CHINA: Marekani iwajibike kwa kueneza UKIMWI Duniani na seasonal flue mwaka 2009 maana chimbuko la H1N1 na UKIMWI ni Marekani

Je, Marekani imelipa hasara kutokana na majanga ya H1N1, UKIMWI na msukosuko wa fedha duniani?

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema, Marekani inapaswa kufahamu kuwa adui wao ni virusi, sio China, kwani kama nchi nyingine, China pia ni mwathirika wa maambukizi ya virusi vya Corona.

Geng amesema hayo baada ya Rais Donald Trump wa Marekani jana kusema China inapaswa kuwajibika kwa ueneaji wa virusi hivyo.

Geng amesema virusi ni adui wa binadamu wote, na vinaweza kutokea wakati wowote na mahali popote, na China ni mwaathirika wa virusi hivyo. Ameongeza kuwa, hakuna aliyeiwajibisha Marekani kwa majanga yaliyoanzia nchini humo kama mafua ya H1N1 yaliyotokea nchini Marekani mwaka 2009 na kuenea katika nchi 214 duniani, na kusababisha vifo vya watu laki mbili, na pia mgogoro wa kifedha uliotokea mwaka 2008 nchini Marekani na kusababisha hasara kubwa ya kiuchumi duniani, aidha ugonjwa wa UKIMWI pia ulitokea kwanza nchini Marekani.

Geng amesisitiza tena kuwa, kwa mshikamano na ushirikiano tu, ndio jumuiya ya kimataifa itashinda virusi vya Corona, ameitaka Marekani kuacha kuipaka matope China, na kujishughulisha vizuri zaidi na juhudi za kukabiliana na virusi hivyo.
Heri ukimwi ukifuata masharti n dawa unakaa hata miaka 25,sio hii china virus wk 3 tu kwisha habari yako.unazikwa kama mzoga wa mbwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heri ukimwi ukifuata masharti n dawa unakaa hata miaka 25,sio hii china virus wk 3 tu kwisha habari yako.unazikwa kama mzoga wa mbwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ukiwekewa ugonjwa au sumu ya kukufanya kuumwa ukaambiwa tutakupa dawa nyingine ya kukusaidia angalau uishi miaka 25 utakubali? uishi miaka 25 ya mateso au ufe baada ya wk 3......
 
Mkuu Hivi hizi program za UKIMWI anazozifund US Hao wachina hawazioni? Naskia Arvs Ni Bure. Nani anafund? Ni US. Atleast they are trying to correct their mistake not to run away from it.

China has to pay and she has to pay dearly. Kwa kupika takwimu na kuchelewa kutoa tahadhari kwa nchi nyingine kuhusu Corona. Yaani walipe for every life that has been lost na wakikataa hakuna kuwalipa loans zao walizokopesha Mataifa mengine na ikibidi they should be isolated by the international community.

Those communists will try to do a cover up lakini naamini joint investigation itawaumbua.Yaaani wafanyiwe kama alichofanyiwa Germany baada ya Kulost World War 1. Racists China.

Yes Keyboard Warrior.
Hujaelewa china anasema nini , ni hivi Ukimwi umeua maelfu ya watu nani kamuajibisha Marekani ? au hayo mafua yameua watu kibao nani kamuajibisha marekani ? unapotuambia ARVS bure hii haitibu ugonjwa yenyewe ni mateso pia vidonge gani ukianza kunywa unakunywa mpaka unakufa !! swali zile roho zilizo kufa na ukimwi au mafua yale marekani aliwajibishwa na nani ?
 
Heri ukimwi ukifuata masharti n dawa unakaa hata miaka 25,sio hii china virus wk 3 tu kwisha habari yako.unazikwa kama mzoga wa mbwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Na wale waliokufa na ukimwi vip marekani kawajibika vip ? hizo sio dawa ni mateso wewe dawa gani kila siku unakunywa !! watu wengi wamekatisha dozi baada ya kuchoka vidonge hivi wameishia kufa
 
Ili kweli kuonesha kwamba hizo program za UKIMWI ni sehemu ya kuwajibika kwa walichofanya walitakiwa kufanya yafuatayo:

1, Kukiri hadharani kwamba wao ndo chanzo cha ukimwi kuwepo na kuenea duniani.
2. Watueleze sababu zilizowafanya wakitengeneze halafu wakisambaze duniani hasa bara la Afrika
3. Waseme kwanini nguvu kubwa inaelekezwa kwenye kutengeneza dawa za ARVS kuliko kupata kinga au tiba ya jumla
4. Je, ni kweli ARVS na program nyingine za UKIMWI zinatolewa bure au kuna masharti wanawekeana na serikali zetu yenye malengo ya kuwanufaisha wao ki uchumi

Vinginenyo chochote kinachofanyika ni usanii tu kama usaniimwingine
Yani ni sawa na MTU alietengeneza virus kwenye computer then akatengeneza antivirus... Ndo walichofanya wahusika kwa maslahi yao.

Majuzi walituwekea kamgomo baridi kondom zikahadimika sana(kama sikosei ni kipindi kile mkulu aliposema tuzaliane tu kama tutakuwa na uwezo wa kulea yani kila MTU azae kutokana na uwezo wake), nadhani mpaka sasa bado hazija shuka.

Hiyo ilikuwa ni intro tu, movie nzima itaonekana tukikosa ufadhili wa A.R.V ingawa sisi sio chanzo cha huu ugonjwa ila ndio tumekuwa wahanga wakubwa!

N.B:- Sio wazungu wote wanapenda hivi vitendo ndio maana huwa tunatumia neno mabeberu na sio wazungu, mabeberu(imperialists) hawa ni watu wachache lakini wenye uwezo wakuchukua maamuzi makubwa kuiendesha Dunia watakavyo kutokana na nguvu waliyo nayo kiuchumi...

Hii teknolojia inasaidia sana kama ikitumika vizuri, lakini ikitumika vibaya hasara yake huweza kugharimu maisha ya wengi.






Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom