrika kuonyesha vivutio vya utalii na wachina kujionea vitu mbalimbali vya sanaa za Afrika vilivyoletwa kwenye maonyesho hayo.
 
Back
Top Bottom