Corticopontine
JF-Expert Member
- Sep 20, 2019
- 664
- 1,272
Je, Marekani imelipa hasara kutokana na majanga ya H1N1, UKIMWI na msukosuko wa fedha duniani?
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema, Marekani inapaswa kufahamu kuwa adui wao ni virusi, sio China, kwani kama nchi nyingine, China pia ni mwathirika wa maambukizi ya virusi vya Corona.
Geng amesema hayo baada ya Rais Donald Trump wa Marekani jana kusema China inapaswa kuwajibika kwa ueneaji wa virusi hivyo.
Geng amesema virusi ni adui wa binadamu wote, na vinaweza kutokea wakati wowote na mahali popote, na China ni mwaathirika wa virusi hivyo. Ameongeza kuwa, hakuna aliyeiwajibisha Marekani kwa majanga yaliyoanzia nchini humo kama mafua ya H1N1 yaliyotokea nchini Marekani mwaka 2009 na kuenea katika nchi 214 duniani, na kusababisha vifo vya watu laki mbili, na pia mgogoro wa kifedha uliotokea mwaka 2008 nchini Marekani na kusababisha hasara kubwa ya kiuchumi duniani, aidha ugonjwa wa UKIMWI pia ulitokea kwanza nchini Marekani.
Geng amesisitiza tena kuwa, kwa mshikamano na ushirikiano tu, ndio jumuiya ya kimataifa itashinda virusi vya Corona, ameitaka Marekani kuacha kuipaka matope China, na kujishughulisha vizuri zaidi na juhudi za kukabiliana na virusi hivyo.