China katika mipango ya kupiga marufuku magari yanayotumia mafuta

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
China ambaye ni nchi yenye soko kubwa zaidi la magari ina mipango ya kupiga marufuku uundaji na uuzaji wa magari yanayotumia mafuta ya diesel na petroli

Naibu waziri wa viwanda nchini humo alisema wameanaa utafiti lakini badoo hawajaamua ni lini marufuku hiyo itaanza kutekelezwa.

"Hatua hizo bila shaka zitalea mabadiliko makubwa katika sekta yetu ya magari," alisema Xin Guobin.

China iliunda magari milioni 28 mwaka uliopita, takriban thuluthi moja ya magari yote yaliyoundwa duniani.

Uingereza na Ufaransa tayari wametangaza mipango ya kupiga marufuku magari mapya yanayotumia mafuta ya diesel na petroli ifikapo mwaka 2040 kama sehemu ya njia za kuzuia uchafuzi wa hewa.

Kampuni ya kichina ya kuunda magari ya Volvo, ilisema mwezi Julai kuwa magari yake yatatumia umeme ifikapo mwaka 2019.

Makampuni mengine duniani yakiwemo Renault-Nissan, Ford na General Motors yote yanashughulikia mipango ya kuunda magari yanayotumia umeme.
 
Hii ni nzuri pia najiandaa kuwa na vituo vya kuchaji magari maana nahisi itakua kama simu tu unachaji na kubust technolojia hii itamuathiri mwarabu

"Never stop learning because life never stop teaching"
Naam! Fursa ya kiuchumi hiyo. Nadhani sehemu ya parking kutakuwa ndio charging centers..
 
Huu ujumbe uwafikie Jirani zetu wanaotaka vita kisa kugundulika mafuta Ziwa Nyasa..
 
Hayawezi kuathirika maana huo umeme unazalishwa na mafuta. Kitakachofanyika ni mahitaji makubwa ya mafuta kwenye mitambo ya umeme ili kuweza kuzalisha umeme wa kutumika kwenye magari.

Sijui kama umenielewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umeme siyo mpaka uzalishwe Kwa mafuta unaweza zalishwa Kwa njia y'a Jua au Upepo hapa inahitajika vilainishi (oil) tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwarabu atakuwa na hali mbaya sana maana ufahari na jeuri yao ni oil. By the way hivi OPEC na OIC zingalipo? Sijawasikia muda sasa.
 
Mwarabu atakuwa na hali mbaya sana maana ufahari na jeuri yao ni oil. By the way hivi OPEC na OIC zingalipo? Sijawasikia muda sasa.
Yes OPEC na OIC zipo ila kwa kua bei ya mafuta inayumba hata uimara wa hizo taasis umeyumba pia.unajua waarab walitegemea sana mafuta.hawakufikir itakuja siku mafuta yawe si kitu.mimi nafikir watarud kwenye yaleyale maisha yao ya kale..kuhamahama jangwani
 
Hii ni nzuri pia najiandaa kuwa na vituo vya kuchaji magari maana nahisi itakua kama simu tu unachaji na kubust technolojia hii itamuathiri mwarabu

"Never stop learning because life never stop teaching"
Usisahau Angola na Nigeria, Kenya, sijui kama na Tanzania bado yapo au zilikuwa story tu...

In short namuona mjukuu wangu akifaidi lita 1 kwa shilingi 100 akiwa na V12 moja ivi
 
Hii ni nzuri pia najiandaa kuwa na vituo vya kuchaji magari maana nahisi itakua kama simu tu unachaji na kubust technolojia hii itamuathiri mwarabu

"Never stop learning because life never stop teaching"
Au kituo betri inabadilishwa kama mtungi wa gesi. Unaacha lililoisha unachukua lililo full fasta na kutembea. Nilisiki changamoto ya hii teknoloji ni kuwa mabetri ni ghali sana kuunda na max yana last km 100 hivi. Kimjinimjini yatafaa sana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom