China, Libya, Dubai, wote tulikuwa level moja kiuchumi; naweza sema Nyerere alikuwa na maono hafifu sana

kwa mtoa hoja na wengine wenye akili mgando kumjadili nyerere kwamba ameiangusha tanzania kwa kukosa maono au uzembe ni sawa na wewe mwenyewe kukosa maendeleo ukiwa na miaka 50 toka uzaliwe na kumlaumu babako na mamako kuwa walikosa maono. sasa wewe mwenye maono lete maendeleo basi...hakuna kitu....pambafu kabisa....mmekaa kula rushwa hakuna mnachoweza kazi maneno ya kishogashoga Kwenye mitandao.

Mnafikiri maendeleo yanakuja kwa porojoporojo za kipumbavu?

Fanyeni kazi.
 
Watu tuliosoma wakati wa Nyerere elimu yetu haina shaka hata kidogo. Elimu ilianza kufa baada ya Mwalimu kondoka madarakani.
Wanaotusainia mikataba wamesoma wakati wa jk eee
 
Huwezi linganisha ukubwa wa Dubai na Tz, wala watu wake na wa Tz.
Ni rahisi sana kucomplain, ila ukitulia ukawaza na ukamsikia alivyokuwa anajustify ungeelewa
Na udogo wao hawana aridhi madini, ilaaaaaa
 
Tena wee jama usinishangaze Mugabe ana digree ngapi unajua lakini? Ila yeye na nchi yake ni maskini
Sisi tulikuwa na madini hadimu
Kila kitu hadimu, hafi mlima vivutio, mafuta, Aridhi, kwani kwa Gadaff walisoma kwanza?
mwache mzee apumzike alikufa masikini kwa level zake angejineemesha sana aliitakia mema nchi lakini kwa makosa yenu mnamlaumu yeye. Je sasa hivi mnafanya nini tofauti kwa manufaa ya nchi baada ya kugundua yeye alikosea?, Je mnajifunza kutoka makosa yake au mnamlaumu tuu?
 
Nilijibu kutokana na nilivyoulizwa na wengi vwalitegemea ningefunguka zaidi kuhusu elimu na historia yangu. Ninadhani ilikuwa nzuri dhough
Hahaha but well done. Nikipata muda nitasoma. I was doing meditation for one hour. nimemaliza nina monks wananisaidia kujifunza meditation.
 
uko vizuriii
Baada ya kuona mkataba wa Williamson Diamond na mikataba mingine ilivyosainiwa kwa hila, Nyerere aliona ni vyema kusubiri Tanzania iwe na wasomi wa kutosha ambao wataweza kusimamia mikataba.

Baada ya uhuru alijua kabisa kuwa hakukuwa na wasomi wengi wa kuweza kukabiliana na ulaghai wa mabeberu. Alipokufariki mabeberu yalifahamu mali iliyopo Tanzania na waliifaidi kama ng'ombe alienguka kila mtu anajikatia kipande na kuond
 
Wanaotusainia mikataba wamesoma wakati wa jk eee
Ndo wale waliokuwa wakisubiri mzee ang'atuke kama kipara. Wapo wengi hao hivi unafikiri baba yake le muntus alikuwa anampanda mzee? Wengi walifurahi siku alipogoo.
 
Huwezi linganisha ukubwa wa Dubai na Tz, wala watu wake na wa Tz.
Ni rahisi sana kucomplain, ila ukitulia ukawaza na ukamsikia alivyokuwa anajustify ungeelewa
Ukifika Dubai tembelea kwenye makumbusho ya how Dubai was developed from a village to a city then you will understand. The British explored oil and decided to take the place and pay the kingdom according to what they earn. Waarabu hawakuwa na haraka wala shida sababu walikuwa na samaki, lulu toka baharini na watumwa hivyo things were good. Walipokea kidogo kidogo na mpaka sasa wanapokea mrahaba na wanafaidi hawana shida. Wafanyakazi wanatoka nje siyo wao wala hawana muda wa kupigwa jua sisi tunapiga kelele weee.
 
Kwamba hata hao wasomi tunaowategemea wametuangusha.Angalia hizo ripoti za madini wanaotajwa na elimu zao. Si bora wajinga ambao hawana elimu. Kwangu mara elfu ya Makonda kuliko maprof kama Muhongo au Lipumba and co.
 
