Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,807
- 11,969
Ahadi hiyo imetolewa leo Beijing na Mkurugenzi wa Afrika wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Nd.DAI Bing alipokutana na Mwenyekiti wa Mabalozi wa Nchi za SADC Nd. Mbelwa Kairuki
Katika kutekeleza ahadi hiyo- wiki ijayo Timu ya Madaktari Bingwa walioshiriki katika mapambano dhidi ya COVID19 nchini China itakwenda katika nchi mbili za SADC- Zimbabwe na DRC kwa ajili ya kukutana na madaktari wa nchi hizo kubadilishana uzoefu wa tiba ya COVID19.
Vilevile China itatuma awamu ya pili ya msaada wa vifaa Tiba kwa nchi zote za SADC.