China kuipa Tsh. Trilioni 69 Afrika, Tanzania ipo kwenye mgao

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,374
8,109
Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba, amesema Serikali itanufaika na msaada wa miaka mitatu wa dola za Marekani bilioni 30 (Sh 69 trilioni), ulioahidiwa na Rais wa China, Xi Jinping wa kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na umasikini.

Dk Nchemba amesema hayo leo Ijumaa, Agosti 19, 2022 jijini Dar es Salaam katika mkutano wa sita wa Kamati ya Pamoja ya Uchumi, Ufundi na Biashara kati ya Tanzania na China uliomuhusisha Naibu Waziri wa Biashara wa China Qian Keming.

Katika mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao, Dk Nchemba amesema msaada huo ulioahidiwa na Rais wa China Novemba 2021, Mjini Dakar, Senegal, utasaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo hapa nchini.

Amesema kupitia msaada huo miradi tisa imekusudiwa kutekelezwa katika sekta za afya, kilimo, kutokomeza umasikini, kuendeleza biashara, uwekezaji, ubunifu wa teknolojia na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,

“Tumewasilisha China miradi kadhaa ya kimkakati na kipaumbele ili nchi hiyo iisadie Tanzania kupata msaada na mikopo nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi na kuwaondolea wananchi umasikini, tunaamini tutapata fedha hizo” amesema.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China Qian Keming, aliahidi China kuendeleza uhusiano na ushirikiano na Tanzania katika Nyanja ya kiuchumi na kijamii ili kuboresha maisha ya watu.

Amsema China itaendelea kuhamasisha uwekezaji kwa kuzishawishi kampuni kutoka nchini humo kuja kuwekeza Tanzania na kusaidia fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao umewashirikisha mawaziri wa kisekta na waziri wa fedha na mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Saada Mkuya, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba,

Wengine walioshiriki kwenye mkutano huo ni maafisa kutoka wizara ya fedha na mipango na wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 
Hivi ni mkopo au msaada, mbona viongozi hawawi wakweli na wawazi juu ya hili! 🤷🏾‍♂️🤷🏾‍♂️🤷🏾‍♂️
Kunufaika tena kwa mkopo! Hivi ni kunufaika au kukamuana kwenye kuulipa! 🤦🏾‍♂️🤦🏾‍♂️🤦🏾‍♂️
 
Naona mpango anazipigia hesabu pesa za kitonga😂… Aisee sisi Africa tuna maili ndefu sana
 
Back
Top Bottom