Kwa upande wangu ngoja nichangie kama ifuatavyo.
Nyerere alikuwa kiongoz mwadilifu lakin hakuwa na vision. Nitatoa sababu.
Mzee kweli alikwenda UN kuomba kujitawala na kwa hilo kwa kushirikiana na wenzie alifanikiwa. Baada ya kujitawala Nyerere alikuwa mbinafs Sana hakupenda mawazo ya wenzie na wala hakutaka wenzie wapewe sifa kama zake. Mfano mdogo baada ya kwenda China akaja na ujamaa wake ambao mpaka Leo hauelewek ni ujamaa wa kimax au ni ujamaa wa kiafrica. Kambona aliona madhara ya hiyo kitu mapema akampinga Nyerere mpaka yule Mzee anaondoka mawazo yake yalikuwa sahihi.
Alimpinga Mzee Mtei kwenye marekebisho ya kiuchumi ili kuendana na ulimwengu mpaka Mtei anaachia kaz na Nyerere kuondoka madarakan ndio ilikuja kujulikana yule Mtei alikuwa sahihi coz baadae walikuja kukubaliana nayo ambao it's to late.
Nyerere alitunga katiba nzur kwa wakat wake akadhibit kila kitu nakubaliana nae lakin yeye alijua hii katiba anaweza kutokea mtu akawa rais na ikamfanya dikteta lakin aliiacha na alikuwa na uwezo wa kuibadilisha akakaa kimya ndio imeidumaza nchi mpaka Leo.
Nyerere alitumia hela ndogo tulizokuwa nazo akafadhili vita karibu maeneo yote ya kusin na Kat ya Africa bila mkataba wowote na hao wanaharakati kwamba cku wakishika nchi tunanufaikaje. Matokeo yake Leo hii tumebakiwa na sifa za kijinga tu kuwa tumewasaidia kushika nchi.
Nyerere alipoondoka madarakan alituambia siasa yake imeshindwa sasa cjui kwanini Watu wanataka tumuige mtu aliyekir mwenyewe ameshindwa.
Nyerere kwa mdomo wake mwenyewe alituambia wakat wa utawala wake kuna mengi mazur alifanya ila kuna mabaya pia sasa hatujawah kujulishwa makosa aliyofanya ni yapi huenda Ndio yaliyotufanya tumekuwa mburula mpaka Leo.
Nyerere mpaka anaondoka ikulu Alishindwa kabisa kujenga nyumba yake ya kuishi kijijin sasa cjui tunataka kuiga Umasikin au.
Nyerere alikua dhaifu Sana. Hatujawah kuambiwa alivyounganisha makabila b4 alikuta kabila gan na gan wakapigana .
Mwisho nachoona ni kuwa hii nchi Iko hv kwa sababu ya Nyerere kataa kubali ukiona watoto ni mbulula tambua baba yao alikuwa mbulula plus. Haikuwekwa misingi shirikishi hii nchi ilijengwa na Watu waadilifu wasiokuwa na maono. Vision.
Sory kwa niliowaumiza.
 
Kwamba hata hao wasomi tunaowategemea wametuangusha.Angalia hizo ripoti za madini wanaotajwa na elimu zao. Si bora wajinga ambao hawana elimu. Kwangu mara elfu ya Makonda kuliko maprof kama Muhongo au Lipumba and co.
Nakuunga mkono 100% wasomi wengi waliweka makucha ndani wakati wetu wakasubiri mzee ang'atuke. Je, kama ingekuwa mambo ya dynasty kama N. Korea watoto wa Nyerere si wangeamua kuchukua utawala wakati anatoka madarakani? Elimu tuliipata na mzee alikuwa na uelewa aliagiza expatriate toka Scandinavia, UK, US, Australia mpaka warusi na wahindi walikuja tulikuwa na walimu wa kila aina. Tulipata elimu nzuri saana. Kilichotokea tukawa tunalazimishwa kuwa wanachama wa Tanu baadaye CCM hapo sasa ndo kila kitu kilikufa. Sisi tuliokuwa na kadi lakini hatukushughulika nazo tukatupwa chini tukabaki bila vyeo wala kupanda madaraja.
Mimi ni mmoja wa wahanga wa elimu ya CCM nilikataa kutoa kadi ya CCM ili kwenda Mlimani what for? Hapo ndo unaona watu wengi walichukua hiyo loop hall kutapeli nchi na siasa kwa ujumla. Watu commited walikataa kulazimishwa na wale cha kupewa walinunua kadi ndo wanatusumbua sasa hivi.
 
Simtetei Baba wa Taifa ila wewe OP ni kilaza. Unapofungua thread uwe na facts za ukweli.
1. Ivi Dubai wameendelea kwasababu ya mafuta? Jibu ni hapana.
2. Je tumeshawai kuwa sawa na wachina? Jibu ni hapana.
Nenda kasome afu uje...
 
Baada ya kuona mkataba wa Williamson Diamond na mikataba mingine ilivyosainiwa kwa hila, Nyerere aliona ni vyema kusubiri Tanzania iwe na wasomi wa kutosha ambao wataweza kusimamia mikataba.

Baada ya uhuru alijua kabisa kuwa hakukuwa na wasomi wengi wa kuweza kukabiliana na ulaghai wa mabeberu. Alipokufariki mabeberu yalifahamu mali iliyopo Tanzania na waliifaidi kama ng'ombe alienguka kila mtu anajikatia kipande na kuondoka.
Wewe utakuwa muhenga tu
 
Acha uongo mleta mada. Hatukua sawa na China wakati wa uhuru kwetu. Hata miaka 3000 kabla bado hatujawahi kuwa sawa nao. Walikua na Taifa na falme ambazo zipo kwenye rekodi mpaka leo. Wakawa na mwanafalsafa ambae hadi leo anafahamika kanuni zake. Confusius. Leo hii chuo kikuu Dar wana taasisi yake.

Maelfu zaidi ya miaka nyuma walijenga ukuta Mkuu wa China (Chinese Great Wall). Waligundua gurudumu likawapelekea kugundua zana rahisi ya toroli na kurahisisha sana kazi. Waligundua kuchapisha (printing) kabla hata hatujajua maandishi ni nini hiyo ikawawia rahisi kutunza kumbukumbu na kutoa maelekezo yaliyonyooka kisiasa, vitani, darasani, kiuchumi n.k. By then sisi wala hatukua tumeshaanza kusafiri kuja Tz. Labda waSandawe na waIraqw tu ndo walikuwepo.

Kimbia mpaka uhuru na baadae kdg. Usisahau wao ndo walijenga Tazara na kuweka treni zao. Wakatuletea chemli na jiko la mchina. Baiskeli ya Phonexi na baadae Shangsheng (Guta... anashangiliwa na umati wa watuuu...).

Sisi tuliwahi kupeleka nini China enzi zile? Namaanisha bidhaa za viwandani. Sanasana Nyerere alienda huko akarudi na falsafa 2. Ujamaa na "Zidumu fikra za mwenyekiti"
 
Tena avanter yako hiyo ni ya huyo mzee
Tulikuwa hatuna tofauti kubwa na libya
Wala china mkuu. Tofauti ilikuwa ndogo , kama angewatumia wawekezaji wakachimba tanzanite kama wenzie wa nchi nyingine walivyofanya tungekuwa mbali
Maino maono sasa nani anayachimba kwa alivyoviacha aridhini
Alikuwa na maono hafifu.
Biashara asubuhi
Wawekezaji wamekuja wamechimba gesi Songosongo na ikaanza kutumika 2004 , jiulize bei ya umeme ikoje ?
Miaka ya 70 kuelekea 80 hadi mwanzoni wa 90 Tanganyika Packers pale Kawe ilikuwa inachinja Ng'ombe 1100 kwa siku julize kilichotokea baada ya hapo. Kiwanda cha maziwa Ubungo kilikuwa kinazalisha lita 75,000 kwa siku - leo kimefungwa
TAMCO kibaha ilikuwa ina assemble Scania , tairi zikiwa za General Tyre - Arusha, Betri toka Yuasa waliokuwa Pugu Rd, Spring zikitoka TASIA ya Dewji , Radiator zikitoka Afro Cooling hapahapa Bongo jiulize leo tumefikaje hapa.
Cheapest technology kwa nchi inayotaka kuingia kwenye uchumi wa viwanda ni Textile, na tulikuwa na viwanda kibao , walivyoingia wenye akili wakavifunga. Tulikuwa na kiwanda cha Maziwa Utegi kule mkoa wa Mara kilichokuwa kinazalisha
UHT milk pamoja na Maziwa ya unga - Skimmed Milk POwder na Whole milk powder. Leo kwenye shelves yamejaa maziwa toka Kenya. Kwa upande wa kilimo tulifikisha 900 kg za pamba kwa acre , Egypt wanapata 1300 kg leo kwenye ekari moja tunapata 250 kg.
Makosa makubwa yamefanyika kuanzia 90's kuendelea ambapo Tanzania ya leo haiwezi zalisha hata kiberiti cha njiti.
Sijui ni muujiza gani utakaotumika ili kutengeneza ajira kwa vijana wanao graduate kwenye vyuo vyetu
 
Akili huna kaka,...okay,tuanzie kwanza,mwaka 1961 tz ilikua na idad ya watu wangap compared na hzo china etc,.kiwango cha elim cha watu wetu na idad ya waliopelekwa nje kipind cha ukolon ilikua ngap compared na china na hzo nchi ulizo mention,.ushawai jiuliza au taka ujua aina ya uhuru tuliopewa sis wazungu ?uhuru wa nchi hzo ulizotaja ulifanyika miaka ipi,je mashirika na taasis kama,ya umoja wa mataifa ambayo yanaweka rules kwenye dunia je tanzania ilikuta yameshaanzishwa ama bado compared na hzo nchi ulizotaja,? ..usimlaum nyerere utakua huna akil,..haya tuje upande wako,wew umefanya mangap ya maana tokea upata elim had leo hii?jib haya yote na uchambue,kama una akili utakua ushapata jib
 
Hivi Tanzania tunachimba mafuta? Kila siku naskia Mikataba ta Mafuta ipitiwe upya, ni mafuta gani hayo??


China/ulaya 2018 itapiga marufuku utumiaji wa magari ya mafuta kulinda mazingira hayo mafuta tuliyo nayo tutayapeleka wapi??
 
Libya walikua wako mbali kielimu mkuu ukisoma historia ya zamani libya ilikua mbali sana, sasa Tanzania yenyewe hii watu serikali inatimiza wajihu wake wa kujenga barabara, shule, zahanati na hospitali wananchi wanashangilia sababu ya ujinga, umaskini wataelewa nini Tanzania elimu duni, watu duni, maendeleo duni...
 
Back
Top Bottom