#COVID19 China iko tayari kubeba jukumu la uongozi katika kuisaidia Afrika kufufuka baada ya janga la Covid-19

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,008
1,031
微信图片_20210430084936.jpg
Kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Mjumbe wa Taifa wa China na Waziri wa Mambo ya Nje Wang Yi amesema China inaona uwezo wa Afrika wa kusimamia COVID-19 ni muhimu katika kusaidia dunia kufufua biashara na uchumi wake.

Serikali ya China imesema Beijing inaiunga mkono Afrika kufufuka baada ya janga, huku lengo lake la awali likiwa ni upatikanaji wa chanjo kama “bidhaa umma”.

Bw. Wang, ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa baraza uliofanyika kwa njia ya video kuhusu Amani na Usalama katika Afrika, ametoa wito wa kupatikana chanjo kwa bei nafuu pamoja na uhamishaji wa teknolojia ili kusaidia bara la Afrika kulishinda janga hili.

“Kutuma msaada katika Afrika ni muhimu, lakini misaada pekee haitoshi kutatua suala la uhaba wa chanjo katika Afrika,” Bw. Wang alisema.

“Ni lazima tusaidie wenyeji waweze kutengeza chanjo katika Afrika, ingawa hili ni jambo gumu kutokana na viwango vya ukuaji wa viwanda.”

Umasikini wazidi Kukithiri

Kwenye mjadala wa wazi, Waziri wa Afya wa Kenya Mutahi Kagwe ambaye anaiwakilisha Kenya kama mjumbe asiye wa kudumu, alisema janga limezidisha umasikini barani Afrika, na kuonya kuwa inawezekana usiwepo utulivu. Hivyo ameliambia baraza kuwa mipango ya kufufua Afrika baada ya janga inapaswa kupewa kipaumbele kwenye uwekezaji wa ustawi wa watu, kuto ajira na uwekezaji kwa vijana.

Bw. Kagwe amewataka wajumbe kufadhili kituo cha Covax, kilichoundwa kwa ajili ya nchi masikini kupata chanjo, na kusamehe hakimiliki za ujuzi za chanjo hiyo ili kuwezesha utengezaji wa chanjo kuenea zaidi, ikiwemo katika Afrika.

Afrika ni bara ambalo halikuathirika sana na Covid-19, lakini wataalamu wamekuwa wakionya kwamba mfumo wake mbaya wa afya unaweza kuleta maafa makubwa kama bara hilo likitengwa kupatiwa chanjo ya kutosha.

China imeapa kutoa chanjo takriban kwa nchi 45 za Afrika ambapo imetiwa moyo na hatua ya Shirika la Afya Duniani kuidhinisha kwa matumizi ya dharura chanjo zake mbili - Sinovac na Sinopharm.

Pia imeipatia leseni serikali ya Misri ambayo itaruhusu kuanza kutengeza Sinovac kuanzia mwezi huu. Chini ya makubaliano, wanasayansi wa Misri pia watanufaika na mafunzo na kuungwa mkono kiteknolojia vitu ambavyo ni muhimu katika kutengeza chanjo.

Cairo na Abu Dhabi katika nchi za Falme za Kiarabu UAE, pia zitaruhusiwa kusambaza chanjo zake zilizotengenezwa nchini katika nchi za Mashariki ya Kati na Afrika.

Kutokuwepo kwa Usawa

Balozi wa China nchini Kenya Zhou Pingjian amesema China inaona upatikanaji wa chanjo ni hatua ya kwanza katika kupata ahueni, na kuongeza kuwa bara la Afrika litahitaji usaidizi kwenye maeneo mengine ambayo yamerudi nyuma kutokana na janga la corona. “Chanjo za Corona ni bidhaa ya umma na China inaunga mkono upatikanaji wake,” Zhou aliwaambia wanahabari.

“Mahitaji yetu ya nyumbabni ni makubwa, lakini tunajitahidi kuweka uwiano na mahitaji ya rafiki zetu wa Afrika. Kama mnavyofahamu, chanjo za China zimekuwa zikichunguzwa vikali lakini zimeonesha kwamba ziko salama kila mahali zinapotumiwa,” Aliongeza Zhou.

China mbayo ina kiasi cha watu bilioni1.4, imesema imewachanja takriban watu milioni 450 nchini. Na kampuni zake zimesema mwaka huu zitatengeneza dozi chini ya bilioni 3, ambapo chini ya uwezo wa sasa wa uzalishaji, umeilazimisha Beijing kushirikiana na watengenezaji wa nje.

Zhou amesema mipango ya uzalishaji haitakuwa ya njia moja, na kushauri kwamba China itaunga mkono watengezaji wa Afrika walio tayari kufanya kazi hiyo ya kuziba pengo.

Mpango wa Pamoja

Kwenye Baraza la Usalama, China imekuwa mstari wa mbele kujiunga na mpango wa pamoja na Umoja wa Afrika, unaojulikana kama "Mpango wa Ushirikiano wa kusaidia maendeleo ya Afrika".

Kwenye taarifa yake kwa baraza, Wang alisema nchi tajiri zinapaswa kuiunga mkono zaidi Afrika kwenye maeneo kama ya kupambana na janga, kufufuka baada ya janga, biashara na uwekezaji, msamaha wa madeni, usalama wa chakula, kuondoa umasikini, mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na ukuaji wa viwanda.

“Tunatakiwa kupeleka rasilimali pale zinapoohitajika zaidi katika Afrika na kuisaidia kuondokna na ugumu na kusonga mbele,” alisema Zhao Lijian, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China.
 
Corona imeshabaki mitandaoni tu uraiani tunapeta tu hatuna habari wala nini,hao rafiki zetu wachina waendelee kukaa kwa kutulia.
 
Tatizo lilianzia kwao,wameleta taaruki kubwa duniani,kutoa msaada itakua wajibu wao sio hisani
 
Back
Top Bottom