China na Afrika kushirikiana zaidi katika anga za juu

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
228
250
VCG31N1235908242.jpg

W020191220513625276468.png

Wikiendi hii iliyopita, chombo cha kubeba binadamu cha anga za juu cha Shenzhou-13 kilifanikiwa kuwapeleka wanaanga wengine watatu katika Kituo cha Anga za Juu cha China. China ni nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, na maendeleo yake kwenye sekta ya safari ya anga za juu ni hamasa kubwa kwa nchi za Afrika zitakazoingia katika kipindi cha maendeleo ya kasi kwenye sekta hiyo, na pia kuonesha kuwa upuuzi na ukandamizaji haviwezi kuzuia nchi kufanya uvumbuzi na kujifanyia mapinduzi kisayansi.

Katika Ajenda yake ya 2063, Umoja wa Afrika ulipitisha “sera ya anga za juu barani humo”, na kusisitiza umuhimu wa anga za juu kwa maendeleo ya Afrika kwenye kilimo, usimamizi wa maafa, utabiri wa hali ya hewa, na sekta nyinginezo. Kwa mujibu wa makadirio ya kampuni ya ushauri ya Space in Africa, thamani ya sekta ya safari ya anga za juu ya Afrika kwa sasa ni dola za kimarekani bilioni 7 hivi, na inatarajiwa kuongezeka hadi dola bilioni 10 katika miaka mitano ijayo.

Kwa kujenga kituo binafsi cha anga kiitwacho “Tiangong”, China inaweza kuhimiza maendeleo ya safari ya anga za juu ya Afrika, na kuziwezesha nchi za bara hilo zitimize ndoto ya kupata bidhaa za teknolojia ya anga za juu.

Katika kuunga mkono mpango wa safari ya anga za juu wa Afrika, katika miaka ya hivi karibuni, urushaji na matumizi ya satilaiti vimekuwa vikipewa kipaumbele katika ushirikiano kati ya China na Afrika. Tangu satilaiti ya kwanza irushwe barani Afrika miongo miwili iliyopita, nchi 13 za Afrika zimerusha satilaiti 44 kwenye anga za juu. Inakadiriwa kuwa katika miaka mitatu ijayo, satilaiti zitakazorushwa na nchi za Afrika zitafikia 110.

Ofisa wa Mamlaka ya Anga za Juu ya Umoja wa Afrika Islan amesema China ni mwenzi muhimu wa ushirikiano katika kuunga mkono ndoto ya anga ya juu ya Afrika. Ikiwa mkandarasi mkubwa wa nne wa satilaiti wa Afrika, China imesaidia nchi za Afrika kama Nigeria, Algeria, Sudan kutengeneza na kurusha satilaiti.

Mwezi Desemba mwaka huu, China pia itasaidia Ethiopia kurusha satilaiti ya pili yenye uwezo wa kutambua kutoka mbali kwa ajili ya matumizi ya utabiri wa hali ya hewa na usimamizi wa mazingira na mazao ya kilimo. Katika kusaidia Afrika kukabiliana na changamoto zinazotokana na janga la COVID-19 kwa sekta ya matibabu na elimu, teknolojia ya anga za juu inayotolewa na China imetajwa kuwa na umuhimu mkubwa katika kueneza ujuzi miongoni mwa watu kuhusu kupambana na virusi na kuhakikisha masomo yanatolewa kwenye mtandao wa internet barani Afrika.

China ikiwa nchi inayowavutia vijana wa Afrika kwa wingi zaidi kusoma, pia imetumia njia mbalimbali kama vile kutoa ufadhili wa masomo, kuzindua umoja wa uvumbuzi wa anga za juu wa“Ukanda Mmoja, Njia Moja”na kufanya semina mbalimbali ili kutoa mafunzo kwa vijana wenye nia ya kutimiza ndoto ya anga za juu wa Afrika. Mbali na hayo, China inajadili uwezekano wa kualika wanaanga wa kigeni wakiwemo wale wa Afrika kutembelea kituo chake cha anga.

Imefahamika kuwa mradi wa majaribio ya kisayansi ya anga za juu unaotolewa na vyuo vikuu vya Kenya umeidhinishwa na China na kuingia kwenye orodha ya kwanza ya miradi ya matumizi ya kituo cha anga cha China, jambo ambalo linamaanisha kuwa wanasayansi wa Kenya wataingia kwenye kituo hicho hapo baadaye. Ni jambo lisilopingika kuwa mafunzo na mawasiliano kama hayo yatainua uwezo wa Afrika kuendeleza mpango wake wa anga za juu.

China inajitahidi kushirikiana na nchi za Afrika kwenye sekta ya anga za juu, ikitoa mfano wa kuigwa kwa ushirikiano kati ya Kusini na Kusini, na pia kufungua njia mpya kwa ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya anga za juu. Uwezo unaoongezeka wa China utafanya nchi hiyo kuwa mchangiaji muhimu wa juhudi hiyo ya kimataifa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom