Akiongea bungeni, January Makamba amesema China imechagua nchi nne Afrika kuhamishia sehemu ya viwanda vyake na moja ya nchi hio ni Tanzania. Nchi nyingine ni Afrika kusini, Kenya na Ethiopia.
Makamba amesema jambo hilo halijatokea kwa ajali bali kwa jitihada za wizara ya mambo ya nje kwa kazi nzuri inayoifanya na anayoifanya Rais Magufuli ambapo nchi ipo kwenye viwanda kama msingi wake mkuu wa maendeleo wa miaka mitano.
Katika hatua nyingine Makamba amesema mbunge Ali Kessy japo ni mbunge wa CCM lakini hawakubali kauli aliotumia kuhusu Zanzibar na amewataka wabunge kutoa kauli ambazo zitaheshimu muungano. Pia Makamba amelisema suala la mgawanyo wa watumishi wa umma kwa pande mbili za muungano, vyanzo na mgawanyo wa mapato katika kuchangia shughuli za muungano na makubaliano mapya yanayoiruhusu Zanzibar kuweza kutafuta misaada yake yenyewe nje ya Tanzania.