China kuendelea kuisaidia Afrika kukabiliana na COVID-19

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,797
4,458
DC8EF951-F73D-4F14-9E03-8150D58072E3.jpeg

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi amesema, China itaendelea kuzisaidia nchi za Afrika kupambana na COVID-19, na kuchangia utekelezaji wa pendekezo la Kundi la nchi 20 la kukubali nchi maskini kuahirisha kulipa madeni. Vilevile China inafikiria kutoa msaada zaidi kwa nchi za Afrika zinazokabiliwa na shida kubwa.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mjini Beijing, waziri Wang amesisitiza kuwa Afrika ni ndugu wa China, na pande mbili zinashirikiana bega kwa bega katika kukabiliana na virusi vya Corona. Amekumbusha kuwa viongozi zaidi ya 50 wa nchi za Afrika waliipa China salamu na uungaji mkono, huku China ikituma timu za wataalamu wa afya barani Afrika, na madaktari wa China waliopo katika nchi 45 za Afrika wamekuwa wanashiriki kupambana na maambukizi, wakitoa mafunzo karibu 400 kwa madaktari na wauguzi wa Afrika. Vile vile Waafrika wanaoishi nchini China wamelindwa na kutunzwa vizuri, na mfano mzuri ni wanafunzi zaidi ya 3,000 wa Afrika walioko Wuhan wako salama, isipokuwa mmoja aliyepona baada ya kupata matibabu.

Bw. Wang Yi amekumbusha kuwa huu ni mwaka wa maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, FOCAC. Amesema uhusiano kati ya China na Afrika umeimarika baada ya kupita wakati wa dhiki. Mbali na hayo, waziri huyo aliahidi kuharakisha utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa FOCAC kuhusu ujenzi wa kituo cha kinga na udhibiti wa magonjwa cha Afrika. Kwa upande wa uchumi, China imeahidi kupanga ipasavyo miradi muhimu ya ushirikiano kati yake na Afrika, kusaidia nchi za Afrika ziweze kurejesha uzalishaji haraka iwezekanavyo.
 
Back
Top Bottom