China kujenga shule ya usafirishaji nchini Tanzania

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
CHINA%2BPICHA.jpg
Serikali ya China imesema kuwa ipo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania ya kujenga shule ya usafirishaji hapa nchini.
Akizungumza leo (Jumamosi) katika hafla ya kutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini iliyoandaliwa na taasisi ya Confucius, Balozi wa China nchini, Dk Lu Youging amesema wakimaliza mazungumzo hayo wataanza ujenzi mara moja.

Amesema lengo la ujenzi wa shule hiyo ni kuwaongezea ujuzi wahitimu na wale wasiokuwa wahitimu wa vyuo vikuu.

Amesema kwa mujibu wa ripoti ya uwekezaji wa China hapa nchini ni kiasi cha dola bilioni saba huku kampuni zaidi ya 1,000 zikifanya shughuli zake na kutoa ajira 1,200 kwa Watanzania.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo amezipongeza kampuni za China kwa kuisaidia Serikali kupambana na changamoto ya ukosefu wa ajira.

“Wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini wasiichukulie fursa hii kimzaha bali waifanyie kazi kuhakikisha wanakuwa na weledi tofauti na wengine,” amesema Samia na kuongeza:

"Lakini pia wanaposoma wajiandae kwa ajili ya kuajiriwa na kujiajiri, hivyo waongeze ubunifu binafsi kujitofautisha ili kuingia kwenye soko la kuajiriwa na kujiajiri."
 
Hii inshu ilikuwepo na NITwalikuwa wamenunua maeneo chini ya udhamin wa CHINA huko pwani zaidi ya ekari 600 kwa ajili ya upanuzi wa chuo na pia kuboresha miundombinu ya kujifunzia kama kufunga reli fupi kwa watu wa railway engineering na kozi zingine za usafirishaji...sasa sijui kama hii ni project mpya au ni muendelezo wa ile ya awali
 
Imetulia nchii yetu ipo nyuma sana kwenye sekta ya logistics,transportation nk
 
Wahuni hawa. Nakumbuka 2013 walikuja na mbwembwe nyingi eti wanajenga chuo cha kisasa cha VETA mkoani Kagera hadi leo hata kijiko hakijawahi kupelekwa site. Labda kwa vile ilikuwa ni mkoa usiopendwa, huenda kwingineko watajengewa
 
Tatizo wamejaa makanjanja huko sie na vyeti vyetu tunahangaika kitaa
Ni kweli a see,dogo flan kaniambia mzumbe kuna ma prof kumi na tatu walioghushi vyeti! Ideally taasisi nyingi zinaongozwa na incompetent people
 
Back
Top Bottom