China kupunguza mkopo kwa Afrika si picha kamili ya ushirikiano kati ya pande mbili

ldleo

Member
Jan 9, 2010
52
125
VCG111255060988.jpg

Utafiti mpya uliofanywa na “Pendekezo la Utafiti kati ya China na Afrika” CARI la Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha Marekani umeonesha kuwa mwaka 2019, mikopo iliyotolewa na China kwa Afrika ilipungua kwa theluthi moja, kitu ambacho kinaashiria kuwa China imepunguza kwa kiasi kikubwa mikopo yake kwa Afrika kutokana na msukosuko wa madeni unaolikabili bara hilo. Kwa sababu takwimu zilizokusanywa na CARI zilitokana na idara za serikali za China na Afrika pamoja na ripoti za vyombo vya habari, matokeo ya utafiti huo yanadhaniwa kwamba yanaendana na hali halisi, lakini hayawezi kuonesha picha kamili ya uhusiano wa ushirikiano kati ya China na Afrika.

Waraka uliotolewa na serikali ya China mwezi Januari mwaka huu kuhusu ushirikiano wa maendeleo ya kimataifa wa China katika zama mpya umesema katika miaka ya hivi karibuni, China imepanua wigo wa fedha za misaada kwa nchi za nje, na kusisitiza kuwa nchi hiyo inazijali sana nchi zilizo nyuma zaidi kimaendeleo barani Afrika, na kupendelea kufanya nazo ushirikiano wa maendeleo ya kimataifa.

Kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2018, fedha za misaada zilizotolewa na China kwa nchi za nje zilifikia dola za kimarekani 415, ikiwa ni pamoja na msaada wa zawadi, mkopo usio na riba na mkopo wenye riba nafuu. Katika miaka hii mitano, fedha za misaada zilizotolewa na China kwa nchi za Afrika zilichukua asilimia 44.65 ya misaada yake yote kwa nchi za nje, kiasi ambacho kimekuwa kikubwa sana kuliko sehemu nyingine duniani.

Baada ya kulipuka kwa maambukizi ya virusi vya Corona, kutoka msaada wa vifaa vya matibabu, kupeleka madaktari hadi kuahirisha kulipwa kwa madeni, China pia imeongeza msaada wake ili nchi za Afrika ziweze kukabiliana na msukosuko huo wa afya ya umma ulioibuka ghafla. Ikiwa nchi iliyotoa mchango mkubwa zaidi miongoni mwa kundi la G20, China pia imesamehe mikopo isiyo na riba ambayo imeshafikia muda wa kulipwa kwa nchi 15 za Afrika.

Mbali na kuendelea kutoa fedha za misaada, ili kuendana na mabadiliko ya hali mpya, China imerekebisha na kufanya mageuzi jinsi ya kutoa misaada kwa nchi za nje na kuimarisha usimamizi kwa utoaji mikopo. China itatathmini kwa uangalifu zaidi miradi ya nchi za nje inayohitaji mikopo. Ni kweli kuwa mwaka 2019, mikopo ya China kwa Afrika ilipungua, lakini kwa ujumla, misaada ya China haitapungua. China inachukua nafasi ya “chombo cha utulivu” kwa Afrika kukabiliana na suala la madeni, na kama ilivyosemwa ripoti hiyo ya utafiti wa CARI, “China itaendelea kuwa chanzo muhimu cha fedha zinazokusanywa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika nchi za Afrika.”

Kwa miaka mingi, vyombo vya habari vya magharibi vilichafua jina la China kwa kusema misaada iliyoitowa kwa nchi za Afrika ina “madhumuni ya kisiasa”, na kupunguza matumaini na uendelevu wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya pande hizo mbili. Lakini tuhuma zisizo na msingi na uwongo wenye nia mbaya haviwezi kuathiri ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika. Katika siasa za kijiografia, nchi yoyote nje ya bara la Afrika haipo katika hadhi ya uongozi barani humo, na misaada ya China kwa Afrika kamwe haibebi sharti lolote la kisiasa.

Maambukizi ya virusi vya Corona yameupa hasara uchumi wa dunia. Mwaka jana, China ilikuwa ni nchi pekee miongoni mwa makundi makuu ya kiuchumi duniani kupata ukuaji chanya wa uchumi. Na “utafiti kuhusu chanjo” unaojitokeza siku hizi umefanya uchumi wa nchi za Afrika ambazo zinahitaji msaada wa nje ili zipite kipindi hiki kigumu uwe dhaifu zaidi. Nchi za Afrika zinakabiliwa na changamoto kubwa za maendeleo, na utekelezaji wa malengo mengi yaliyowekwa kwenye “Ajenda 2030 ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu” umekwama. Katika hali hii, watu wana matarajio makubwa zaidi na jinsi China na Afrika zitakavyokuza ushirikiano wao.

Ukweli ni kuwa mustakabali wa ushirikiano kati ya China na Afrika ni mzuri. Kiuchumi, China na nchi za Afrika zinasaidiana kibiashara. Afrika inaweza kutoa bidhaa zinazohitajika katika soko la China na China pia inaweza kukuza maendeleo ya Afrika kupitia biashara. Mathalan, maonyesho ya 129 ya Canton yanayofanyika kwenye mtandao wa internet na maonyesho ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China ambayo yamefanyika kwa miaka mitatu mfululizo yametoa jukwaa kwa wajasiriamali wa China na Afrika kuwasiliana na kutoa fursa mpya ya maendeleo kwa ushirikiano wa kibiashara kati ya pande hizo mbili haswa katika kipindi cha maambukizi ya virusi vya Corona.

Kwa kupitia njia mseto ikiwemo misaada ya fedha, biashara na uwekezaji, China itaendelea kuhimiza maendeleo endelevu ya nchi za Afrika na kuzisaidia kukabiliana na msukosuko wa madeni.
 

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
11,697
2,000
Sio kupunguzwa,

Waache kabisa kutoa MIKOPO yao UMIZA.

Kiuhalisia MIKOPO ya mchina Ni kichefu CHEFU.

Hailipiki kabisa,
na nchi za kiafrika zikifanya mzaha linauzwa bara lote kwa mchina.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom