China inaithibitishia dunia kuwa njia za kisasa

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,000
1,019
1111111.jpg



Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC ulimalizika hivi karibuni mjini Beijing. “Njia ya China Kujiendeleza Kisasa” iliyotolewa kwenye Mkutano huo sio tu ilivunja mantiki ya baadhi ya nchi kwamba "usasa ndio mtindo wa kimagharibi”, bali pia inatoa njia mpya ya kujiendeleza kisasa. Njia ya China kujiendeleza kisasa sio tu ina sifa za kawaida za mambo ya kisasa ya nchi mbalimbali, pia ina sifa yake maalum kulingana na hali ya taifa la China.

Matokeo ya utafiti wa maoni uliofanywa hivi karibu ya vijana 4,700 wenye umri wa chini ya miaka 30 katika nchi 30 za mabara matano yalionyesha kuwa 84.7% ya waliohojiwa wanakubali kwamba njia ya maendeleo inapaswa kuendana na hali ya taifa, na kwamba hakuna mtindo mmoja wa kisasa unaofaa kila nchi. Kujiendeleza kisasa bila shaka ni matumaini ya binadamu wote, lakini nchi mbalimbali zina tofauti kubwa katika historia, tamaduni na idadi ya watu. Kwa upande wa China, watu bilioni 1.4 wakitaka kuendelea kisasa, ni changamoto kubwa kwa rasilimali na mazingira. Hii ndio sifa pekee ya taifa la China. Ndiyo maana kama China ikiiga mfano wa nchi za Magharibi kujiendeleza kisasa, labda tusiweze kuiona China ya leo.

Kuwawezesha watu bilioni 1.4 kuishi maisha bora, yaani, "ustawi wa pamoja", pia ni tofauti kati ya China na nchi za Magharibi. Ustawi haupaswi kuwa ni fursa ya tabaka fulani, na watu wote wanapaswa kushiriki katika mchakato wa kuijenga nchi kuwa ya kisasa na hatimaye kunufaika na matunda. Mwaka jana, China ilipata ushindi katika vita dhidi ya umaskini, na karibu watu milioni 100 maskini wa vijijini waliondokana na umaskini. Huu ni mfano bora ulio hai.

Katika baadhi ya nchi zilizoendelea, umuhimu wa vitu umesisitizwa kupita kiasi katika maendeleo ya kisasa, watu wamekuwa wachoyo, wabinafsi na wasiojali mbele ya pesa, na hata mifano ya kwenda kinyume na ubinadamu kama vile baadhi ya makundi kuhalalisha dawa za kulevya ili kujipatia faida imeibuka. Lakini njia ya China kujiendeleza kisasa inasisitiza maendeleo ya pamoja ya uchumi na roho. Katika miaka ya hivi karibuni, katika wimbi la utandawazi, China imefanikiwa kulinda na kuendeleza utamaduni wake bora wa jadi, hasa "upepo mkubwa wa tamaduni za jadi" umevuma mara kwa mara miongoni mwa vijana, na kufanya ustaarabu wa kiroho kuwa sehemu muhimu ya kisasa.

Hata hivyo, katika mchakato wa binadamu kutafuta maendeleo ya kisasa, hakuna nchi inayothubutu kusema kwamba maendeleo yake ya viwanda na ukuaji wa miji havijasababisha uharibifu wa mazingira na maliasili, na China pia ni mojawapo. Hata hivyo, katika miaka 10 iliyopita, chini ya dhana ya "maji safi na milima ya kijani ni mali yenye thamani kubwa", China imechukua hatua kadhaa ili kupunguza kasi ya uharibifu wa mazingira ya ikolojia, na kuwa nchi yenye ongezeko jipya kubwa zaidi la maeneo ya misitu duniani, na nchi ambayo hali ya hewa imeboreshwa kwa kiasi kubwa zaidi duniani. Kutambua kuishi kwa masikilizano kati ya binadamu na mazingira ya asili sio tu ni moja ya malengo ya njia ya China kujiendeleza kisasa, bali pia alama muhimu ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Mataifa mengi ya leo yaliyoendelea sana yamejiendeleza kuwa ya kisasa kupitia ukoloni, vita, na uporaji wa maliasili za mataifa mengine. Tabia hizo bado zinaendelea kuonyeshwa katika baadhi ya nchi kwa mfano Mashariki ya Kati, na kuleta maafa kwa nchi nyingi zinazoendelea. Lakini China haijawahi kuzusha vita kwa ajili ya maendeleo yake, wala haijavamia hata inchi moja ya ardhi ya nchi nyingine. Kwa sababu msingi wa mtindo wa kisasa wa Kichina ni maendeleo ya amani. Miaka 2,500 iliyopita, Confucius, mwanzilishi wa Falsafa ya Confucius, aliwahi kusema kwamba "amani ni kitu cha thamani zaidi" na "usiwafanyie wengine kile usichotaka kufanyiwa." Njia ya China kujiendeleza kisasa kwa amani imeandikwa katika DNA yake ya kitamaduni.

Baadhi ya nchi zimepata mafanikio kiasi kwa kufuata njia ya kisasa ya Magharibi, lakini pia zimeanguka katika changamoto kubwa kwa sababu ya kutoendana na hali zao halisi. Njia ya China ya kujiendeleza kisasa, haina maana kuwa nchi nyingine ziifuate China, lakini inachotueleza ni kuwa kama kila jamii ikiangalia hali halisi ya mazingira yake na kuwa na njia ya maendeleo inayoendana na mazingira yake, bila shaka inaweza kutoka jamii ya jadi na kuwa jamii ya kisasa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom